Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Jaji Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jana katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
Rais kikwete akimwapisha Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na makamishna wa Tume ya Uchaguzi
Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Jaji Mkuu Mh Mohamed Chande Othman na viongozi wapya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Rais Kikwete akiwa na makamishna wa Tume ya Maadili
Rais Kikwete akipozi na familia ya Jaji Damian Lubuva
Rais Kikwete akipozi na familia Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid
Makamu wa rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali akipozi na Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid na mkewe mama Ummy Hamid
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi akivishwa shada na Mh Hillary Mkatte
Rais Kikwete akipozi na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba pamoja na Jaji Damian Lubuva na wake zao
Rais Kikwete akiongea baada ya kuapisha viongozi hao wa tume
Hawa wazee waacheni wapumzike, mnataka wafie ofisini?
ReplyDeletemakamu wa mwenyekiti kageuza koti!!
ReplyDeleteHAPO NAONA UMEME HUA HAUKATIKI KWANINI ? HAO NDIO WATANZANIA PEKEE?
ReplyDeleteMDAU LONDON
Dunia nzima ni vijana ndio wanapewa madaraka ya uongozi lakini kwetu tanzania ni wazee sasa hao wakifariki nani atakuwa na experiense ya uongozi? Oneni mfano dunia nyingine hakuna viongozi wazee kiasi hicho wape VIJANA NAFASI
ReplyDeleteleed, UK
TUNAHITAJI TANZANIA MPYA , HAO WAZEE TANGU NYERERE YUPO MPAKA LEO SASA KULA MPAKA LINI ? BASI WAWAPE NAFASI ANGALAU WATOTO WAO.
ReplyDeleteTANZANIA INAENDA KUBAYA SANA WOTE HAO SIO ACTIVE NA OFISI. HUYO BABU AKIAMSHWA SAA TISA YA USIKU, KWELI ANAWEZA AMKA NA KUCHUKUA KAZI KIKAMILIFU?
MARA YA MWISHO HUYO KAFANYA MAZOEZI LINI YA MWILI ILI AKILI YAKE IWE ACTIVE ? SIDHANI HATA KAMA ANALIJUA GYM
LAKINI SAWA.
Vijana kama mambo yenyewe ndo haya mmekwisha!!when will you practice your carrier man!Wazee babu mpaka udondokee!
ReplyDeleteKuna maana gani ya kuwa na Universty,sijui school of law kama hawapewi kazi!!Mr. President give them chance they can!
jamani hivi vijana hawaaminiki kushika nyadhifa Tanzania?
ReplyDeleteWadau mmenena ukweli, hii hulka mbaya ya kujenga imani kuwa Vijana hawaaminiki, hawana uwezo wa Uongozi imepitwa na wakati!.
ReplyDeleteAchilia mbali huko nchi za mbali humu humu karibu na kwetu hakunaga mambo ya namna hii.
<<<<<<>>>>>>
Wakati yote haya yanajiri, vijana wabichi wahitimu wanatapatapa na makabrasha makwapani na machupa ya maji ya kunywa wakipoza njaa na kiu huku wakitafuta kazi!
<<<<<<<>>>>>>>
Huu ni utamaduni hatari kwa vile hawa wazee wanakufa na ujuzi wao vile hawachanganywi na vijana ili kuacha urithi, pia pana kuwa na mianya ya kitaaluma pindi vifo vinapotokea huku hakuna walionadaliwa kushika.
UWEZO WA UONGOZI UNATEGEMEANA NA UZIMA WA MWILI NA AKILI PIA, KWA VILE SAYANSI IMETHIBITISHA KUWA KUZEEKA KUNAPUNGUZA UWEZO WA KUFIKIRI NA KUMBUKUMBU!
SASA JE, NI AINA GANI YA UZALISHAJI WA UONGOZI (Umakini,Usimamizi thabiti, Maamuzi),UTATOLEWA NA MIILI NA AKILI ZILIZOCHOKA?
Jamani there is something about Momose Cheyo, he is very presentable, stylist old man. I love ( si kimapenzi jamani) John Momose Cheyo, his smile, the way he talks etc.
ReplyDeleteHawa Wazee maisha ya Mtaani hawayawezi, weweee kule kugumu usisikie omba usiwe Muajiriwa halafu Ukastaafu utakoma!
ReplyDeleteMita hazisomi, rada zina simama, zile bahasha za juu ya meza Ofisini kwa Mzee hakuna tena, labda uende banda la ngo'mbe huko uani ukachukue hesabu ya mauzo ya maziwa!
