Mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya ya Songea Bi Beatrice Mshimizi akijibu kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Magagura jana wakati wa mkutano wa kamati ya pembejeo na mkuu wa mkoa wa Ruuvuma Said Mwambungu wa pili kulia,wa pili kushoto ni mkuu wa wilaya Songea Roy Thoms Sabaya,
Askari polisi ambaye hakufahamika jina lake,kulia akimsaidia mkuu wa mkoa wa Ruvuma kumzuia asinyeshewe mvua alipokuwa akitoka ndani ya ukumbi wa kanisa katika kijiji cha Mgazini songea vijijini ambapo haya hivyo Mkuu huyo wa mkoa alishindwa kuongea na wananchi kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Roy Thoms Sabaya wa tatu kushoto akimuongoza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kwenda kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Luhagara songea vijijini ,wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya hiyo Beatrice mshomizi,
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Muungano Zomba halmshauri ya wilaya songea.
Baadhi ya wazee wa kijiji cha Muungano Zomba Edwin Mwingira(80) na Mzee Method Soko(74) wakifuatilia kwa makini taarifa ya ugawaji wa vocha za kilimo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya songea Roy Thoms Sabaya jana kijijini hapo,
Mama ambaye hakufahamika jina lake mara moja wa pili kushoto akimlalamikia jambo mkuu wa Mkoa wa Ruvuma MH SAID MWAMBUNGU wa kwanza kulia katika kijiji cha Muungano Zomba Songea vijijini,wa pili kulia ni mkuu wa wilaya ya songea Roy sabaya.
Baadhi ya akina mama wa kijiji cha Mgazini songea vijijini wakimikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu,hayupo picha ni wakati wa ziara ya mkuu huyo wa mkoa kukagua miradi ya maendeleo na kufuatilia ugawaji wa vocha za kilimo.PICHA NA MUHIDIN AMRI
Viongozi wa Bongo shida kweli kweli. Angalia picha ya RC Mwambungu alivyoshikiwa mwavuli na huyo askari mrembo! Hivi kweli Mwambungu mwenyewe asingeweza kuushika mwavuli huo? Mbona Juzi JK alikuwa Morogoro na akashika mwavuli mwenyewe? Ama kweli, wabongo kwa kutaka makubwa, hatujambo!!!!
ReplyDeleteHivi unajisikiaje kiongozi wako anapokuja kuongea na wewe akiwa na maaskari (tena waliojiandaa vilivyo)? Hivi anakuwa anamaanisha kuwa wewe ni mhalifu tu na si lolote au yeye ni mlaghai na anaweza kushambuliwa wakati wowote?
ReplyDeleteUstadhi Muhidin jitahidi upate jina la huyo na contacts kama bado yuko singo
ReplyDeleteDavid V
Huwezi amini sura hizi za kukata tamaa ya maisha ,wawakilishi wa matatizo yao wanataka ongezeko la posho kwa kigezo cha maisha magumu dodoma.
ReplyDeleteNaomba namba ya simu ya huyo afande aliyeshika mwavuli.
ReplyDelete