Ankaal na wadau wote Assalaam Alaykum,

Ndugu zangu naomba msaada kwa haya nayowaeleza mpate kunijuza yawezekana kuna mwenye ufahamu wa hili.

Mwezi Oktoba niliagiza gari toka nchini Japan,gari aina ya Toyota Premio kupitia Kampuni la NOBA INTERNATIONAL na kwa bahati nzuri nilipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa hii Kampuni.

Na hatimaye NOBA INTERNATIONAL akamkabidhi nyaraka zote wakala wa usafirishaji KNOT GLOBL CO.LTD pia ya Japan,nyaraka hizi ni pamoja na ORIGINAL BILL OF LADING Na.12004007203.Kwa masikitiko baada ya hatua zote za kutaka kumalizia kutoa gari yangu bandarini pamoja na kulipa gharama zenye kujumuisha Freight na Delivery Order Fees, 

nimeambiwa na wakala wa Meli wa INCHCAPE SHIPPING SERVICES kuwa napaswa kuwa na Original Bill of Lading na nilipowasiliana na Shipper pamoja na Agent wa huko Japan niliambiwa kuwa Original Bill of Lading imepotea na napaswa kuwasiliana na INCHCAPE Japan (MOL) na pamoja na kufanya hivyo nikaambiwa na hao MOL niwatumie Affidavit toka Court ya Tanzania na tarehe 18/01/2012 nilipata Affidavit na kuituma MOL Japan,

Inchcape Tanzania na kwa Wakala wa Japan,Knot Global,lakini mpaka leo nimeendelea kusafa kupata haki yangu.Ni zaidi ya miezi Mitatu sasa nahaha kupata kutoa kwa wakati stahili gari hiyo.Sasa nilipofuatilia utaratibu wa malipo ya ICD nikaarifiwa nitalipa takriban USD 2300 mpaka leo zikiwa ni Storage tu.

Na kunaa dalili nitaendelea kuumia zaidi mpaka itakapopatikana hiyo Original Bill of Lading ama hawa Ichcape Shipping Services au MOL JAPAN ama huyo wakala KNOT GLOBAL LTD ambaye mara zote nimekuwa nawasiliana nae hanipi taarifa za msingi.

Wadau naomba msaada wa mawazo mnisaidie nipate haki yangu,ninaamini hapa mtandaoni kuna watu wenye uzoefu watakaoweza kunisaidia niondokane na kadhia hii.

Wabillah Tawfiq
Mdau Jamaal Hassan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Jamaal pole sana ndugu yangu kwakweli dunia sasa hivi niyaujanjaujanja na yote haya yanakuja kutokana na serikali zetu hazina vyombo vya usalama wenyeuaminifu!Hiyo deal kaka inawezekana kwamba hiyo gari ulioletewa niyawizi imechongwa bil ya mtu mwengine sasa wewe huwezi kupata original na kama kuna uhalali hapo wao hao waliopoteza kisharia wakulipe mapesa mengi sana ninakushauri lipeleke swala hili kwa mwanasheria!Kukwambia hiyo gari niyawizi nafikiri umeshasikia hata england yameibiwa magari mengi sana na jamaa wengi wako ndani linaibiwa gari linatiwa kwenyecontena usiku asubuhi inachongwa bil kwahiyo kaka wewe haki yako ukiikosa hapo utaikuta mbele!Pole sana kaka!

    ReplyDelete
  2. nakuonea huruma ila ndo ushalizwa hivooo.

    ReplyDelete
  3. Msaada wangu kwako ni POLE maana ulishaliwa. Angalia usitaarabu mwingine maana hiyo gari is no worth it.

    ReplyDelete
  4. Pole, siku nyingine uwe unaagiza gari kutoka kwenye makampuni yanayoeleweka,haya mambo ya kutaka 'vya bei ndogo' angalia sana ustadhi.Wadau watakupa ushauri zaidi.

    ReplyDelete
  5. Noba international ltd is the only dealer you can trust.we export used japanese vehicles world wide.membership in many auto auctions in Japan include internet.for your need.feel free to contact us

    ReplyDelete
  6. Ilete na jamiiforums,nako utapata msaada vilevile,wapo na wausika kule

    ReplyDelete
  7. Nimesoma habari yako,nimesikitika sana,,Ila mimi sina ushauri wowote kwa mambo hayo ya magari,,Ila wanaojuwa zaidi wakusaidie mawazo ili upate haki yako,,,Ama kwa nini usishitaki kwa wakuu wanaohusika,,ili upewe haki yako au urudishiwe pesa yako na gharama zako zote?Hawa watu wanakupotezea muda,,mbona nimeona kuna kampuni nyingine inaagiza magari hapo Dar?Ukidai haki yako deal na hao,,,Pole sana!!!Ahlam UK

    ReplyDelete
  8. Kwa ufupi umeshaibiwa. Gari itabidi uisamehe!!

