Na Ripota wa Mahakamani
MTUMISHI wa Bodi ya Mikopo ameburuzwa kortini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidaiwa kuiba Sh Milioni 90.

Ester Budili anaedaiwa kuwa ni mhasibu ingawa kwenye hati ya mashitaka haikuelezwa nafasi yake ya kazi, amepandishwa kizimbani leo  na kusomewa mashitaka kumi yakiwamo ya kughushi na mmoja la wizi wa fedha hizo.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka alikana yote na kuachiwa kwa dhamana ambayo mashalti yake ilikuwa ni wadhamini wawili wa kuaminika ajira zao, mmoja kutoa Sh milioni 45 ambapo mshitakiwa mwenyewe alitakiwa kusarenda pasi yake ya kusafiria.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Budili anadaiwa  kuingiza majina ya wanafunzi ambao hayatambuliki 91 kwenye orodha ya malipo ya mikopo ya wanafunzi katika vyuo tisa.

Mashitaka hayo yalisomwa na mwendesha mashitaka Frida Mwela mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Binge Mwashabala.

Budili alidai katika siku isiyofahamika kati ya Augosti 5 na April 24 mwaka jana katika ofisi za Bodi ya mikopo iliyoko wilayani zilizoko Msasani wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akiwa mtumishi wa umma aliiba fedha mali ya mwajiri wake Sh 90,775,800. 

Shitaka la kwanza alidaiwa kughushi katika tarehe hizo hizo orodha ya majina na kuongeza majina Chuo Kikuu cha Bugando, John Suzan, Peter Bahati, Mombo Yusuph, Bitaliho Gordian, Kwangaya Ibrahim, Alfred Happy, Isack Simon na Nyangige Juliana huku akijua si kweli.

Chuo cha Uhandisi na Tecnolojia, Catherine Nkya, John Nkyaa, Andrew John, Goliama Ally, Simon Pamela, Gaash damian na Suzane John.

Chuo cha maendeleo ya Jamii, Suzane John Meela Christopha, Zake Ezra, Goliama Ally, Simon  Michael, Peter Massawe, Naruo Peter, Pamela Simon na Catherine Nkyaa.

Chuo Kikuu cha Ualimu cha Dar es Salaam, 
Pamela Simon, Minisi Grace na Hamza Goliama. 

Chuo cha Ustawi wa Jamii, 
Pamela simon, John Suzan, Alfred Happines, Wambura Juliana, John Andrew, Andrew nkyaa, Hamza Golima na Suzane John.

Chuo cha Tiba cha KCMC, 
Peter Naruo, Simon Nkyaa na Pamela Simon. 

Mzumbe,  
Pamela Nkyaa, John Nkyaa, Simon Andrew, Pamela Michael, Ester Goashi, Ester Damian, Daudi Ester, Adiambula Ester, Peter Bahati, Naruo Peter na Suzane John.

Tumaini, chuo cha Ruaha, 
Hamza Goliama, Ester Lissu, Kalinga Ester, Alfred Happy, Andrew John, Pamely Michael, John Nkywimba, Pamela Simon, Suzane Nkya, John Nkuba, Catherine John, Simon Nkya, Adia Elisha, Suzane John, Naruo Peter, Ester Lucus na Adihambo Delinja.
Huaha, Suzane, Paul Naruo, Michael Pamela, Bahati Peter, Dismas Ester, Lilian Victory, John Sukamule, Diambo Mbudala, Pamela John, Suzane John, Anordl Bulili, John Suzane Simon Pamela Catherine Nkyaa, Damas Ester na Simon Ngonyani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Professor Mukandala upo hapo??....Sitaongea mengi kwa sabau kesi ndiyo kwanza imeingia Mahakamani.

    David V

    ReplyDelete
  2. Ila watu tumekosa ubinadamu. Hawa ndio wanaostahili kupigwa mawe mpaka kufa na sio kibaka anaeanua shuka ili auze anunue muhogo. Sasa hii milioni 90 ndio alipokamatiwa, huko nyuma wakati anaiba vikumikumi hadi 30 ili kupatia uzoefu wa wizi hatujui ameshaiba vingapi. Ikithibitishwa afilisiwe kwasababu hawa ndio wanasababisha wadogo zetu wanaandamana kila siku na kufukuzwa vyuo vikuu. Sijui mtu kama huyu analalaje usingizi.

    ReplyDelete
  3. du kweli wabongo ni wabunifu hasa kwenye fitina na wizi. Ukisoma kwa makini hayo majina ya wanafunzi mengi yanajirudia katika vyuo tofauti.

