Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gahrib Bilal akiongoza sala maalum ya kuombea marehemu mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina, kabla ya mwili huo kusafirishwa leo kwenda Korogwe kwa mazishi. Shughuli hiyo ilifanyika nyumbani kwa marehemu, Wazo, jijini Dar es Salaam leo.


BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mwandishi wa habari naona ameteleza kidogo kwa sababu anayeongoza sala ni yule aliyeshik microfon ambaye si Ghalib Bilal. Ghalib Bilal anaonekana amepanga safu na waumini wengine.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli anaeongoza sala ya maiti hapa ni imamu ambaye amesimama mbele. Muheshimiwa Bilali anashiriki tu katika sala hii na wala haongozi.

    ReplyDelete
  3. MIMI NAONA MWANDISHI HAJAKOSEA HATA KIDOGO SABABU MUHESHIMIWA BILALI ANAONGOZA KAMA INAVYOONEKANA YUPO MSTARI WA KWANZA AMA KWA LUGHA NYINGINE MSTARI WA MBELE NA NYUMA YAKE KUNA MISTARI MINGINE

    ReplyDelete
  4. nop amekosea,ukizungumzia jambo la sala anayeongoza anaitwa imamu na simwengine.

    ReplyDelete
  5. hapa angelisema hivi:dr mohammed gharib bilal ambaye ni kiongozi wa ngazi za juu katika serikali naye alishiriki katika kumsalia marehemu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...