    ReplyDelete
  9. Pole sana ndugu,Jamaal Hassan.Kwanza nikupe hongera kwa yote uliyojitahidi kufanya,ningekushauri uliuzie bandarini ila pia hutopata haki yakeo kwani halina docuement mhimu.Pia ni vema kujua Document hiyo ilipotelea wapi,Tanzania au Japan na kisha nakushauri ufuatilie kwa wanasheria hapo Dar-es-salaam na hasa wale wa law of contarct au Business law watakupatia ushauri wa kisheria zaidi ili kujua uwasiliane na nani.
    Japo pia ni vema ukatinga ubarozi wa Japani ili kuapata msaada wa haraka.
    Pole sana

    ReplyDelete
  10. wawekee lawyer hao mwenye kujua sheria za biashara kila kitu watalipa wao,sio makosa yako kwahiyo angalia wasikuzidi maarifa

    ReplyDelete
  11. Ndugu Jamaal, pole sana. Mimi naishi Japan na nauza magari Afrika. Kama kampuni hio imesajiliwa hapa, basi ni rahisi kupata haki yako haraka. Kama haijasajiliwa na ni ya mtu binafsi , ana internet tu, basi umeibiwa.

    Kitu muhimu wadau ni kijua kampuni imesajiliwa na ina PAY TRADE status, maana kama huna gari mkononi pesa yako haipotei. Kama makampuni ya internet wanatumia PAY TRADE, hawapati peza zao mpaka mteja anapokee agari. Pia nununua gari pamoja na insurance, sio ghali, chini ya mia dola.

    Ukitaka info zaidi angalia kampuni hizi:

    http://www.tradecarview.com

    Mdau,
    Tokyo

    ReplyDelete
  12. wasije kuwa WANAIJERIA wamekuliza wakijidai ni hiyo kampuni. so sorrymy dear

    ReplyDelete
  13. Pole kaka,ila kuna utata fulani kwenye haya maelezo..umenunua gari kwa hao noba japan,sasa baada ya wao kusafirisha gari lako kwanini hawakutuma original docmnts kwako kwa dhl au fedex..kazi ya huyo shipn agent sio kukutumia wewe docmts..hao noba jp hawakwambii ukweli kaka,wamekupiga changa la uso..baada ya gari lako kuondoka jp walitakiwa wakutumie docmts wewe..kama utaamua kutafuta clearing agent bongo ni chaguo lako...au wewe ndie uliwaambia wawape hao knot global docmts zako kama ma-agent wako?jina lenyewe ni`knot´ maana yake mwenyewe unaijua,kitanzi kaka...pole sana

    ReplyDelete
  14. Nakushauri ndugu yangu uende mara moja ubalozi wa japan ili wakupe ushauri kuhusu hao mabwana halafu process zote zitaanzia hapo nenda mara moja usipoteze muda mungu atakusaidia ishu ndogo sana hiyo

    ReplyDelete
  15. Alaykum Salaam,

    Sheikh Jamaal pole sana ndugu yetu, hii ni matokeo ya Makampuni kuendesha mambo kama wanavyotaka huku wakitumia Rushwa kufikia malengo!.

    Mamlaka kama hiyo Mahakama Kuu iliyotoa AFFIDAVIT kukupa wewe zinatakiwa kuwawajibisha hao Wajapani INCHCAPE SHIPPING SERVICES na hao KNOT GLOBAL LTD. kwa kuwa hawawezi kufanya kazi na Tanzania bila Mkataba na utaatibu wa kufanya kazi!

    ReplyDelete
  16. Kuna information zinamiss hapa, hizo original documentszilipotea vipi? kama ni shipper alipoteza mbona huwa wanabaki na copy of the original moja, ambayo inaweza kupokelewa kama imetoka kwa shipper, kwa hiyo anayeweza kukusaidia ni shipper tu hakuna mwingine, maaana wanaogopa wakitoa gari halafu akaja mtu ana original BL watafanya nini? kuthibitisha kuwa wewe ndiye fulani haitoshi maana unaweza weka BL bond kwenye loan halafu ukadefault na aliyeweka bond akaja ku claim mali yake na original BL, mimi ilinitokea ilibidi nilipe deposit ya thamani ya gari kma premio ulinunua $2800, unalipa tena kwa shipper ili wakutumie docs. zingine unatoa gari yako, hiyo pesa uliyoweka deposit utarudishiwawithin 12 Months kama hakuna mtu mwingine atatokea na original BL, kwa hiyo na options 2, ulipie tena gari hiyo hiyo with a refund in 12 Months au usamehe gari maana storage tu inakaribia bei ya gari, mtu yeyote asikudanganye, anyekwambia uende kwa mwanasheria, mimi yalinitokea hayo na ni mwanasheria/advocate. ukitaka kufahamu zaidi chukua BL uisome pale nyuma terms na conditions utaelewa vizuri haya ninayokwambia, sasa hili liwe ni fundisho kwa wengine BL ndio gari, ukiipoteza jua umepoteza gari FULL STOP.

