wanakikundi wa mradi wa shamba darasa wa Kijiji cha Kaoze wakiimba wimbo maalum wa shamba darasa.
shamba darasa lililopandwa kitaalam lililopo katika kijiji cha Kaoze wilaya ya Sumbawanga.
baadhi ya wanakikundi cha CHEMKA wakiwasikiliza wataalam wa kilimo(hawapo) pichani walipowatembelea kijijini kwao Kaoze wilaya ya Sumbawanga.
Baadhi ya Maafisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na wakulima wakikagua shamba darasa katika kijiji cha Kaoze wilaya humo juzi.

NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA SUMBAWANGA

VIKUNDI vya wakulima katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vimeanza kufaidika na miradi ya kilimo kupitia Mashamba Darasa inayodaiwa kuwaongezea mbinu za kisasa za kilimo bora hali inayotarajiwa kuwaongezea mavuno na kipato ikiwa ni juhudi za kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini.

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha CHEMKA kilichopo katika kijiji cha Kaoze kilichopo bonde la ziwa Rukwa walisema wamenufaika sana na elimu ya mradi wa shamba darasa uliotekelezwa katika kijiji hicho na kwamba wamekuwa wakipoteza mazao mengi kwa kulima kilimo cha kiasili.

Walisema kuwa, kwa kipindi kirefu wamekuwa wakivuna magunia matatu mpaka matano kwa hekari moja walipokuwa wakilima kilimo cha asili lakini kwa kilimo bora cha kisasa wanategemea kupata magunia 25 mpaka 30 kwa hekari moja hivyo wanategemea kujiongezea kipato na kujikwamua katika umasikini.

Kwa mujibu wa Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Shaaban Bahari, Halmashauri hiyo ina jumla ya mashamba Darasa 151 katika vijiji mbalimbali wilayani humo na kwamba hali hiyo inatarajiwa kuwafaidisha wakulima.

“Tunategemea miradu hii itawasaidia wakulima wetu kujiongezea mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa ikiwemo matumizi ya mbolea, kupanda kwa kuzingatia nafasi, pamoja na kutumia mbegu bora” alisema Juma.

Miradi hiyo ya mashamba darasa inatekelezwa na wilaya hiyo katika vijiji na Kata mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wakulima wilayani humo, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea pamoja na mbinu nyingine za kilimo cha kisasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mfano mzuri sana wa kuigwa na songeni mbele daima! imependeza

    ReplyDelete
  2. Hilo shamba limepandwa kitaalam vipi? Bibi yangu alikuwa anapanda mahindi hivyo hivyo miaka ya themanini. Sioni la ajabu hapo.

    ReplyDelete
  3. La ajabu ni ongezeko la mavuno au hujaona kuwa wenyewe wamesema kuwa mavuno yameongezeka?

    ReplyDelete
  4. Wewe anony wa Wed Jan 25, 04:54:00 PM 2012 siyo lazima kitu kiwe cha ajabu ndiyo kiitwe cha kitaalamu. Inawezekana kabisa bibi yako alikuwa akipanda kitaalamu.

    Kuna vitu vingi tu wazee wetu walikuwa wanafanya kitaalamu ingawa hakikuwa kimeandikwa popote. Tunakosea tunapokuwa tunaoanisha kusoma na utaalamu. Unaweza ukawa mtaalamu wa kitu ili hali hujui kusoma.

    Wenu mtanzania

    ReplyDelete
  5. Jamaa wangetuwekea more details hapo mfano.. mbegu ngapi kwa shimo, umbali wa shimo na shimo, umbali kutoka mstari had mstari, aina ya mbegu na mbolea ya kutumia ningefurahi zaidi maana nina mkakati wa kujikita kwenye kilimo maana naona hapa mjini hailipi bora nikakomae na kale kashamba kangu pale kijijini for 5 yrs am sure nitarudi town kifua mbele.. wataalam naomba mnirushie hizo data..

    ReplyDelete
  6. huyo wa pili kulia kwenye picha ya kwanza na picha ya mwisho nilifikiri ni ankali nayeye ana shamba lake huko sumbawanga

    nilianza kumuogopa ankali maana sumbawanga mmhh

    ReplyDelete
  7. jina la kundi walibadilishe mi sijalipenda, litawaafect saikolojikale. Kwa nn wajiite CHEMKA? Watachemsha shaur yao

    ReplyDelete
  8. Safi sana wakulima wa Sumbawanga, hayo ndo maendeleo. Nimependa 'Ze fulanazz' ya mdau.

    ReplyDelete
  9. Unaweza kuwa na mashamab darasa hata mia,lakini je walengwa wanaelewa wanachofundishwa?
    Mimi nashauri,mabwana shama watumie pikipiki zinazowekwa mafuta na serikali kukagua na kusimamia mashamba ya wanchi ili yafuate utalaam katika hatua zote.Pia huwezi kuvuna wakati umelima kwa jembe la mkono,kwani trecta linachanganya udongo vizuri na linatifua ardhi tofauti na mkono.
    JE TUTAFIKA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...