Kwa heshima kubwa naomba nitumie blo Globu yetu ya Jamii kuwafahamisha Watanzania wenzetuna wengineo kuwa kuna nafasi za  ajira nchini Australia kwa  wale  wenyesifana consultancy experience katikamaeneoyafuatayo:

1.Civil Designing Engineering
2. Structural Engineering
3. Mechanical Engineering
4. Geotechnical Engineering
5. Geologists

Kwa Mining na Design Engineering  mshaharanikati ya $60K- 160Kkwamwaka ,wataweza kupata  nyongezahadikufikia $250K  kilawanapoendela  kupata  uzoefuwa Australian projects .Kwaupandewa  Building services industry mshaharanikati ya $50K -$100K .

Kwamaelezozaidiandika  email kwenda  :
ili pia uweze kutumiwa fomu za  awali za maombi ya  ajira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Uncle mto tangazo bado maelezo hayajitoshelezi.Hizo nafasi za kazi ni za serikali au kampuni binafsi?Hii email uloweka hapa ni ya nani muajiri au agent wa hizo ajira?Weka wazi vigezo vinavyotakiwa awenavyo muombaji na gharama za maombi.
    Nataka uweke wazi bcoz km ni Skilled Migration ya Australia binafsi naifahamu na kwa maelezo uliyoweka hapa hayasaidii sana kwani kuna procedure kibao.Naomba usinielewe vibaya sio kwamba nakupinga ila nataka ufafanue zaidi ili wadau waelewe na kupata picha nzuri zaidi kabla hawajachukua hatua muafaka.
    Thanks.

    ReplyDelete
  2. Hmmm, ...@yahoo.com, hili litakuwa chezo

    ReplyDelete
  3. Ili kuondoa utata,weka link genuine ya hizo kampuni/taasisi zinazotangaza nafasi za kazi.

    ReplyDelete
  4. Wewe tangu lini kazi ya uhakika ikatolewa na mtu mwenye yahoo?? haya katoeni details zenu mtume na vyeti muone mnavyolizwa na Wa-Nigeria-like matapeli....!!

    ReplyDelete
  5. Tokea lini Geologist akawa Mhandisi?

    ReplyDelete
  6. Mimi ninayo degree ya Civil Engineering lakini sijawahi kufanya kazi hata siku moja ya Civil Engineering. Lakini course zote nimesoma na nazijua vizuri tu, je wanaweza kunipa ajira?

    ReplyDelete
  7. jamani taasisi hii mbona inajulikana sana ni moja ya taasisi chache zilizotutoa nje wa Tanzania.

    mimi nafanya Masters University of Wales.nimekuja UK kwa msaada wa hii taasisi imesajiliwa na ofisi zao ziko hapo Haidary plaza ghorofa ya kwanza.

    kuna msemo maarufu wa Mao kuwa NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK.kwanini msiwasiliane nao kwanza na kujua ukweli kuliko kukurupuka na kuja kutoa maoni msiyo na uhakika nayo.

    Mimi kabla ya kuwatumia hawa Abroad Studies nilikwenda Brela na kuona uhalali wa kazi zao.
    huyu aliyeshangazwa na yahoo nae ni mvivu wa kufanya tafiti hapa UK bado kuna taasisi zinatumia email za yahoo.itakuwa na Tanzania?

    ina maana huwezi kuamini kuwa Michuzi Blog ni moja ya Blog kubwa duniani sioAfrica kwa mujibu wa Google sababu tu Michuzi anatumia gmail.com?

    anayetaka kujua zaidi aulize kwa wanafunzi wanaosoma London School of Commerce iwe pale London Bridge Campus au Elephant and Castle.chuo hiki ndicho chenye watanzania wengi kwa sasa na 70% wameingia hapa Uk kupitia taasisi hii yenye email ya yahoo.

    Kujifanya wajuaji wa mambo bila kufanya tafiti ndio kumewafanya wenzetu toka Zanzibar kuwa wengi nje ya Tanzania sababu wenzetu ni risk taker na watu wenye kuthubutu.sisi waTanzania wa Bara kila jambo tunataka kuweka siasa mbele.

    Ushauri kwa watanzania wenye nia ya kutafuta kazi muwasiliane na hawa jamaa then mtakuwa kwenye nafasi ya kujua ukweli kuliko kusikiliza maoni ya hawa wasiowatakia mema watanzania.jaribuni kuwasiliana na London school of Commerce mjaribu kupata credibility ya Taasisi husika.au tafuteni wanafunzi wanaosoma Uk wawaelezejuu ya Abroadstudies.

    Vinginenvyo fursa kama hizi zingekuwa kwa Wakenya au nigeria tungeanza kulalamika.hata zinapotokea scholarships au kuomba kazi Jumuiya za East African wenzetu huchangamka kwa haraka wakati sisi tunajitia ujuaji usio na maana.
    Mdau James Charles.
    lewisham-UK.

    ReplyDelete
  8. Hiyo email address in mashaka kidong, anyway goodluck to all who want to come to Australia, it is the best country in the world.

    ReplyDelete
  9. kwa maoni yangu sidhani kama kuna ukweli kwenye hili swala watu wawe makini wasije wakaibiwa.

    ReplyDelete
  10. Wezi hawa jamani msitume chochote!

    Mtaliwa hela bure!

    ReplyDelete
  11. Usije ukajuta ndugu,kaka Michu yaweza kwa kujua au kutokujua unatumika katika mtandao unaotiliwa mashaka.

    ReplyDelete
  12. nyie mnaojitia wajuaji ati yahoo sijui upuuzi gani mnajidai mwajua saana mambo, acheni wenye kutaka kujaribu wajaribu bahati zao na kama huna vigezo husika vilivyotajwa kojoeni mkalale, maana kitu cha manufaa kikiwekwaga humu, basi itaibuka miwatu flani inajidai inajua sana mara changa la macho ali mradi wameleta pumba zao humu! kwani yahoo ina shida gani mbona kabla watu walikuwa wanaitumia bila shida acheni upuuzi wenu! na kuna makampuni nyeti kibao hapo bongo yanatumia yahoo!

    ReplyDelete
  13. Mbona jazba mdau wa "Fri Jan 20, 10:38:00 AM 2012" Watu wanauzoefu wa madudu kama haya,pengine wewe ndie mwenyewe unaona dili lataka kuponyoka. Kumbuka tuna wajibu wa kuwatadhalisha wenzetu juu matapeli kama ninyi ambao mnatumia udhaifu wa walio wengi kutakakupata utajiri bila jasho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...