Na Francis Godwin, Iringa
Wakazi wa Tanangozi na Ihemi katika wilaya ya Iringa vijijini katika harakati za kukinga mafuta kutoka kwenye lori la kusafirisha mafuta lenye namba T 575 AXH lililoanguka na kumwaga mafuta katika barabara kuu ya Iringa-Mbeya eneo la Ihemi, huku polisi wakishuhudia bila kuchukua hatua zozote endapo mlipuko utatokea.
Ni jambo la kushangaza sana kuwa baada ya visa vya watu kulipukiwa na moto wa mafuta ya dizeli au petroli si tu nchini mwetu bali hata nchi jirani kama vile Kenya, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nigeria nk, licha ya habari na taarifa hizo za kutisha ambazo zimeua maelfu ya watu, watu bado wanasogelea hatari hiyo.
Ni kama vile tahadhari zinazotolewa za kutokukaribia hatari hiyo zinapuuzwa, au watu wana kiburi kwa kujiamini wao ni spesheli na wajuzi zaidi kamwe hawawezi kukumbwa na hatari au ni ujinga ama kutokujali na kusingizia maisha magumu.
Kama hiyo haitoshi, wanaonekana baadhi ya askari nao ambao jukumu lao la msingi ni kulinda usalama wa raia katika hali yoyote, anaonekana kukubaliana na kinachotendeka mbele ya macho yake. Nilitarajia wawe mstari wa mbele kuweka utepe wa njano kuzunguka eneo lenye lori hilo na kuhakikisha yeyote anavuka utepe huo anatiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani kwa kuhataria maisha yake, ya jamii na kukiuka maelekezo halali ya askari.
Kweli, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa!" - Hosea 4:6
Usiwalaumu sana hawa ni ugumu wa maisha umewafikisha kwenye hatua hii ya kujihusisha kwenye matukio hatarishi!! Maosha yamekuwa magumu sana kiasi cha watu kuamua liwalo na liwe!!
ReplyDeleteMungu wangu mnakumbuka yale ya watu wa ile sehemu waligeuka ndafu wa sherehe.
ReplyDeleteyani sisi watanzani ni mawazo mgando kweli kweli yani hata kufikiri hatufikirii dah! hii siilishawai kutokea na wa2 wakafa vibaya mno jamani.
ReplyDeleteMungu weee, wa picha ya pili wanaonekana wamepanga foleni kabisa na watoto mgongoni.Inaonekana polisi yupo kukusanya "ushuru" kwa wanaotaka kushota hayo mafuta.
ReplyDeleteLakini picha inaonyesha direction ya ilo lori ni Dar es salaam so lipo tupu.
Maneno ya Mungu kuwa Nukuu..."Tazama Watu wangu wana angamia kwa ujinga wao".Mwisho wa nukuu.
ReplyDeleteWatu wamekuwa wana angamia ki rahisi rahisi tu kwa kukosa maarifa na busara.
Kila la heri na Tanzania yetu yenye ujinga tele.
serikali ya tanzania inaongoza wapumbavu wengi na viongozi wako happy kwa hilo kwa kuwa hata mkiibiwa na kudanganywa mtakubali...mimi naamini kabisa asilimia ya watu wenye elimu ni ndogo sana na ndio maana watu kama kina babu wa loliondo wakiibuka wajingani wengi wa kuwafuata.
ReplyDeletejamani mbona binadam saa nyingine tunakua na akili za kuku. yaani watu wenye akili timamu wataweza kujaribu kuchota hayo mafuta wakati wanajua moto unaweza anza hapo na watu wote waliopo hapo wakafa. huyo polisi aliyekuwa hapo anatakiwa ashtakiwe kwa uzembe wake. haya mambo yamekua yakitokea africa mara nyingi na unafikiri watu watajifunza lakini wapi. i hope vyombo vya habari na serikali wata waelimisha wananchi kuhusu hatari za mafuta.
ReplyDeleteHakuna tafauti katika ya UK na TZ. Hau wadau wanaonyesha ni watu wenye afya kamili isipokuwa yapo mafuta ya bure kwahivyo wanachangamka kama vile walivyofanya London wakati wa ghasia za Totenham kuvamia maduka ya simu na TV!!
ReplyDeleteHuyu baba aliyekuwa anaendesha hili lori ni nini kilimtokea ni mambo kulala usingizi nini?
ReplyDeleteMdau, technically sioni sababu ya wewe kukandia sana police sababu kama lori limeanguka tayari na kila kitu kipo intact kama inavyoonekana kwa picha mtu unaweza kinga hayo mafuta si sawa na kwenda petrol station hamna tofauti. ila tu watu asiwashe moto, sigara au kujaribu kutoa battery la lorry. au we unaonaje?
ReplyDeleteembu yaone yalivokaaa na wengine wamebeba na watoto kabisa shuwaini hawawazi hatari ambayo inaweza ikawapata hapo!
ReplyDeleteJamani njaa mbaya!
ReplyDeleteMIFANO YA UNUFAIKAJI KUPITIA MAAFA ILIYOWATOKEA WATU PUANI:
1.AJALI YA BASI SINGIDA-Julai, 2007
-Watu walifakamia kuingia katika basi lililokuwa linawaka moto ili kupora mali baada ya basi kuanguka na kulipuka kutokana na hitilafu ya umeme, matokeo yake wote wakaungana na abiria waliomo ndani kuelekea ahera!
2.MAFURIKO JANGWANI-Disemba, 2011
-Watu walifakamia matairi ya magari na mifuko ya simenti kutoka ktk ghala lilibomolewa na maji ya mafuriko, matokeo yake wote wakaenda ahera!
Tujitahidi kujikomboa kutoka katika makucha ya umasikini angalia sasa watu wanafikia malengo ya kimaisha kwa njia hatarishi, wanaponea njaa kupitia Maafa!
Ugumu wa maisha isiwe sababu ya kufanya vitu hatarishi kwa maisha. Hiyo ni ujinga wa kutokujua madhara yanayoweza kutokea endapo mlipuko wa moto utatokea. Hata huyo polisi na yeye ataungua licha ya kusimamia uhalifu badala ya kuhakikisha watu hawafanyi uhalifu. Lakini hii ndiyo KASI MPYA ya JK na wenzake. Watu wamedumaa akili kiasi wanasubiri mana ishushwe toka mbinguni kama wana wa Israel. Hawataki kufanya kazi halali. Polisi naye inaonekana ameshikishwa uchache ili aache waendelee na shughuli yao. Yale yale ya Bulyankulu, polisi wanalinda mashimo ili watu wasiingie humo wanapewa urua na kuwaruhusu. Serikali inakuja kufukia wanasema hakuna watu huko chini. Tutafika?
ReplyDeleteHii nadhani itakuwa ni dizeli au mafuta ya taa. Kama ingekuwa ni petroli hawa wote saa hizi wangekuwa ni marehemu.
ReplyDeletekinamama kachoteni maji acheni kuhatarisha maisha yenu na watoto
ReplyDeleteMdau wa 03:49 umesema ukweli, mbona na huko UK na hata Marekani kukitokea vya dezo huwa wanaviiba kwa wingi tu, kwa hivyo usiwalaumu wa Tz eti wajinga.
ReplyDeleteNa hawa madereva wa magari ya aina hii mimi naamini huwa wameshaiba mafuta halafu wanafanya upuuzi wa kuyapindua ili yasifahamike wameiba kiasi gani.
Mbona wao siku zote huwa hawafi wala hawaumii?
Ooooooo lalala............bizness as usual. Ngoja litokee la kutokea usikie viongozi wetu.
ReplyDelete