akiwa kwenye staili ya mishikio ya birika
 anasikitishaaaa jamaniiiii
Kilio cha nguvu uwanjani.

Mzee wa Libeneke naomba unitundikie hii mada.Kijana huyu aliondoka kwa nyodo kubwa kule Bwana la Maini kuwa hakuna viwango vya pasi kama vilivyo Chelsea.akaahidi kwa washabiki wa Chelsea wategemea kushangilia mabao tu.

akasema pasi za frank Lampard,Au Nicholas Anelka,au Michael Essien zitamfanya awe ana tundika nyavu kila mechi. hivi sasa wiki iliyopita ameomba Chelsea wamuongeze muda wa ziada wa mazoezi na afundishwe jinsi ya kufunga. jumamosi ndio kafanya madudu kabisa yeye na goli kapiga nje.

Mechi na Manchester alikosa goli kiasi cha mashabiki wa Manchester kumuonea huruma badala ya kumzomea.mashabiki wa chelsea wameanza kumuita mwizi kuwa awarudishie pesa zao.kijana hana raha kabisa.kiasi mechi za Chelsea na Wigan anaweza kula benchi kama bwana mkubwa Drogba yupo.

Pia kuna maneno kuwa ukienda Chelsea kuchukua namba ya Drogba ni vigumu kutokana na imani za ndumba na ngaye.

Tulitegemea kuwa kwa vile Drogba yuko kwenye Mashindano ya Africa basi Torres angeona nyavu.mechi ya juzi kiasi kocha wa Chelsea alie kwa Torres kukosa goli la wazi,jee ni laaana na maneno yake ya nyodo kwa Liverpool au ndio mambo ya Drogba?

Mdau Jongo wa kisiju toka Kimanzichana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Ndiyo maana katika mechi yao ya wikendi hii mtangazaji alimwita "misfiring Torres". Lol.

    ReplyDelete
  2. Mi nafikiri arudi kwao spain

    ReplyDelete
  3. wazungu si hawaamini uchawi, atoke hapo aende hata timu ndogo tu tuone kama atakuwa afungi, drogba nuksi kamkaanga mwenzie jamani.

    ReplyDelete
  4. Duhhh matokeo ya kudaia talaka, umepewa umeachika unakumbuka ulivyokuwa katika ndoa na kurudi huwezi!.....lol.

    ReplyDelete
  5. Ajaribu kucheza sinema,,,maana maisha ni kile chochote uwezacho na , ingawa kujitambua mwanzoni ni vigumu mtu huweza kuwa na vingi vipaji alivyozaliwa navyo!

    ReplyDelete
  6. KAFULIA NA HUYO AU ARUDI KWAO SPAIN AKACHEZE MOVIES ZA USHOGA . WEWE UNAFANYA MCHEZO NA DROGBA?

    ReplyDelete
  7. Dah! bongo kweli kwa mambo ya utamaduni hatujambo. Mnapeleka issue za uchawi wa simba na yanga hata kwenye ligi za ughaibuni. Kuna wachezaji wengi Premier league ambao hawafunngi magoli kama ilivyotarajiwa, mfano vipi kuhusu Andy Caroll (Liverpool)or Chamack(Asernal) Hawa nao wamelogwa na nani?

    ReplyDelete
  8. hakuna ndumba wala nini jamaa anasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia

    ReplyDelete
  9. Mimi nadhani kajimaliza mwenyewe wala hajalogwa na Drogba. Nimeangalia picha zote kwa makini na nimegundua kuwa huenda akili yake haipo uwanjani anawaza starehe tu. Kwa mtutumko ule wa bukta ni dhahiri hajapiga kiwalo cha ndani na anawaza mechi iishe ande kwa totoz!!!

    ReplyDelete
  10. Drogba atarudi kutoa ACN atakuta Torres hajafunga goli hata moja...haha

    ReplyDelete
  11. kwenye msimamo wa ligi nadhani chelsea ni wa 4 na deeperpool wa 7. Kwa hivyo basi inawezekana alikuwa sahihi kwamba viwango ni duni sana kwenye timu ya wabaguzi wa rangi.

    ReplyDelete
  12. lazima ashindwe maana ukiangalia sana hiyo picha ya kwanza... utaona "wrong parking"...inaelekea anawaza kwingine... totoz au?

    ReplyDelete
  13. Kamanda Drogba kamaliza wengi hakuna aliyekwenda Chelsea akadumu shivshenko.hakudumu.
    anayesema kuwa Ulaya hakuna uchawi basi yuko Ulimwengu mwingine wazungu wana wachawi registered na waganga jaribu ku google utaona.
    wazungu wanaroga sana.hata queen anashiriki kwenye mambo hayo.uliza history ya windsor.

    ReplyDelete
  14. ANDY Caroll na Chemakh si level ya Torres na mwenyewe Torres kakiri kuwa Liverpool kulikuwa kuzuri sana kwake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...