Mjalojia mkuu wa kampuni ya Mantra Tanzania,Emauel Nyamsika (aliyeinama) akiwaonesha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Ruvuma,wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo,Mh. Said Mwambungu (wa nne kulia) ramani maalumu inayoonesha maeneo yote yenye madini ya uran katika mto mkuju wilayani Namtumbo jana.
Mjalojia mkuu wa kampuni ya Mantra Tanzani ltd,Emanuel Nyamsika akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu kipande mojawapo cha madini ya uran yaliyogundulika katika pori la hifadhi ya taifa ya Selou wilaya ya namtumbo mkoni humo.
Mkuu wa utambuzi na usalama wa jeshi la kujenga taifa (jkt) luten kanal Malembo akitoa salamu za mkuu wa JKT,Meja Jeneral Samuel Kitundu wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi ya miezi sita kwa vijana waliojiunga na jeshi Hilo kikosi cha 842 KJ mlale JKT hivi karibuni,katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Songea,Roy Thomas Sabaya na kushoto ni Mkuu wa Brigedi ya 401KV,Kanal John Marwa Chacha.
Afisa Mahusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania,Bernad Mihayo (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma walipotembelea katika mgodi wa madini ya uran juzi,kwa ajili ya kuona shughuli zinazofanyika katika mgodi huo.
Baadhi ya watendaji wa kampuni ya mantra tanzania ltd inayojishughulisha na utafiti wa madini ya uran katika mto mkuju wilaya ya namtumbo Mkoani Ruvuma,Emanuel Nyamsika kulia,Bernad Mihayo,wa pili kutoka kulia na afisa mazingira wa kampuni hiyo Johnnie Ntukura wa kwanza kushoto wakimuongoza mkuu wa mkoa wa Ruvuma wa tatu kulia mwenye kaunda suti kuangalia maeneo yaliyogundulika kuwa na madini ya uran katika mto mkuju wilayani namtumbo jana, wa pili kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo savery maketta.
Luten Jackson Otaite wa kikosi cha 842kj mlale jkt akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw Said Mwambungu kikosini hapo kwa ajili ya kufunga mafunzo ya kijeshi ya miezi sita kwa vijana zaidi ya 822.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw Said Mwambungu, akisalimiana na mkuu wa utambuzi na usalama wa jeshi la kujenga taifa makao makuu luten kanal Malembo katika ofisi za kikosi cha 842kj mlale jkt mkoani humo,katikati ni mkuu wa brigedi ya 401 KV John Marwa Chacha.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kijumla mimi binafsi wanajeshi nawapenda sana kuliko usione wakati mwingine mambo yanajitokeza kuwapiga watu au kuonyesha ujeuri fulani lakini ni watu wenye nidhamu wenye juhudi ya kufanya kazi katika mazingira yeyote

    ReplyDelete
  2. Emma nakuona mkuu unashusha nondo za Exploration na Mining Geology.Hongera sana kwa nafasi yako mpya hiyo.Tuko pamoja mzee.

    Ni mimi rafiki yako tuliyekuwa wote Ashantigoldfields,Nyankanga, 1997-1999!

    ReplyDelete
  3. Kaka Johnnie Ntukula,
    Naona Watanzania sasa tumejaribu na tunaweza kushika nafasi za juu katka makampuni haya ya kigeni...Kaka Hongera sana. Ankal Michuzi huyu jamaa Johnnie Ntukula ni Environmental Manager (Meneja wa Mazingira na sio afisa wa mazingira)mpe haki yake tafadhali. Hongera WATZ!

    ReplyDelete
  4. Hivi kwenye hili suala la madini lazima wazungu wawemo!?

    ReplyDelete
  5. He he hehe uh!! Wao wazungu ndio wenye matumizi nayo na thamani nayo sisi tunawafanyia kazi tu na kuwahifadhia ktk ardhi ambayo pia ni ya kwao mwe.."wawekezaji"

    ReplyDelete
  6. JAMANI MAKENI UTAJIRI WETU WANAUSIMAMIA WAZUNGUU

    ReplyDelete
  7. Haya madubwana Madini ya NYUKLIA yana madhara makubwa sana kwa binaadamu hasa hao wakazi wa Nantumbo.

    Ni muhimu huyo mwekezaji MANTRA zaidi ya faida ya kibiashara atakayopata ahakikishie usalama wa afya za watu ,usalama na mazingira ya eneo!

    ReplyDelete
  8. Johnie long time kumbe uko huku siku hizi, hongera kaka

    Serenge
    college mate UDSM 1994

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...