YAANI NI UOZO KWELI KWELI WAKATI WENGINE WANAENDELEA SISI TUNARUDI MWAKA 1975. JAMANI WATANZANIA TUAMKE NA SISI TUWE NA KAULI SIO KILA KITU HEWALA BWANA ! NO THIS IS TOO MUCH TO BE TRUE.WEWE RAIS MBONA UNAKUWA KAMA HUKWENDA SHULE? WEWE UNAKUJA HUKU ULAYA KILA SIKU NA UNAJIONEA MWENYEWE KILA KITU LIVE NA UNAFUNDISHWA NA MENGINE MENGI AMBAYO HUYAJUI LAKINI BADO HULETI LOLOTE LAKUJUVUNIA HUWEZI KUWA UNAWAAJIRI WATU TU AMBAO UNAWAFAHAMU TANGU WEWE NI MTOTO MDOGO. HAO WALIKUWA NI KAMA BABA ZAKO LAKINI BADO TU NUNAWANGANGANIA TU ? WAPE CHANCES NA VIJANA TUJIFUNZE MENGI HAKUNA URITHI UTAKAO ACHWA NA WAZEE HAO .HUSISHA BASI VIJANA NAO UONE LIBENEKE LAO. HAO WAZEE NI OLD FASSION NOW , LET THEM GO AND ENJOY THEIR PENSIONS, ENOUGH IS ENOUGH . TUNATAKA MAENDELEO SASA SIO KUJUANAJUANA TU HIO NCHI SIO YA FAMILI MOJA NI YA WATANZANIA MILIION46 NA WASOMI WALIOKUWA WENGI WENYE SIFA . HUYO MZEE HAWEZI LOLOTE LA UONGOZI SASA KUTOKANA NA UMRI WAKE HANA UWEZO WA FIKIRA THABITI NA NCHI ITAYUMBA TU . ONA BALAA LA AJALI ZA MABASI KILA SIKU TANZANIA, KWA SABABU HAKUNA UTAWALA NWA KISHUJAA NDIO MAANA TUNAZIDI KUFA KAMA KUKU KILA SIKU. KWANI KILA TAJIRI MWENYE BASI ANAMJUA KIONGOZI WA ZAMANI TANZANIA, AMBAYE ATAMPA KIBALI HATA KAMA BASI LAKE NI BOVU NA DEREVA WAKE ASIEKUWA NA UJUZI WA KUWASAFIRISHA ABIRIA(BINADAMU)
ReplyDeleteNA HAKUNA HATUA YOYOTE INAYOCHUKULIWA KWA UOZO HUO .
MDAU UJERUMANI.
kweli inatia huruma mambo yanayoendelea nchini kwetu angalia hapo kwenye sherehe unachoona ni vichwa vyeupe hamna hata kijani kama ni kijana basi huyo ni mlinzi Raisi anahitaji mabadiliko hachoki kuziona sura hizohizo kila wakati hamna changamoto kabisa mambo yale yale kama maji yanavyofwata bonde
ReplyDeleteShambani kugumu baada ya kustaafu!
ReplyDeleteUnamkuta Mzee alikuwa Mkuu wa Taasisi alikuwa anaongoza watu kibao tena Wasomi kama yeye,,,anafikisha kustaafu anarudi shambani kwake.
Kule anategemea miradi ya mauzo ya mayai, kuku, maziwa na mbuzi na ngo'mbe, anatumia muda mwingi kubishana na Shamba boi au Mmasai juu wa mauzo ya ndoo za maziwa mayai na kuku!
Wakati mwingine anapigwa mabao ya kiusanii na mjinga mjinga Shamba boi au Mmasai!
SASA LEO UNARUDI OFISINI ,DUHH INABIDI USHUKURU NA USALI KIMOYOMOYO!
AKIONDOKA YEYE MZEE SIUNAWAONA WATOTO...HAO NDIO WATAENDEELEZA...SASA SI UTAKUWA WIMBO ULE ULE JAMANI.
ReplyDeleteHahahah Mdau unanichekesha UJASIRIAMALI BAADA YA KUSTAAFU ni kazi kwelikweli!
ReplyDeleteUnakuta wakati mwningine Mmasai ameuza ndoo zote za Maziwa na hela amekunywa!!! yupo chakari amelewa!
Bosi nae alitegemea hela hiyo hiyo ajazie mafuta ktk gari na gharama zingine kwa wiki inayokuja!
Du ni lazima afanye Ibada baada ya kuitwa kurudi Ofisini!
Hongereni sana wazee tatizo vijana wa tz wanapenda madada sana wakipewa madaraka kama hayo ndiyo wanajiona washafika tena kila siku wanabadili machangudoa tuu na ofisi haiendeshwi hivyo basi bora wakae wazee watumie hekima zao. Vijana nyinyi msiwazeni ngono tuu mfanye kazi ili kuendeleza taifa lenu na si kusambaza ukimwi tuu.
ReplyDeleteMDAU UGHAIBUNI
Kazi baada ya Kusaafu kazi!
ReplyDeleteDu ama kweli kila kinyozi na kinyozi wake, sasa Mzee na elimu yako ulikuwa bosi unawawajibisha wenye elimu zao na wajanja, leo hii BAADA YA KUSTAAFU ukiwa Shambani kwako unabishana na Shamba boi ambaye labda ''hajaonana na daktari'' juu ya hesabu za mauzo ya ndoo za maziwa?
Mnhh kwa mtaji huu itabidi umshukuru Mungu kwa kurudi Ofisini!
Duhh hawa wazee wana bahati sana wenzao wastaafu lohhh wamepigika kweli huwezi amini!
ReplyDeleteMara nyingi watumishi Mashirika kama Benki, na Taasisi za Kiuendeshaji wanastahimili msoto na hekaheka wakitoka kazini vile akili zao zinakuwa hai wengi wanajishughulisha na miradi tokea wakiwa bado kazini, ila wa Serikali wanachoka sana wakiingia mashambani au mitaani kwa vile wengi walipokuwa kazini walibweteka akili wakawa wanaishi kwa wizi, mipango na rushwa!,
Vijana mnalalamika, well then come back home and do something, siyo midomo tu kutoka US, UK
ReplyDelete