Watoto ambao hawakufahamika wanatoka sehemu gani katika mji wa mbinga wakiendelea kuvunja kuta za vibanda vilivyokuwa vikizunguka stend kuu ya mabasi wilayani humo kutokana na amri ya halmashauri hiyo kuvunja vibanda vyote vya biashara kupisha kuanza kwa ujenzi wa maghorofa kuzunguka stend hiyo.
Kijana huyo ambaye alikataa kutaja jina lake akiwa na mifuko ya vitunguu katika stand ya mabasi mjini mbinga wakati alipokuwa akitafuta wateja kama alivyokutwa na mpiga picha wetu mjini humo.
Akina mama wanaojishughulisha na uuzaji wa ndizi katika mitaa mbalimbali wilayani mbinga wakiwatafuta wateja kama wanavyoonekana pichani.
Moja kati ya mitaro iliyojengwa katika ya mji wa mbinga mkoani ruvuma ikiwa imeachwa wazi bila kufunikwa hali inayoweza kusababisha madhara makubwa hasa kwa watoto wadogo kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mbinga kama Kigoma vile(kibondo) kwa kuangalia picha.Kuna udongo mwekundu sana huko bwana Muhidin?Itabidi nije kutembea,Ruvuma ndiyo mkoa mmoja tu Tanzania bara ambao sijawahi kufika.Nauvutia pumzi...

    David V

    ReplyDelete
  2. Maghorofa Mbinga!

    Uwekezaji mwingine bwana wee acha tu!

    Sasa huyu mwekezaji ana maana gani kuwakwamisha wajasiriamali kwa kuwavunjia Vibanda vyao vya biashara kwa nini asitafute njia ingine kufikia lengo lake ikiwa yeye anazo pesa?

    ReplyDelete
  3. haya huyu kijana atakikutaja jina lakini auze sura pumbavu kweli.

    ReplyDelete
  4. Go mbinga go! wamachinga kama kazi saafi sana 10,000 thumbs up........haya mambo ya kusema wamachinga wapigwe marufuku hayana maana

    ReplyDelete
  5. Sasa ataje jina lake ili iweje?...yeye ana privacy policy zake na moja ndo hiyo hataki kutaja jina lake ,hataki amekataa.....na wewe unaprivacy policy zako unajifanya anonym ili utukane watu wanaohangaika kutafuta maisha basi tunaheshimu privacy policy zako kama tuvyoheshimu za huyo kijana

    ReplyDelete
  6. apo kwenye mitaro kaka umechemsha...sasa iyo mitaro ikifunikwa kote ikiziba, itazibuliwaje?? si wameweka vivuko au uyo mtoto atayedumbukia kipofu hataona madaraja hayo.....nilizani utasifia usafi wa mitaro...kama hamna maneno ya kuelezea hali halisi ya picha jamani msipotoshe wananchi...

    mdau mbinga-mbinguni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...