Unapobahatika kufanya utalii wa ndani katika hifadhi zetu za Taifa, kamera yako isilenge kwenye wanyama wakubwa tu. Hata ndege na wadudu wako wengi wa kuvutia. Hapa ni katika hifadhi ya  Serengeti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Utalii wa ndani mlalahoi hauwezi. Utalii wa ndani kwa wenye kazi za mishahara kuanzia £800,000/= kwenda mbele ndio wanaoweza ambao idadi yao ni watu laki 3 tu Tanzania nzima.

    ReplyDelete
  2. haha nchi watu milion46 sio@ anonymous hapo juuu

    ReplyDelete
  3. utalii kwa watanzania wenyewe ilitakiwa uwe ni bure

    mpaka leo hii wanafunzi wa mashule mbalimbali hawafiki kujionea wanyama au mlima kilimanjaro kutokana na hakuna mipango iliyoandaliwa kuwafikisha kujionea vitu vyao watabakia kuimba mashuleni mlima kilimanjaro ni mlima mrefu una vilele viwili kibo na na nini sijui

    wakati wenyewe watabakia kuona kwenye picha tu

    huku ughaibuni kuna mipango maalumu ambayo kila baada ya kukaribia kufungwa mashule wanafunzi huandaliwa safari za pamoja kwenda kujionea vitu mbali mbali vilivyopo ndani ya nchi yao

    kwa ghalama za serikali kwani ni moja ya elimu kuwapatia wanafunzi elimu ya kufahamu mambo mbali mbali

    ReplyDelete
  4. Mmejaribu kuuliza kuhusu gharama za safari za kutalii ili kuthibitisha msemayo?

    naomba annony 1 & 2 mfanye hivyo ndio mje mseme hayo msemayo maana sidhani kama ni ya ukweli. Ni swala tu la mipango na muda. TANAPA wanakuwa na safari za kwenda Mikumu toka Dar na kule Arusha pia kwa gharama ya TSH 10,000/=. lakini sidhani kama wengi tunaiona hii kama ni fursa ya utalii kwetu. Utalii una madaraja yake na kila daraja lake lina kiwango chake cha gharama - kama ulivyo usafiri wa anga au reli.

    Tuthubutu na tuache kuosha vinywa kwa mchanga kwenye mambo ambayo tunayamudu tikuamua kuchagua

    Mkereketwa

    ReplyDelete
  5. watoto wetu wanahitaji shule,walimu,madawati,vitabu, madawa,yunifon, na chakula cha uhakika utali hauna nafasi kwa watanzania walowegi hawana uhakika na maisha yao na watoto wao wapo wanaohitaji utalii ni watoto wa vigogo mafisadi si mtoto wa mkulima

    ReplyDelete
  6. Fanyeni mpango basi hata kunguru wa dar na inzi wawe vivutio vya utalii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...