Maryam Ussi namba yake ni 0654336459, hakika anahitaji msaaada wa hali na mali kutokana na kubahatika kupata watoto watatu mapacha kwa wakati mmoja.watoto wanatumia maziwa LACTOGEN NO 2. yaani kwa siku anatumia kopo zima na linaisha.hatari......sasa huyu ana mapacha watatu na hana kazi ni mama wa nyumbani tuuuuuu!!!


HIVYO SHIME SHIME WADAU NAOMBA MUMSAIDIE MAMA HUYU MWENYE MAPACHA WATATU NAKUWASILIANA NAE MCHEKI KWENYE NAMBA 0654 336459 anahitaji maziwa pamoja na vitu vingine ambavyo ni muhimu kwa malezi ya watoto.

Watanzania wote na taaasisi mbali mbali husika tafadhali tunawaomba msaidieni huyu Mama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. poor her! cute kids

    ReplyDelete
  2. kwanza kabisa nampa huyu mama hongera kwa kujaaliwa kupata watoto watatu kwa pamoja.....na pili ninaungana na wengine watakaojihusisha katika kumsaidia huyu mama ni kweli kabisa anahitaji msaada

    kwa upande wangu nitafanya mawasiliano na huyu mama ili nijaribu kumsaidia nitakachojaaliwa na wengine msisite kumsaidia.

    shukrani sana michuzi kwa habari hii.

    ReplyDelete
  3. Si jambo baya kumsaidia huyu mama, ila taarifa imeshindwa kuwajulisha wadau details za baba wa watoto.

    Ujumbe unasema kuwa mama hana kazi, jee baba yao anafanya kazi gani? Anasaidiaje familia yake?

    ReplyDelete
  4. Naona sasa imekuwa mtindo mtu akiona ugumu wa maisha anaingia kwenye blogu. Huyo baba wa hao watoto yupo wapi na anafanya nini? Huyo ndiye mwenye jukumu la mwanzo kuhakikisha hao watoto wanapata matunzo stahiki. Asiingie mitini awajibike. Ukipanda michongoma huna budi kuitunza ili ipendeze.

    ReplyDelete
  5. BABA WA HAO WATOTO YUPO WAPI ???!!!

    ReplyDelete
  6. jee huyu bibi ameolewa au amekwenda kujitafutia tu?

    Ikiwa ameolewa ni jukumu la mume kutafuta na ahakikishe habebi mimba nyengine mpaka baada ya miaka mitano.

    Ikiwa hakuolewa huko ni kuzini na hiyo ndiyo faida ya kuzini. Mwenyezi Mungu amekataza sana zinaa, tujitahidi kuepuka hili.

    Otherwise siku hizi maisha ni magumu sana siyo ya kuchezea.

    ReplyDelete
  7. Ni Jambo jema sana kwa watanzania kusaidiana kwani huo ndiyo utamaduni wetu. Lakini kabla ya kutoa misaada watu huwa na maswali ya kuuliza ili kujiridhisha kuwa wanapeleka michango yao mahali stahiki.

    Ni dhahiri kuwa huyu mama kapata watoto hao kwa kushirikiana na mzazi mwenzake( Mume, boyfriend etc utakavyomwita). Swali ni je mwanamume ambaye yupo responsible na watoto hao anamsaidia?, kamkimbia?, hajulikani?. Nafikiri maswali haya yangekuwa yamejibiwa kwenye maelezo ya kuomba msaada nina imani tupo wengi tutakaojitokeza kumsaidia.

    Ahsante!

    ReplyDelete
  8. Hana shida angekuwa na shida angewapa hao watoto maziwa ya ng'ombe. Hata wenye watoto mmoja mmoja wengi tu hawana uwezo wa kununua Lactojen

    ReplyDelete
  9. Mwenyezimungu amlindie wanae kwa elimu na maisha bora, mie naona hizo pesa ziende kwa vyakula ila kama mtu anauwezo angemsaidia tu huyu mama elimu na njia ya kazi awatizame wanae vizuri la sivyo vyakula vitaisha itarudi palepale, khalid.

    ReplyDelete
  10. Baba wa watoto hao aanze kwanza kuwasaidia watoto wake. Akishindwa, ajitokeze kuomba msaada.