    ReplyDelete
  4. Bodi ya mikopo kuna ufisadi wa kutisha pamoja na vyuoni, udom,udsm, muce,duce n.k

    ReplyDelete
  5. Kwa akili za mtu timamu ni wazi kabisa anaweza kutambuwa kwamba hapa kuna kundi la watu walioshirikiana kutekeleza huu ufisadi. Na pia ni vyema ikafahamika kwamba hili swala la wizi ambalo linajitokeza sasa kwa umma ni baadhi ya ufisadi ambao unaendelea ndani ya bodi ya mikopo.Yapo mengi ambayo yamejificha. Hapa nampa Hongera Mh.Zitto Kabwe na kamati yake ya uhakiki wa hesabu za mashirika ya serikali kwa kuibua huu uozo.

    ReplyDelete
  6. Jaman hii bodi ichunguzwe kwakweli,nahisi huyo ni chambo 2,cse kama kuna graduate amemaliza 2009 but nw ananyumba 3 hapa dar na magar kadhaa na wanategemea kaz 2,hapo kuna wa2 wanamajina hewa,na kuna wale ambao kama hajapata mkopo au ana% ndogo anaambiwa kama anakiac chochote atoe na anapata mkopo with full 100% na wala hata hastahili ndo maana sometimes kuna malalamiko.jamn pachunguzwe hapo

    ReplyDelete
  7. You do not need auditing certificate to discover forgery (how many suzan john,john suzan)she deserved long prison sentence!

    ReplyDelete
  8. Safi sana serikali kwa kuanza kuwabana hawa wezi,maana wanatutesa wanafunzi bila sababu za msingi kumbe wanalipa wanafunzi hewa! Pia naishauri serikali kupitia majini upya ya wanafunzi ambao wako URUSI na UKRAINE wenye sifa ya kupata mkopo kwan kuna wanafunzi wasio na sifa za kupata mkopo wa serikali lakin wanapewe kisa ni watoto wa WAKUBWA! Hii sio haki kwan wanapewa pesa nyingi wakati huko tanzania kuna watoto wa wakulima wanakosa mkopo!

    ReplyDelete
  9. UKIYAANGALIA MAJINA TU,UNAPATA PICHA YA KUGUSHI MAANA MAJINA MENGI YAMEJIREJEA AMA KUGEUZWA TU KATIKA VYUO TOFAUTI, KWA MFANO SIMON PAMELA

    YAONEKANA WAZI MTUHUMIWA ALIISHIWA NA MAJINA YA KUGUSHI.

    ReplyDelete
  10. Wizi jamani hauna macho inakuwaje jina moja litokee vyuo zaidi ya vitatu, wakati huohuo kuna waliofukuzwa chuo wakidai pesa. Mamlaka husika lazima iangalie hili jambo kwa makini

    ReplyDelete
  11. huyo tangu ameachiwa kwa dhamana hamna kitu. Dhulma mbaya sana. ukikutana na watu hawa amini mungu wanakuwa kama wanyama...wanakuwa hawana utu. Na yote kujichumia mali za wizi na kuwadhulumu wanafunzi wengine. Hadi lini tabia kama hizi zitakwisha au mnasubiri watu waanze kuuwana na kutekana. Chakusikitisha akiachiwa huru anaendelea kufanya kazi bila ya restriction yeyote.

    ReplyDelete
  12. Vyuo vyote viangaliwe sio mikopo tu!!

    ReplyDelete
  13. Najaribu tu kuwaza kwa sauti. Hivi kungekuwa na utaratibu maalumu wa kumonitor progress za hawa wanaopata mikopo mfano kuwe na progress report kila mwisho wa semester kwa kila aliyepokea mkopo, huyu Esther angekuwa anaandika reports zote hizo za wanafunzi hewa au? dah inaelekea loopholes za kula ni nyingi sana aisee

    DWS

    ReplyDelete
  14. WIZI HUO HAUJAANZA LEO,NI VEMA WAFANYE UCHUNGUZI TOKEA NYUMA.NA PIA KILA CHUO CHA SERIKALI KINA MHASIBU WA BODI NA HAO WACHUNGUZWE KWA MAKINI,WAMENUNUA MAGARI SANA NA WAMEJENGA NDANI YA MDA MFUPI WAKATI VIPATO VYAO NI VIDOGO.

    UNYAMA KAMA HUO UPO KOTE HALMASHAURI,WIZARANI NA SECTA ZINGINE ZA SERIKALI.

