Kadri siku zinavyozidi kwenda na ndivyo jiji letu la Dar linavyozidi kupendeza kwa vikwangua anga vya kisasa na mvuto mkubwa kwa wageni wanaotembelea nchini,.au wadau mnaonaje??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Jamaa wanajenga majumba makubwa tu, lakini miundo mbinu hamna. Utajengaje majumba makubwa wakati mabomba ya maji masafi na machafu ujapanua?!!, bara bara ziko vile vile? Umeme haueleweki-ngoja ukwame ghorafani kazi ya kutelemka na joto la bongo kama lift hazina umeme. Ingebidi jamaa wanaotoa vibali vya ujenzi wanawaambia hao jamaa wanaojenga hizo nyumba lazima waweke bajeti ya miundo mbinu kwenye bajeti yao.

    ReplyDelete
  2. Hivi ankali unafikiri wageni wanataka kuona vikwangua anga au wanavutiwa na hivyo vikwangua anga au wanachokifata na kuwavutia ni wanyama pori na mambo ya makumbusho

    vikwangua mawingu vitawasaidia nini wageni? Huko watokapo kuna vikwangua nyota na mwezi leo hii watafata vikwangua anga vyetu?

    Sema tu mji unazidi kujibana na joto linaongezeka maana kila mtu anajenga mjini.

    ReplyDelete
  3. Majengo tu .. tunaendelea vizuri ila jiji ni chafu sana...

    ReplyDelete
  4. Maendeleo mazuri...endapo tu kama ni kwa pesa halali na kwa uhalali.

    ReplyDelete
  5. Anony 12.35 AM, Kwako wewe wageni ni wazungu tu? Hujui kwamba Zambia, Malawi, Burundi, Rwanda na Uganda aliyefika Dar anaonekana mjanja? Basi watu hao wakirudi kwao ni simulizi hasa!Angalia pande zote, wenye kupenda wanyama wapo na magorofa na barabara za lami kutoka boda moja na nyingine wapo pia!

    ReplyDelete
  6. Kaka hapo umeongea kwanza majengo yawepo ndipo sewage system zitaboreshwa kulikingana na mahitaji,umeme tutapata wa kutosha maji, changamoto ni kwa je watumiaji wapo. hata Us haikujengwa miaka 50 kama watu wanavyofikiria ni zaidi ya miaka 200 sasa ww badala ulete mabadiliko nchini mwako kwasababu selikali imekusomesha kama sio ww mzazi wako halafu taaruma unayo uko uko hacha kulalamika njoo utoe ideas na co polojo tuuu.

    ReplyDelete
  7. hayo majengo bado mafupi sana,malaysia hayo ndiyo condominium kila kona ghorofa si chini ya 20,miundo mbinu hipo nyumba za chini zilishapotea na ghorofa 10 zinavunjwa kujengwa 22 hadi25,bonde kama msasani pale kunajengwa magorofa na packing za akika ni basi tu umimi mwingi hata kimala yakisimama magorofa ya hakika si kukimbilia town,mji sasa ufike chalinze tunataka,nitaleta tren ya umeme kama ngeleja akiwa mkweli

    ReplyDelete
  8. Anko kweli wewe unahitaji maombi tena Makubwa saaana INAWEZA kujifananisha na WATU ambao wamejioganize na miji Yao ni misafi Kama blantaya miji ambayo bado ina room ya kuongeza miundombinu sio KWAMBA wazamnia au wamalawi wanafurahii wanashanga Hawa WATU walivyo dis organized unajenga sky scraper chini unabara bara aliyo itumia mjerumani MWAKA 1897 akiendesha farasiii are u OKEY KWELI

    ReplyDelete
  9. Mdau wa 5 Anony Fri Jan 27,03:08:00 AM 2012

    Nakuunnga mkono sio tu Zambia,Malawi,Burundi,Uganda na Rwanda...pia wajanja Wa Congo na Wa Kenya wanaojiita wameendela kuliko sisi Dar na TZ wanaijua ilivyo na mtu anaetoka huku akienda huko au mtu wa huko kuja huku ni Kijiko sana kwao!

    Mfano Wa Congo pale Keys Hotel huwa wanasena Ahhh Dari Salamee ni bahari ya raha Madamee Muzuri ni Weupee (Machangu Doa),,,nagoma telefone wanikatie MAKUTA!,,,(napiga simu wanitumie PESA!)

