WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kitengo cha Elimu na Sanaa ambao hivi karibuni waligoma kushinikiza kupatiwa fedha za kujikimu, jana walimaliza mgomo na kurejea madarasani.

Wanafunzi hao waligoma kwa lengo la kushinikiza uongozi kuwapatia fedha za kujikimu kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB).

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa harakati za kudai fedha za kujikimu, Rafiki Rufungo wameamua kurejea madarasani baada ya kuahidiwa kulipwa fedha hizo Ijumaa.

“Mgomo umesitishwa, tunasubiri Ijumaa ya wiki hii kulipwa fedha zetu kama tulivyoahidiwa na chuo,” alisema Rufungo.

Awali, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alithibitisha kuwa wanafunzi hao watalipwa kama walivyoahidiwa kwa kuwa tayari fedha zao zipo.

Wakati huo huo, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St John nao walianza masomo baada ya chuo hicho kufungwa kwa muda kutokana na vurugu za kudai kupatiwa fedha za kujikimu.

Ofisa Uhusiano na Msemaji wa chuo hicho, Karim Meshack alisema kuwa kazi ya kujisajili imekamilika juzi jioni na wanafunzi wameingia madarasani jana kuendelea na masomo.

“Wanafunzi wamemaliza kazi ya kujisajili juzi jioni na hali iko shwari kabisa, wameingia madarasani wanaendelea na masomo kama kawaida,” alisema Meshack.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...