Sehemu za soko tarajiwa la Mwanjelwa linavyoonekana sasa

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya  Bw. Juma Iddi

SOKO jipya la Mwanjelwa lililoanza kujengwa Februari 25,2010 ujenzi wa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2012 ambapo ujenzi huo ulipaswa kukamilika Agosti 24,2011.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Iddi alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali na waandishi wa habari .

Mkurugenzi huyo amesema kuwa soko hilo likikamilika liatarajia kuondoa mlundikano wa wafanyabiashara katika masoko ya Sido na Soweto ambapo tangu juzi wafanyabiashara wa masoko hayo waligoma wakilalamikia kupanda kwa ushuru kwa zaidi ya asilimia 50.

Katika suala hilo la kupanda kwa gharama za ushuru kutoka Shilingi 200 kufikia shilingi 300 mpaka 500 kutegemeana na biashara yenyewe, amesema kuwa gharama hizo zipo kisheria na baraza la madiwani liliridhia lakini jana juzi na jana wamekaa na wafanyabiashara hao na kufikia makubaliano ya kulipa Sh 200-300

Amesema licha ya makubaliano hayo, wafanyabiashara wameendelea kugoma waishinikiza uboreshwaji wa miundombinu katika masoko hayo likiwemo soko la Sido ambalo ni chafu jambo ambalo ametolea ufafanuzi kuwa Jiji la Mbeya haliko tayari kufanya hivyo kwasababu masoko hayo 
si rasmi.

Ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanjelwa unatarajia kutumia Sh Bil 10 ambapo ukijumulisha na gharama za kibenki na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), gharama inafikia Sh bilioni 13. Kampuni ya Tanzania Building Works TBW ya Dar es Salaam ndiyo inajenga soko hilo. DESEMBA 2006 Soko  hilo la Mwanjelwa jijini Mbeya lililokuwa na ukubwa wa eka 4.7 liliteketea kwa moto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hilo soko inabidi watumie fire proof material bila hivyo bil 13 zitapotea kwa moto wa Mbeya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...