NA Khadija Khamis–Maelezo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee (pichani) amesema kuwa Serikali inapofanya maamuzi, ya kuuza Mali au Majengo huuza kutokana na uchakavu wa majengo hayo kwa utaratibu maalumu uliowekwa na Serikali.

Ameeleza kuwa Serikali haikurupuki kuuza majengo yake ila kuna utaratibu maalumu ambao hutumika kwa kukaguliwa na wakaguzi wa Serikali kisha hufanya maamuzi yakinifu .

Hayo aliyasema leo huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni, Nje kidogo na Mji wa Zanzibar, wakati alipokuwa akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma ,aliyetaka kujua ukweli wa Jengo la Makao Makuu ya zamani ya Wizara ya Elimu .

Alisema kuwa jengo hilo lililokuwa la Wizara ya Elimu liliyopo Shangani Mjini ni Jengo la zamani ambalo limejengwa kwa kutumia malighafi ya mawe na chokaa kutokana na uchakavu mkubwa wa Jengo hilo Serikali mnamo mwaka 2010 iliamua kuliuza .

Aidha alisema kuwa Jengo hilo limeuzwa kwa Said Salim Awadh Raia wa Tanzania kwa lengo la kuliendeleza na baadae kulitumia kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa .

Waziri huyo alieleza kuwa kuuzwa kwa majengo ya Serikali kunatokana na kujali zaidi usalama wa raia ambao hutumia majengo hayo machakavu,

Akifahamisha utaratibu ambao unafanyika alisema kuwa kabla ya kuuzwa kwa kitu chochote cha Serikali ni lazima kikaguliwe na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kisha kutangazwe kwa Tenda , na kwa njia ya Mnada na pia akijitokeza mtu ambae ataomba kukinunua Serikali ikiridhia atauziwa .

Omar alisema kuwa kuuza Majengo ya Serikali kiholela si rahisi kwani Mali zote za Serkali huu.zwa kwa idhini ya Serikali yenyewe .

Jengo hilo la Wizara ya Elimu limeuzwa oktoba 2010 kwa dhamani ya sh Billion moja na nusu za Kitanzania .na Fedha hizo zimewekwa kwenye mfuko maalum wa kujengea Majengo mapya ya Serikali .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wewe kweli ni mzee kama jina lako,aliekwambie jengo likichakaa na ardhi inachakaa ni nani?kisiwa chenyewe ni kidogo mnataka kujenga baharini?sasa endeleeni kuyauza muone kama si mnatengeneza mifereji ya ufisadi maana baadae mtaanza kupangisha serikali kwenye majengo binafsi au kulipa wananchi fidia ya kubomolewa majengo ili mjenge ya serikali kama si kuishia kuiuza serikali kabisa.Heri mgeyaacha mje kuvionesha vizazi vijavyo ilipokuwa wizara ya elimu kuliko kuyauza,haya endeleeni bwana,si nyie mna mamlaka?

    ReplyDelete
  2. Ni nani aliyeona tenda ya jengo hili? ni lini na wapi palipoendeshwa mnada wa jengo hili?

    si jengo la wizara ya elimu, mambo msiige, starehe club, jumba la mchina la simu, yote yameuzwa bila ya wazanzibari kujuwa, hakujatangazwa tenda na wala hapakuwepo minada.

    Tunakumbuka wazi majibu aliyotowa rais wa zanzibar tulipojaribu kutaka kujua kwa nini jumba la mambo msiige linauzwa, kwa hivyo tusidanganyane bure!!!!!

    Majumba yanauzwa kwa kujuana, wakaguzi wa serikali na viongozi fulani fulani wanapata makato yao na sote tunajua hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...