Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akiteta jambo na viongozi wa dini ya kiislamu.
 Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akizungumza na viongozi wa dini ya kiislamu mkoa wa Kilimanjaro(hawako pichani)
 Sheakh wa wilaya ya Siha ,Sheakh Mlewa akichangia hoja katika mkutano wa viongozi wa dini ya kiislamu na mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo.
 Meya wa manispaa ya Moshi Jafary Michael akizungumza katika mkutano na viongozi wa dini ya kiislamu mkoa wa Kilimanjaro(hawako pichani).
Viongozi wa dini ya kiislamu mkoa wa Kilimanjaro.


Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi .

WAKATI serikali ikiwa imeshatoa msimamo wake juu ya suala la Mahakama ya kadhi,Mbunge wa Moshi mjini(CHADEMA),Philemon Ndesamburo ameahidi kusimama kidete kutetea waumini wa kiislamu kuitaka serikali kuanzisha mahakama hiyo.

Ndesamburo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika hotel ya Keys mjini hapa wakati akizungumza na waumini wa kiislamu ikiwa ni sehemu ya mipango yake kusikiliza na kujadiliana na makundi hayo kuisadia jamii 
katika masuala mbalimbali.

Alisema haoni sababu kwa serikali kukataa kuanzishwa kwa mahakama hiyo ikiwa wameweza kutenga mabilioni ya fedha kuendesha vyama vya siasa na masuala mengine yasiyo na tija kwa maendeleo ya taifa.

“Kama mbunge wenu sioni sababu ya serikali kukataa kuanzisha mahakama ya kadhi, waislamu wana masuala yao ambayo wangependa kuyashughulikia….wakati ikikataa kufanya hivyo serikali hii hii inatenga mabilioni kuendesha vyama vya siasa”alisema.

Ndesamburo aliitaka serikali katika kutenda haki dhidi ya waumini hao ni vyema ikaandaa bajeti kila mwaka kati ya Bil 2 hadi 3 kwa ajili ya Waislamu na wakikristo ili  kuendesha masuala yao kulingana na mipango wanayojiwekea.

“Serikali yetu haina dini, mimi sitetei kundi moja lipewe na lingine liachwe, wote wapewe fungu fulani la fedha kuendesha mambo yao ili mradi wasikiuke katiba ya nchi …hii itasaidia kuondoa misuguano isiyo ya lazima”alisema.

Alisema madhehebu ya dini yamekuwa yakihudumia watanzania kiroho na kimwili kwa kuanzisha miradi mingi ya maendeleo ikiwamo ya Elimu,Afya, Maji na Kilimo ingawa baadhi ya masuala yalipaswa kutekelezwa na 
serikali.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake , mmoja wa wajumbe wa waumini wa kiislamu mkoani Kilimanjaro, Shekh Mlewa kutoka wilayani Siha alimtaka Mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema mkoani humo kufuta 
dhana iliyojengeka kuwa chama hicho ni cha kikristo.

Alisema dhana ya kwamba chama hicho ni cha kikristo inafuatia chama hicho kutotoa tamko lolote wakati rais Jakaya Kikwete alipotoa msimamo wa serikali kwamba haitaweza kuunda mahakama hiyo bali ni jukumu la 
waislamu wenyewe.

Mapema mwaka jana akizungumza na waislamu katika baraza la Idd El Fitri lililofanyika Septemba mosi mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema Serikali haitaanzisha Mahakama ya Kadhi na kwamba badala yake Waislamu 
 wenyewe ndiyo waanzishe mahakama hiyo.

Pamoja na kauli hiyo lakini pia rais alisema Mahakama ya Kadhi haitowekwa ndani ya katiba jambo ambalo lililalamikiwa na baadhi ya waumini wa kiislamu.

Aidha waumini hao walisema kutokuwekwa kwa suala hilo katika katiba litasababisha kutokuwa na nguvu kama  ilivyo kwa mabaraza ya Kiisilamu ambayo yamesajiliwa kwa utaratibu wa kawaida lakini hayana uwezo wa 
kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ya ngoswe mwachie ngoswe!...usitake umaarufu bana!