    ReplyDelete
  17. Hassan, kwanza ni kwa nini Noba International alipitisha BL kwa consolidator (Knot Global)? Alikuwa anaokoa gharama gani kwa gari moja? Nashauri deal na na shipper aliyekuuzia gari, ni jukumu lake akukabidhi documents original. Alafu kwa nini ulipeleka affidavit wakati docs hukupoteza wewe aliyepoteza ndo alitakiwa kuapa sio wewe. Nashauri Noba ndo ambane knot global pia forwad bill ya storage kwao if possible involve lawyers wakikataa waambie utawaaribia jina.

    ReplyDelete
  18. pole sana mzee kwa yaliyokukuta. nijuavyo mm ni kwamba kampuni ulionunulia gari ndio inapaswa kukutumia wewe uliyenunua gari original BILL OF LADING na sio kumpa msafirishaji. Hii mimi sijaielewa, Kama NOBA ni kampuni makini kwanin wasijue namna ya kutuma bill of lading kwa mteja wao? mm nilishawahi na bado naagiza magari toka Japan ila hua napata original bill of lading toka kwa muuzaji. ninawasiwasi na uzoefu wa hiyo kampuni uliyonunulia gari. pole sana.

    ReplyDelete
  19. Nenda Ubalozi wa JAPAN haraka sana utapata msaada, ukizinguliwa na uende na waandishi wa habari next tym huwa wanaogopa sana kashfa kwa media. Am sure utapata zaidi ya hicho.

    ReplyDelete
  20. Pole sana mkuu,ila kwa ushauri tu nikuwa Kwanza aliyekuuzia gari NOBA sijui ndie alitakiwa kukutumia document zije kwako so kumpa mtu mwingine ni ubabaishaji,pili hao Inchcape hawakutakiwa kupokea shipping agency fee bila kuwa na original document coz wanapopokea hizo hela wanatoa delivery order amabayo inatoa ruhusa kwa bandari kukukabidhi gari yako. Unless unaniambia kuwa haukutumiwa Document za gari ambazo huwa ni invoice original,Inspection certificate original pamoja na hizo Bill of lading Original mbili na copy nne. Kama ulipokea hizo document ndipo uliweza kufanya process za Customs otherwise isingewezekana,na kama haukuopokea hizo document basi pole sana piga moyo konde hilo gari halipo tena.

    ReplyDelete
  21. jaribu kwenda SUMATRA uone kama unaweza kupata msaada maana wao pia ni wadhibiti wa usafirishaji majini pia ndio wanaotoa leseni kwa hao shipping agency

    ReplyDelete
  22. wadau wengi nathani hawajaelewa nini mdau analalamika. Mdau kapoteza original bill of lading na ukipoteza OBL sheria ya MOL ambaye ni principle na inchcape ni agent ni kwamba, unadeposit 150% CIF value. ndio uweze kupata release. cha msingi weka mawasiliano yako.
    mdau

    ReplyDelete
  23. mie sinunui tena gari kutoka japan kwa sababu asilimia 90 ya wanaoagiza wanatapeliwa! utapeli mtupu! wafanyabiashara wa magari japan wote ni matapeli wa kutupa!

    ReplyDelete
  24. Wacha wizi na we mdau wa carview..paytrade kitu gani..kama mnawajali watu si mzifute kampuni zote feki zinazojitangaza kwenye mtandao wenu?mnapokea hela kutoka kwenye kampuni kujitangaza humo,hamjui kama zinawaibia watu?mnajidai wadhamini halafu mnaziachia humo ili watu wakitapeliwa mseme kwa vile hawakutumia hiyo paytrade..kila gari mnakula sio chini ya dola 150,unafikiri ni ndogo..hukawii kukuta nahao noba japan wanajitangaza humo kwenye mtandao wenu

    ReplyDelete
  25. Kununua gari direct toka japan ni rahisi kwa maana ya gharama ukifananisha na kununua toka showroom ukizingatia magari mengi ya show room za hapa ni toka dubai ambayo yametumika sana. Ila angalizo linalotakiwa hapa ni kununua toka kwenye mitandao inayoamika ambayo watu washapata magari bila usumbufu.
    Shekhe wangu pole kwa hilo, usiangalie sana bei ya gari unapotaka kununua gari toka japan.mimi binafsi nimeagiza gari tatu kwa nyakati tifauti toka autorec na jamaa wananiambia ratiba yote ya gari mpaka inatiwa kwenye meli na napata docs copy kupitia email na pindi gari akikabidhiwa shipper natumiwa docs zangu originals through DHL au TNT na nazipata ndani yasiku tatu hadi nne.kwa hiyo gari kabla haijafika docs zangu originals nakua nazo na kuanza utaratibu wa kodi na hatimaye likifika ni kulitoa bandarini tu.
    Kwa hiyo mdau nakushauri gari za kuagiza japan mojakwamoja ni nzuri sana ila angalia mitandao unayotua sisemi autorec ndio uagize wapo wengin wengi ila mie experience yangu ni autorec
    Mbegu.

    ReplyDelete
  26. Noba International ni kampuni ya Mtanzania aliyeoa Mjapan. Imekuwepo muda mrefu ikifanya biashara hiyo . Mimi binafsi nimeshaagiza gari tatu kwa wakatati tofauti na pamoja na marafiki zangu. Namba ya huyo Noba ni +819017337447

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...