Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo hilo lililopo Chakechake Lushoto jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasalimia na kuwaaga wasanii waliokuwa wakitoa burudani, wakati akiondoka Chakechake baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa mbogamboga, Juma Kambaga, kuhusu uzalishwaji wa mbogamboga hizo wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia chupa ya Juisi iliyotengenezwa na wajasiliamali, Salome Mtawa (kulia) wa kikundi cha Usambara Lishe Trust, wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkulima wa Nyanya, Judith Munis, wa Kikundi cha Upendo Jegestal, kuhusu kilimo cha nyanya, wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ex Khatibu BDHJanuary 28, 2012

    Hongera mh.Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luten mstaafu.Chiku Galawa kwa kusimamia maendeleo ya Taifa.Unafaa mama,tunakufahamu vizuri.Utakuja kuwa waziri nakuombea!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Sophia mjema,nakumbuka enzi zetu za upanga na harusi tulizosimamia pamoja,mungu akuzidishie nilikuwasijui kama umeingia serekalini nilidhani bado huko kwenye mambo ya compture wow ni muda mrefu sana almost 20 years hatujawasiliana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...