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa anaanza kulewa sifa! hamna mtu anayewakataza Waislam kuwa na mahakama ya Kadhi ila mambo ya serikali kuendesha hiyo mahakama yao ya masuala ya Dini ni NO and BIG NO!

    ReplyDelete
  3. tukianzisha mahakama ya kadhi tunaomba serekali wasituingilie wala wasilete fitna zao. Najua hapa kinachowafanya wasite ni posho kwa kitengo hicho. naamini kama waislam wenyewe bila ya kuingiliwa wala kuekewa longolongo tunaweza kuendelea.

    ReplyDelete
  4. OOngereni sana viongozi kwa uwongozi wenu bora,,,,mko neutral!Inapendeza hiyo jamani!
    Ahlam ,,,UK

    ReplyDelete
  5. Mhe. Ndesamburo anaanza kukosa mwelekeo. Kama anakubali kuwa serikali haina dini kwa nini ailazimishe serikali kuanzisha Mahakama ya Kadhi? Mhe Ndesamburo kama alivyosema mdau wa kwanza "Ya Ngoswe mwachie Ngoswe". Waache waanzishe mahakama yao kwa kufuata taratibu zilizokubalika. Usiilazimishe serikali kufanya mambo unayofikiria wewe ni sahihi. Suala la serikali kutumia mabilioni kwa vyama vya siasa ni pamoja na chama chako na ni utaratibu wa siku nyingi. Kwa nini leo aanze kuona kuwa pesa zinatumika vibaya. Mbona hazungumzii posho wanazolipwa bungeni au fedha anazopewa mbunge kwa kununulia mafuta ya gari lake? Mheshimiwa usiligeuze suala hili likawa ngazi ya kupandia juu kisiasa. Lakini Mheshimiwa anaona mbali (2015). Na serikali basi angeishauri ikawa na mikakati ya walau miaka 50 ijayo. Hapo tutasonga mbele.

    ReplyDelete
  6. Safi sana mze ndesa pesa hapo nimekuunga mkono kama umeliona hilo, maana watu wanaikataa mahakama ya kadhi kwa chuki tu bila sababu yoyote ya msingi. Kwa sheria zilizopo ikifanyika mirathi ya kiislamu mara nyingi mahakama huwaita masheikh kufafanua sheria hizo kwakua inazitambua. sasa tabu yote hiyo ya nini kwanini kisiwepo tu kitengo cha kuisaidia jamii hiyo?mbona ktk nchi nyengine inafanyika hiyo kama vile Uganda na hatujasikia kama kuna tatizo lolote kwa wasiokua waislamu? mi naona kunawakati ukweli utajidhihirisha wenyewe na hasa watatoka watu wa kuutetea kutoka hukohuko ktk kundi la wapingaji.

    ReplyDelete
  7. Hongera muheshimiwa Ndesamburo. Sijui hayo uliyoyasema ni msimamo wa chama chako au msimamo wako mwenyewe?. Lakini napenda nikukumbushe kua serikali tayari inatoa ruzuku kwa dini ya kikiristo kupitia MOU (memorendum of understanding).

    ReplyDelete
  8. Hivi ubaya wa kuendesha mahakama ya kadhi kwa kodi za wananchi ni nini au Waislam siyo katika hao wanachi?

    ReplyDelete
  9. Hivi wewe unaesema kulewa sifa unamaanisha kitu gani haswa.Tatizo ni nini hapa kwani.Kwanini nyinyi wakristo mnaubaguzi sana na kujifanya hii nchi ipo chini ya mikono yenu.Kwanini mampendi haki itendeke ktk nchi hii?Angalieni hii nchi ilipofika sasa umasikini mtupu kwa ubaguzi wenu.Itafika siku hapa machafuko yatatokea na hakuna atakaeweza kushusha pumzi.Hao mnaowafuata wote watapanda ndege wakimbilie majuu halafu sie masikini tuchinjane.Yote ya nini haya jamani.Simpo tu kila dini ipate haki yake.Na kila kiongozi akamate wauza unga na mafisadi full stop.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...