    UBINADAMU UMEISHA NA HAKUNA WA KUJARI,WATU WANFIKIRI WATAISHI MILELE HAPA DUNIANI NA HUYO MALI ZAKE ZOTE ZIKAMATWE NA KILA ALIYE KARIBU YAKE OFISINI PIA ACHUNGUZWE.
    JAMANI TUSHIRIKIANE KUTOA HADHARANI VIPATO,MALI WALIZONAZO NA NDUGU ZAO NA MIRADI WALIYONAYO WATU KAMA HAO ILI TUJUE UKWELI HATA TUKIANDAMANA MUNGU ATATUSIKIA TU.

    ReplyDelete
  15. Watu wa dini fulani bwana, wao ni kufoji foji taaluma na wizi wizi tuu.

    ReplyDelete
  16. Nadhani huu mchezo ni wa uzoefu ktk hiyo board. Wakifukua zaidi watakuta mambo makubwa. Watoto wetu wanakosa mikopo wakati sifa wanazo ukiuliza unakuta sababu za ajabu eti kasoma shule ya private A-level wakati watoto wa wakubwa wamesoma hizo shule na mikopo wamepata. Tutafika jamani?

    ReplyDelete
  17. Angalieni sasa,,,Masikini wee Wanafunzi wa Elimu ya Juu wanaandamana huku wakipigwa Virungu na Polisi wakidai Mikopo kwa ajili ya Masomo halafu Genge la Wezi wanaiba mihela yote hii wanajengea majumba na kununulia magari!

    Huyu Mwizi wa Milioni 90/= cha kwanza ataje alioshirikiana nao katika Wizi huo wa mwaka, na cha pili kundi lao WARUDISHE FEDHA ZOTE NA PIA BAADA YA HAPO WAFUNGWE GEREZANI!

    ReplyDelete
  18. Hii inatisha na kuumiza maana watoto wanakosa mikopo wanaishi maisha ya taabu kumbe kuna mambo kama haya yanaendelea . Achukulie hatua kali kabisa

    ReplyDelete
  19. Mimi nawafahamu sana hawa jamaa wa bodi ya mikopo. Ni wezi wa ajabu hata huyo aliyekamatwa ni dagaa tu. Ukiangalia matumizi na matanuzi yao utashangaa kama kweli ni watumishi wa umma ambao kama tujuavyo mishahara ya serikali. Wizi wao unalenga zaidi kwenye
    1. Majina hewa.
    2. Ulipaji wa asilimia. Hapa utakuta mwanafunzi kapata mfano 40%. Lakini kwenye fungu anaonekana amepata 80% au 100%.
    3. Wanafunzi wanaofeli au kufukuzwa au kuacha masomo kwa sababu yeyote. Pesa hapo inaendelea kuliwa.
    Jamaa yangu aliniambia kuwa anaweza kutengeneza 10mil kwa dk chache

    ReplyDelete
  20. Haya majamaa ni majizi makubwa sana,chunguzeni wanavyoiba hela kwa kughushi gharama halisi za usafiri kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma abroad!Jamani ni shirika gani la ndege linalotoza dola 1900(One way ticket) kwa kusafiri kwenda China/urusi?Ninaushahidi na hili nawavutia kasi tu wezi wakubwa hawa!

    ReplyDelete
  21. ninachoweza kusema ni kwamba hayuko peke yake mpaka wanaotoa pesa hizo vyuoni wamo, anapataje pesa yake kama hawashirikiani na wahusika wenginge.harafu wanadai fedha zimeisha kumbe wamwlipwa wanafunzi hewa.

    lakini yote haya hay yanatokana na usimamizi hafifu/utendaji mbovu wa serikari.

    ReplyDelete
  22. SEKTA NYINGI ZA SERILALI NDIO ZIPO HIVYO, KAMA HUYO TU KAPATIKANA NA KOSA HILO VIPI KUHUSU WATENDAJI WENGINE WA BODI? INA MAANA ANAFANYA KAZI PEKE YAKE? HUKO VYUONI WALICHUKUA HATUA GANI?

    ReplyDelete
  23. Mwenzio akinyolewa ww tia maji, tusifanye mchezo kama huu tutakamatwa tu sasa hivi mambo yamekuwa magumu, hizi kmati zinafanya kweli, tutaacha familia zetu zinaangamia tutafia jela kisa maisha ya harakaharaka!

    ReplyDelete
  24. Huyu Mhalifu ESTER BUDILI....

    KESI ZA UFISADI ZINA DHAMANA?

    HAKUSTAHILI DHAMANA KABISA NI MUHIMU ARUDHISHWE NDANI MARA MOJA!

    ReplyDelete
  25. Huyu Mhalifu ESTER BUDILI....

    KESI ZA UFISADI ZINA DHAMANA?