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana kabisa kuwa huyu mama hakuzaa MAPACHA WATATU, bali kazaa watoto watatu. Kiswahili sanifu cha pacha ni vitu viwili. Ukisema pacha watatu, maana yake huyu mama kazaa watoto sita! Kama hivyo ndivyo,hao wengine wako wapi? Watanzania msiharibu Kiswahili. Kwa tabia hii ya kujifanya hamnazo, sasa Wakenya watautangazia ulimwengu kwamba Kiswahili asili yake ni Kenya, ilhali sote tukijua kuwa huo ni uwongo.

    Nasisitiza: Watoto hao ni watatu, na si mapacha watatu! Mapacha watatu ni watoto sita!!!

    Muhunda

    ReplyDelete
  12. mi natumia mpesa weka namba ya voda ka hana yeye hata ya mumewe au wakala atakayempa pesa niwasilishe kateni kangu.

    ReplyDelete
  13. Ankal, nadhani wadau wangependa kupata taarifa zaidi kuhusu huyu mama na watoto wake. Kwa mfano, swali ambalo linakujia moja kwa moja akilini baada ya kusoma taarifa hii ni: baba wa watoto hawa yuko wapi? Wadau wangependa kupata taarifa zaidi ili waweze kuamua endapo kweli mama huyu anastahili kusaidiwa.

    ReplyDelete
  14. Mbona huongelei baba wa watoto?

    ReplyDelete
  15. kwa kweli mungu ni mwema.Ila ushauri wangu kwa hali ya maisha ya sasa,msaada atakaopatiwa awaanzishie maziwa ya ng'ombe.Hela anayowanunulia kopo la lactogen kwa siku anaweza kuwalisha maziwa ya ngombe hata siku 3.

    ReplyDelete
  16. NANI ALIYEMWAMBIA AWE MAMA WA NYUMBANI?YATIMA WASAIDIWE NA YEYE KHAAA!TUTOLEENI HAPA BAADA AOMBE KAZI YEYE ANAOMBA MAZIWA HANA AKILI KWELI.KAKA NAOMBA UMPE KAZI HUYO DADA NDO MSAADA WA MAANA.NAONA ANAPENDA KUPEWA MAISHA NI MAGUMU SIKU ZA MWISHO HIZI JAMANI.

    ReplyDelete
  17. mpachika mimba yukwapi?

    ReplyDelete
  18. Mbona kuna watu wengi wanatafuta watu wa kazi za nyumbani au hata shule za watoto chekechea ambapo anaweza kuenda hata na watoto wake. Pamoja na kusaidiwa naye pia inabidi achakarike.
    Kusema ukweli natamani hao watoto

    ReplyDelete
  19. hilo ni wazo zuri sana lakini baba wa mapacha watatu yuko wapi?????????

    ReplyDelete
  20. Nafikiri wengi wetu tungependa kujua Baba ya hao malaika yuko wapi na anafanya shughuli gani.Ikiwezakana na kipato chake pia.Maana tusije tukanya watu wakakimbia majukumu yao.

    ReplyDelete
  21. Hongera dada umebarikiwa saaaaaana

    ReplyDelete
  22. Jamani embu asasi zinazo shughulika na masuala ya wanawake, this is a genuine case. Msaidieni huyu mama tusiendelee kuona tangazo lake, anatia huruma sana jamani.

    ReplyDelete
  23. mme wake yupo hai???baba ya watoto wapo hai?tupe ukweli na hali halisi.

    ReplyDelete
  24. MwanaSekapamaJanuary 18, 2012

    Kwa kweli UMOJA mo NGUVU na UTENGANO ni UDHAIFU, KUSAIDIANA ni MUHIMU, na IMEHIMIZWA, KIDINI, KIMILIA na KIJAMII, mimi namhurumia sana huyu dada, hasa nikiwaangalia hao MALAIKA wa ALLAH, huu ni USHAURI TU, Mimi nadhani KUMSAIDIA huyu dada ni kujaribu kumtafutia ufumbuzi wa KUDUMU, kama mtaji wa kufanya biashara kwa mpango na muelekeo ITHIBATI ili aweze kujikimu vizuri, kwani mahitaji ya hao viumbe ni mengi tu, kuliko kumpa vitu rejareja, kuna methali ambayo naambiwa ni ya kichina, kuwa ukitaka kumsaidia mwenye, mfundishe kuvua,(kwa kumpa nyenzo na ujuzi) usimpe samaki mmoja moja kila siku, kwani akijuwa kuvua, ataweza kuvua samaki wengi, wengine akala wengine akauza, kipatao akajikimu na mambo mengine, basi jamani tumsaidie huyu kwa njia ya ufumbuzi wa muda mrefu. Nawasilisha Hoja, Mwanasekapama.

