Habari ndugu zamgu wabongo,
wabunifu huko china wanatatua matatizo ya TRAFIC JAM bila kubadilisha miundo mbinu yao , barabara zile zile , kinachoengezwa ni mstari wa rangi wapi bus hili jipwa lipite haya wakubwa wa mji tizameni  hicho kideo hapo chini na mpate ufumbuzi wa DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. nzuri sana ni wazo la ikweli

    ReplyDelete
  2. Hii yaweza kuwa suluhu mahala pengine si hapa kwetu ambapo watu kuheshimu sheria ni dhambi. Mdau asante kwa mchango ila ukitaka kuona uhalisi wa mambo kuwa nia ya kutaka kupunguza kero ya foleni haipo angalia: -mfumko wa biashara holela barabarani,-uegeshaji mbovu wa magari barabarani,-uwekaji wa matuta yasiyozingatia utaalamu bali kwa nguvu ya kisiasa nk. Haya yote hayahitaji uwekezaji mkubwa kuyadhibiti ila badala yake tunafikiria kama vile tunaota.

    ReplyDelete
  3. Itatuchukua karne 10 kufikiri kama wachina hawa

    ReplyDelete
  4. EE hiyo kali,,mdau unafikiri sisi wabongo hizo pesa tutazipatia wapi!kwanza ya kujengea hiyo reli,na kwa Bongo haitachukua hata miezi madreva wataigonga gonga mpaka itoke barabarani,kwa kuwa bongo hakuna usalama wa barabara,,Lakini hata hivyo iko bomba na inapendeza sana
    Ahlam ,,,UK

    ReplyDelete
  5. haya jamaa ni noma hakuna anaeweza kuwapata.....

    wakati bongo ndio kwanza tunaanza ujenzi wa kidaraja kimoja cha kutuvusha upande wa pili wa mji

    na ndio kwanza tanzania tunaanza mipango ya ujenzi wa highway za juu ambazo zitakuwa ni 2 ili kuepuka foleni za barabarani

    wenzetu wameshapita huko tokea miaka ya 1950 na sasa wanabuni tanali litakalotembea na huku linabeba abiria na kuwafikisha kwenye shughuli mbali mbali

    na hapohapo tanali hilo linalotembea litasaidia kupunguza msongamano wa magari.

    big up.

    ReplyDelete
  6. Daa mi huwa napenda kuona wachina wanavyoshambulia maendelea yaani kama ni timu uwanjani wachezaji wote kumi na moja hawakamatiki achilia mbali walio kwenye benchi. na hii yote ni uwekezaji mzuri kwenye sayansi na kujenga taifa lenye watu wanaofikiria kwa kiwango cha juu. Nilipata kuona Thesis ya mwanafunzi wa masters wa kichina anayefanya kozi ya Mawasiliano ya kiielektroniki kwa kweli mawazo aliyokuwa ameyajumuisha kwenye paper yake si ya kawaida na ndo maana unaweza kuona namna hoja ilivyojengwa kwenye hii video ya mtoa mada. kama ambavyo wadau wengine waliotangulia mambo haya kwetu ni ndoto kwa kuwa hatuheshimu sheria za mipango miji, waziri anasema watu wamevamia eneo la barabara kundi la wabunge linakimbilia kwa wziri mkuu kuomba watu wanendelee kuvamia! tutaishia kuona hivihivi kwa uchina

    ReplyDelete
  7. nadhani hata karne 10 ni kidogo labda 15. sisi tumezoea kuwa walaji tu. wengine watengeneze sisi tutumie. sisi ni jamii iliyojengwa katika misingi ya kutojitegema

    ReplyDelete
  8. unasema bongo kuwa na hiyo ni ndoto. uk ndiyo kwanza wanapigana kuwa na fast train sasa wakati huko china na japan zinashika kutu. maanake ni long long long time ago wanazo hizo.
    china ni fast developed country in da world wakifanya hiyo programme ujue tayari washaanza. bongo sahau. daraja la kigamboni bado kitendawili sembuse hiyo electric buses.

    ReplyDelete
  9. Hata nchi zingine za dunia ya kwanza can not pull this off, at least not in this decade.
    China inatajilika kutokana na tamaa za nchi tajiri kupeleka viwanda vyao huko shauli ya gharama nafuu za uzalishaji.
    Kumbuka Olympics,nchi tajili zilisema zinataka nazo ku-host coming Olympics but not anything close to what the Chinese did.

    ReplyDelete
  10. Basi hili linatumia umeme!!!
    Sorry Bongo, for that alone, you are out of prospective customer's list.

    ReplyDelete
  11. sisi tuanze kwanza na kusimamia sheria (law enforcement) haswa za barabarani tukiweza ndiyo turudi kwenye project kama. Vinginevyo itakuwa hadithi ile ile.

    mbeba box,
    culumbus,oh

    ReplyDelete
  12. Kwanza ili tuweze kusonga mbele lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu sheria za miji. Kusiwe na mmoja anasimamia sheria wengine wanasema hana utu. Hii ni kudumaa kimawazo. Pili watanzania tuwe na uzalendo na nchi yetu. Siyo mtu akipata madaraka anafikiria kula tu.

    ReplyDelete
  13. Hatukuweza hata kuyakumudu makumbakumba. Yoyote anayeyakumbuka makumbakumba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...