    HAKUSTAHILI DHAMANA KABISA NI MUHIMU ARUDHISHWE NDANI MARA MOJA!

    ReplyDelete
  26. Genge hili ni Adui Mkubwa wa Maendeleo ya Nchi yetu!

    Elimu na Sayansi ndio mhimili wa maendeleo wa jamii yeyote ile na jamii inayopuuza Elimu matokeo yake ni laana ya kukwama kimaendeleo!

    HAWA WATU WANATAKIWA ,WASAKWE MTANDAO WOTE UPATIKANE, HALAFU WARUDISHE FEDHA HIZO NA KAMA WAKIPATIKANA NA MALI WAFILISIWE MALI NI ZA WIZI!...HALAFU MWISHO WAFUNGWE SANA!

    ReplyDelete
  27. Mwanangu kanyimwa mkopo kisa alisoma shule ya private ambayo nilisaidiwa kulipiwa na marehemu mjomba wangu kwa sasa anasoma kwa taabu mlo mmoja kwa siku tumeomba mkopo tumenyimwa pamoja na kueleza hali ngumu ya mzazi mmoja na maradhi yanayonikabili ambayo yamepunguza ufanisi wangu wa kazi bado watu wana fodge mapesa kibao huyu mama asingepewa hata dhamana na anastahili kupigwa mawe adi afe kama vile watoto wetu chuoni wanavyopigwa na mapolisi.

    ReplyDelete
  28. msianze taja wengine huyu alokamatwa hata mahama ikimuachia hizo hela atazitapika tena tunatoa onyo muda wa kudai mikopo ukifika msituambie hela zimekwisha maana tunakuja choma moto mtu.

    ReplyDelete
  29. Pole dada Esta, wewe kwa kujisalimisha wataje wenzako wote mliokula nao, hilo njanga si lako peke yako. pole sana

    ReplyDelete
  30. Huyu kuiba fedha nyingi kiasi hicho hakuwa peke yake. Hayo majina waligawana hapo bodi ya mikopo. Kama fedha zilikuwa zinapitia benki wakaangalie picha za wenye akaunti utakuta ni wafanyakazi wa hapo hapo bodi ya mikopo. Huyu katolewa tu kama mbuzi wa kafara kama ilivyokuwa kwa Liyumba. Hawa ndiyo wanasababisha wanafunzi kugoma wakati wao wanselebuka na fedha za mikopo. Serikali iamke naona imelala usingizi kila mtu anafanya anavyotaka. Malipo ya wanafunzi hewa yanatoka haraka kuliko wanostahili. Hatuwezi kufika. Sheria za makosa kama haya zibadilishwe iwe ni uhujumu uchumi na mtu akipatikana na hatia afilisiwe mpaka hata kijiko ili aanze upya baada ya kutoka jela.

    ReplyDelete
  31. Ester Budili na Genge lake:

    Watu wa namna hii wanauwa kabisa ile ARI YA UTAIFA KWA VIJANA WANAOSOMA.

    Hebu fikiri mtu anamaliza Chuo kwa kusoma kwa taabu akidai nyongeza ya Mkopo kwa ajili ya Masomo anachapwa virungu na Polisi, huku akina Ester Budili na wenzake ktk Bodi wanachota Mamilioni wanatumia,,,mbaya zaidi inatokea kesi inakwisha na hakuna hatua zozote zinachukuliwa dhidi yao au unakuta wanafungwa MIAKA MIWILI TU!

    ReplyDelete
  32. Huyo simon pamela ni nani yake mbona amemtumia sana tena amtafute amwombe msamaha kwa kumchafulia jina.

    ReplyDelete
  33. Kuna mfanyakazi wa pale BODI anaitwa Rose Marwa huwa anampelekeaga dili.

    ReplyDelete
  34. ushenzi kama huu umeenea nchi nzima.
    Mtu mmoja anaiba fedha za serikali wizarani na kutamba bila ya woga kuwa hajawahi kutumia mshahara wake miaka mi-3, kama si wizi anapata wapi pesa za kujikimu? Miaka mitano tu ana nyumba 10, viwanja 10na magari matano!
    Ikifika zamu ya kuingia mtaani sisi wala mlo mmoja wa bamia na dagaa wachungu tutapora kila tajiri kwani wote wezi wa mali ya umma!

    ReplyDelete
  35. serikali ikitaka mtu wa kupiga mawe waarifu mpaka wafe kazi hiyo naomba nipewe mimi mganga njaa wa Dar, HASIRA yangu kuwatoa roho wezi wa mali za umma inaumiza sana wengine tunataabika na wapo wanaokula kuku kwa mrija wa wizi. Shwain wakubwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...