Picture
Na Francis Godwin, Iringa
Wakazi wa Tanangozi na Ihemi katika wilaya ya Iringa vijijini katika harakati za kukinga mafuta kutoka kwenye lori la kusafirisha mafuta lenye namba T 575 AXH lililoanguka na kumwaga mafuta katika barabara kuu ya Iringa-Mbeya eneo la Ihemi,  huku polisi wakishuhudia bila kuchukua hatua zozote endapo mlipuko utatokea.
Ni jambo la kushangaza sana kuwa baada ya visa vya watu kulipukiwa na moto wa mafuta ya dizeli au petroli si tu nchini mwetu bali hata nchi jirani kama vile Kenya, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nigeria nk, licha ya habari na taarifa hizo za kutisha ambazo zimeua maelfu ya watu, watu bado wanasogelea hatari hiyo.

Ni kama vile tahadhari zinazotolewa za kutokukaribia hatari hiyo zinapuuzwa, au watu wana kiburi kwa kujiamini wao ni spesheli na wajuzi zaidi kamwe hawawezi kukumbwa na hatari au ni ujinga ama kutokujali na kusingizia maisha magumu.

Kama hiyo haitoshi,  wanaonekana baadhi ya askari nao ambao jukumu lao la msingi ni kulinda usalama wa raia katika hali yoyote, anaonekana kukubaliana na kinachotendeka mbele ya macho yake. Nilitarajia wawe mstari wa mbele kuweka utepe wa njano kuzunguka eneo lenye lori hilo na kuhakikisha yeyote anavuka utepe huo anatiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani kwa kuhataria maisha yake, ya jamii na kukiuka maelekezo halali ya askari.

Kweli, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa!" - Hosea 4:6
Picture
Askari ni kama vile nao ni... kwa jinsi alivyosimama na kuonekana kuacha anachokishuhudia kiendelee kana kwamba hakumbuki kazi yake ni kulinda usalama wa raia nyakati zote.
Picture
Na watoto wamo katika hatari hiyo pasina kutaka. Picha na  Francis Godwin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Usiwalaumu sana hawa ni ugumu wa maisha umewafikisha kwenye hatua hii ya kujihusisha kwenye matukio hatarishi!! Maosha yamekuwa magumu sana kiasi cha watu kuamua liwalo na liwe!!

    ReplyDelete
  2. Mungu wangu mnakumbuka yale ya watu wa ile sehemu waligeuka ndafu wa sherehe.

    ReplyDelete
  3. yani sisi watanzani ni mawazo mgando kweli kweli yani hata kufikiri hatufikirii dah! hii siilishawai kutokea na wa2 wakafa vibaya mno jamani.

    ReplyDelete
  4. Mungu weee, wa picha ya pili wanaonekana wamepanga foleni kabisa na watoto mgongoni.Inaonekana polisi yupo kukusanya "ushuru" kwa wanaotaka kushota hayo mafuta.

    Lakini picha inaonyesha direction ya ilo lori ni Dar es salaam so lipo tupu.

    ReplyDelete
  5. Maneno ya Mungu kuwa Nukuu..."Tazama Watu wangu wana angamia kwa ujinga wao".Mwisho wa nukuu.

    Watu wamekuwa wana angamia ki rahisi rahisi tu kwa kukosa maarifa na busara.

    Kila la heri na Tanzania yetu yenye ujinga tele.

    ReplyDelete
  6. serikali ya tanzania inaongoza wapumbavu wengi na viongozi wako happy kwa hilo kwa kuwa hata mkiibiwa na kudanganywa mtakubali...mimi naamini kabisa asilimia ya watu wenye elimu ni ndogo sana na ndio maana watu kama kina babu wa loliondo wakiibuka wajingani wengi wa kuwafuata.

    ReplyDelete
  7. jamani mbona binadam saa nyingine tunakua na akili za kuku. yaani watu wenye akili timamu wataweza kujaribu kuchota hayo mafuta wakati wanajua moto unaweza anza hapo na watu wote waliopo hapo wakafa. huyo polisi aliyekuwa hapo anatakiwa ashtakiwe kwa uzembe wake. haya mambo yamekua yakitokea africa mara nyingi na unafikiri watu watajifunza lakini wapi. i hope vyombo vya habari na serikali wata waelimisha wananchi kuhusu hatari za mafuta.

