Mfalme wa mipasho, Mzee wa kulambisha akipagawisha Mont Vernon, New York kwenye Show kabambe Jumamosi Janauary 21, 2012 iliyokonga nyoyo za mashabiki kwa kuimba nyimbo zake kwa ustadi mkubwa huku akiwa mcheshi muda wote.
Juu na chini ni Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York.
Kulia ni Balozi wa Somalia Umoja wa Mataifa Mh.  Dr.Elmi Ahmed Dualeh akiwa na mke wake wakipiga picha ya pamoja na Mzee Yusuf (kati), Mh. Dr. Elmi Ahmed Dualeh alishawahi ishi Zanzibar miaka ya nyuma wakati Mzee Yusuf alipokua mdogo.
Mzee wa alamba, Haaam, Haaam akifanya makamuzi New York.
Mashabiki waliokuja kulambishwa wakichenguka na huku wakimtunza Mzee Yusuf aliyekonga nyoyo zao kwa show iliyofana iliyofanyikia Mont Vernon, New York, Nchini Marekani.
Juu na chini mashabiki wa New York na Vitongoji vya jirani wakiendelea kulambishwa na Mzee Yusuf.
 
Ilikua balaa hakuna kukaa chini Mzee wa Alamba, Mfalme wa mipasho alivyofunika New York.
Mashabiki wakiimba pamoja na Mzee Yusuf
Ilikua si mchezo uliyekosa karibu DC Feb 4 atalambisha mashabiki wa DMV.
Mashabiki wa New York na Vitongoji vyake wakipagawika na Mzee Yusuf, Mfalme wa mipasho.
Mashabiki wakilambishwa na Mzee Yusuf alipofanya show Mjini New York Jumamosi January 21, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi! Hapa pamekaaje,je huko kwa Obama hakuna wanaume wa kibongo maana naona akina Dada tu ndo wanaselebuka! Au ni vijana hawaendi na mitindo ya huyo Mzee Yusuf.

    ReplyDelete
  2. sasa huyo dada myenye mkanda mwekundu alichukia nini mwenzie kucheza na Mzee Yusuf

    ReplyDelete
  3. Na mimi nimemshangaa huyu dada kama anadharau au hakupendezewa mwenzie ashikwe kiuno,,,taarab sana sana huwa ni starehe ya kina mama,,ni siku hizi tu naona mpaka wanaume wanaingia katika starehe hiyo,,,au walikuwepo wakaamuwa kukaa tu bila kucheza...hata hivyo huyo aliyekuwa akiandika hapo katika matangazo inaonyesha bado anafanya promo watu sio wengi kiivyooo!Maana picha za watu wa kujaa huwa ni mshike mshike,kama Diamond akija hapa UK,,,kweli picha unaona watu nyomii!

    ReplyDelete
  4. Toka lini Mipasho ikachezwa na wanaume ? Wanawake tunapashana zaidi.

    ReplyDelete
  5. jmn nilikuwa nachk totoz zikishikwa mauno,watu walikuwa nyomi sema tu walikuwa nyuma.

    ReplyDelete
  6. wewe unaitaka wanaume wawepo hapo, hivyo mwenzetu ni wa wapi? unajua kinachoimbwa hapo? kwa hali inavyokuwa hapo ikatokea kuwepo mwanamme ambae hayupo hapo kwa kikazi basi kila mtu atauliza sexuality yake.

    ReplyDelete
  7. hivyo nyinyi mnaosema huyu dada anaangalia kwa dharau hamkuwahi kuona watu wakifanya mtizamo huo? mtizamo huo watu hufanya na kusema mmm.

    ReplyDelete
  8. Huo si mtizamo wa dharau. Anakagua mienendo ya Mzee Yusuf hasa anavyopapasa hiyo kiuno ya mrembo.daa Hii shughuli ilitulia nadhani hii ilikuwa magomeni in new york.

    ReplyDelete
  9. jamani huyu dada mwenye mkanda mwekundu,yeye ni kubeba box tuu,leo ndiyo kaenda kuosha uso,ndiyo maana anaangalia watu kama anataka kulia.

    ReplyDelete
  10. no kwa wale ambao hawamuelewi huyo dada na muangaliao wake naomba kuwafahamisha..siyo dharau, wala hasira..hiyo inaitwa "NEW YORK ATTITUDE"..you can only see it in nyu yoku only.

    ReplyDelete
  11. hawa dayaspora wanameremeta sana.ndo maana hawakumbuki kurudi huku nyumbani.

    ReplyDelete
  12. Niambieni jamani, anawalambisha nini?

    ReplyDelete
  13. I like the girl with a blue dress in the last picture she is gorgeous!

    ReplyDelete
  14. Hiyo ''NEW YORK ATTITUDE'' lohhh mbona ipo kama wivu vileee!

    Kama ni hivyo basi watu wakiwa Marekani hapafai kutembelea!

    ReplyDelete
  15. ME I DONT LIKE ANY!!!! Teh teh,,

    ReplyDelete
  16. du mzee yusuphu si mchezo aliwalambisa mbaya kabisa,ila yote kwa yote mambo ilitulia sasn

    ReplyDelete
  17. jamani huyo dada wa blue, mashallah! naomba namba yake kwa wale wanaoifahamu...nitakuwa Manahattan February yote!

    ReplyDelete
  18. piga 911 au 311 muulizie utampata huyo binti wa blue dress

    ReplyDelete
  19. yusufu ukumbuke kurudi home kaka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...