    ReplyDelete
  10. Ujinga mtupu, tunaondoa majengo mazuri ya miaka ya 60 na kujenga maboksi ya vioo... anyway, kama ndio maendeleo basi tulipaswa kuyajenga along Sam Nujoma na Mandela rds, kwa sababu huko tuna muindombinu mizuri inayoruhusu flow nzuri ya magari

    ReplyDelete
  11. KAMA MJI WA DAR ES SALAAM UNGEBAKI NA MAJENGO YA ZAMANI KWA KUYATUNZA. MJI MPYA UKAAMIA SEHEMU NYINGINE HUU UKABAKI KAMA ULIVYOKUWA NA MAHITAJI YAKE. MPYA UKAJENGWA NA KUWEKEWA HUDUMA KULINGANA NA MAHITAJI YAKE.

    ReplyDelete
  12. Kati yenu kuna mwenye apartment hata mmoja?

    ReplyDelete
  13. Ongeeni yote lakini mnashau kua hayo majengo yenyewe...zaidi ya 70%hayana viwango thabiti ngojeni lipite tetemeko la ardhi (siombei hivyo)kwa sekunde chache alafu mtanipa ripoti.....

    ReplyDelete
  14. HEHEHE MDAU UMEULIZA SWALI ZURI SANA

    KATIKA WOTE HAPA TUNAOTOA MAONI NA KUPIGA POLOJO KAMA MASKANI JE KUNA MMOJA ANAEMILIKI HATA KIGOROFA KIMOJA?

    TUTABAKIA KUPIGA DOMO NA KUOSHA VINYWA TU NCHI INA WENYEWE SISI WASINDIKIZAJI TU

    TUSUBIRI UCHAGUZI TUWAPE WANAOJUWA KULA KURA ZAO ZA USHINDI ALAFU SISI TUBAKIE NA STORY ZETU ZA KIJIWENI

    ReplyDelete
  15. vikwangua anga havinogi kama havina umeme manake lift hazifanyi kazi ofisi ipo gorofa ya 12 pachungu hapo! halafu parking za tabuu wakati inatakiwa vikwangua anga viwe na parking za kufa mtu, umeme full time maji full time vyoo viwe visfi nk, sio majengo tuu ndani full joto!

    ReplyDelete
  16. Anonymous wa Fri Jan 27, 01:04:00 PM 2012 na Fri Jan 27, 10:12:00 AM 2012

    Kutoa hoja ni kuendeleza mji na jamii kwa ujumla, siyo lazima uwe na gorofa au nyumba. Kwani vyote vinatugusa wote, kwani tunaweza kuwa tunapanga nyumba, ofisi au maduka kwenye hayo majengo na itilafu yoyote ikitokea hapo inagusa wewe au mimi. (Ndiyo hapa, mtandao, ni kama kijiweni tunavyoongea), lakini ongea kitu cha kutuendeleza. Kama hauna wazo sio lazima kuoropoka mbofu mbofu. Wenzetu (mataifa mengine)wanatumia mtandao kubadilishana mawazo kama hapa, kudadsi fikra za watu zikoje. Tukisema tuna gorofa fulani si utaona kama tunajigamba? Vile vile matajiri wangapi umewaona wanajigamba eti haya magorofa yangu? Kwa hiyo kwa vile weye hauna gorofa, basi haki ya kuongea hauna? kwa vile wewe masikini huwezi ukagusika na hayo magorofa?, kwa mfano kama jamaa mmoja alivyosema hapo juu, je tetemeko likitokea unadhani hayawezi kudondokea watu wengine au mwenye gorofa tu ndio anaingia hasara? Je unadhani kodi yako haifanyi kazi kutoa mikopo ya kujenga miuondo mbinu ambayo inasadia hayo magorofa? maswali ni mengi mno. Kumbuka mtu siyo kisiwa. Kumbuka Bill Gates aligundua mtandao, lakini wengi wengi tunahutmia.

    ReplyDelete
  17. Taswira ya Dar es Salaam inaharibiwa. Hakuna standard za ujenzi. Hapa ghorofa refu, jirani nyumba ndogo yenye choo cha magunia. Ghorofa zingine hazina naasi kati yake unaweza kutokea dirishani la moja na kuingia la nyingine. Bado ni kutengeneza ghetto (slums) lakini mara hii ni za ghorofa. Ugly planning and architecture. Anayeona kuwa ni majengo ya kisasa basi tu ahurumiwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...