    ReplyDelete
  8. Hakuna tafauti katika ya UK na TZ. Hau wadau wanaonyesha ni watu wenye afya kamili isipokuwa yapo mafuta ya bure kwahivyo wanachangamka kama vile walivyofanya London wakati wa ghasia za Totenham kuvamia maduka ya simu na TV!!

    ReplyDelete
  9. Huyu baba aliyekuwa anaendesha hili lori ni nini kilimtokea ni mambo kulala usingizi nini?

    ReplyDelete
  10. Mdau, technically sioni sababu ya wewe kukandia sana police sababu kama lori limeanguka tayari na kila kitu kipo intact kama inavyoonekana kwa picha mtu unaweza kinga hayo mafuta si sawa na kwenda petrol station hamna tofauti. ila tu watu asiwashe moto, sigara au kujaribu kutoa battery la lorry. au we unaonaje?

    ReplyDelete
  11. embu yaone yalivokaaa na wengine wamebeba na watoto kabisa shuwaini hawawazi hatari ambayo inaweza ikawapata hapo!

    ReplyDelete
  12. Jamani njaa mbaya!

    MIFANO YA UNUFAIKAJI KUPITIA MAAFA ILIYOWATOKEA WATU PUANI:

    1.AJALI YA BASI SINGIDA-Julai, 2007
    -Watu walifakamia kuingia katika basi lililokuwa linawaka moto ili kupora mali baada ya basi kuanguka na kulipuka kutokana na hitilafu ya umeme, matokeo yake wote wakaungana na abiria waliomo ndani kuelekea ahera!

    2.MAFURIKO JANGWANI-Disemba, 2011
    -Watu walifakamia matairi ya magari na mifuko ya simenti kutoka ktk ghala lilibomolewa na maji ya mafuriko, matokeo yake wote wakaenda ahera!

    Tujitahidi kujikomboa kutoka katika makucha ya umasikini angalia sasa watu wanafikia malengo ya kimaisha kwa njia hatarishi, wanaponea njaa kupitia Maafa!

    ReplyDelete
  13. Ugumu wa maisha isiwe sababu ya kufanya vitu hatarishi kwa maisha. Hiyo ni ujinga wa kutokujua madhara yanayoweza kutokea endapo mlipuko wa moto utatokea. Hata huyo polisi na yeye ataungua licha ya kusimamia uhalifu badala ya kuhakikisha watu hawafanyi uhalifu. Lakini hii ndiyo KASI MPYA ya JK na wenzake. Watu wamedumaa akili kiasi wanasubiri mana ishushwe toka mbinguni kama wana wa Israel. Hawataki kufanya kazi halali. Polisi naye inaonekana ameshikishwa uchache ili aache waendelee na shughuli yao. Yale yale ya Bulyankulu, polisi wanalinda mashimo ili watu wasiingie humo wanapewa urua na kuwaruhusu. Serikali inakuja kufukia wanasema hakuna watu huko chini. Tutafika?

    ReplyDelete
  14. Hii nadhani itakuwa ni dizeli au mafuta ya taa. Kama ingekuwa ni petroli hawa wote saa hizi wangekuwa ni marehemu.

    ReplyDelete
  15. kinamama kachoteni maji acheni kuhatarisha maisha yenu na watoto

    ReplyDelete
  16. Mdau wa 03:49 umesema ukweli, mbona na huko UK na hata Marekani kukitokea vya dezo huwa wanaviiba kwa wingi tu, kwa hivyo usiwalaumu wa Tz eti wajinga.

    Na hawa madereva wa magari ya aina hii mimi naamini huwa wameshaiba mafuta halafu wanafanya upuuzi wa kuyapindua ili yasifahamike wameiba kiasi gani.

    Mbona wao siku zote huwa hawafi wala hawaumii?

    ReplyDelete
  17. Ooooooo lalala............bizness as usual. Ngoja litokee la kutokea usikie viongozi wetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...