    ReplyDelete
  25. ongera mama kwa watoto watatu,,Ma'ansha'Allah Mwenyezi Mungu akukuzie.Mimi naona huyu aliyesaidia kumuweka humu,angesaidia pia kupeleka katika vyombo vya habari za huko home,maana watu wanaongalia internet kwa nyumbani ni wachache sana,hasa katika TV magazeti na pia katika makampuni ya tigo voda,,ili wachangie kwa haraka msaada huwo..hata watu wakituma mia tano tano au mia tatu tatu,hata kwa cash au msg,,pesa itatosha ya kuwatunza watoto,,Mwenyezi Mungu akulainishie jambo hili
    Ahlam..UK

    ReplyDelete
  26. baba alielenga hilo shimo mpaka wakashinda ushindi wa kishindo wa magoli matatu 3 yupo wapi au hamjui alieshinda hayo magoli?

    ReplyDelete
  27. Mazingira ya taarifa hii yanaonyesha na kuthibitisha pasipo shaka kuwa hakuna baba wa damu anayehusika na watoto hawa watatu,
    Mimi najitokeza kuwasaidia watoto na MAMA YAO kama huyo Mama anaafiki.
    Ankal, nitumie ujumbe wa siri kwenye e-mail yangu kama yuko tayari.

    Kidume Cha Mbegu, New York

    ReplyDelete
  28. Kwa kweli baba wa watoto hawa angejitokeza kuomba msaada tungeelewa na tungemkimbilia. mama kuja peke yake inaleta maswali. Tupeni taarifa kamili msitutege.

    ReplyDelete
  29. haaaaaaaa Jesus Alahu Akbaruuu hivi kweri hawa watanzania wakiombwa msaada wanakashfu hivi sasa naomba mungu hawa wote wanaokashfu na kuandika vibaya mungu awape maisha marefu yenye hukumu kali ya kukashfu watu, hata kama wana vipato mungu awaonyeshe namna mtu masikini anavyopata taabu, wasife bila ya kupata taabu

    ReplyDelete
  30. Acheni hizo. Wako wenye shida siyo huyo. Kwanza Ustawi wa jamii huwaga wanatoa msaada kwa mapacha wanapozidi wawili lakini hata hivyo mzazi mwenzie ndiye anawajibu wa kazi walioifanya. Tunasaidiaga waliopatwa ajali na mambo ya majanga siyo ya starehe.

    ReplyDelete
  31. mwe! kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  32. waombwa msaada wakali hao mmhh!! mama anajuta kujitokeza

    ReplyDelete
  33. imenibidi nicheke wadau wakali hao; ugumu wa maisha upo popote nashangaa mama huyu kukimbilia lactogen ambayo mwananchi wa kawaida hawezi ku-aford!! atumie maziwa ya ng'ombe na uji mwepesi sana kwa wanawe; mtu unashida alafu bado unachagua vitu vya gharama kweli ni akili au matope?

    ReplyDelete
  34. WEWE MDAU HAPO JUU UNAELAANI WATU,KWANI WEWE UMEKUWA NANI,,WEWE NDO UMELAANIWA,,KUSEMA JESUS NA ALLAHU WAQBARU!
    KWANI WATU KUTAKA KUJUWA BABA WATOTO KUNA UBAYA GANI,MUNGU NDO KAKATAZA ZINAA,,SASA WATU KUULIZA ILI WAPATE USAHIHI WA MAMBO,ILI MSAADA YAO WAITOE KWA ROHO MOJA.KUNA BABA MMOJA ALIJITOKEZA NA YEYE HANA KAZI,NA ALIKUWA NA WATOTO WATATU(MAPACHA),,,MBONA ALIHUDUMIWA NA MICHANGO NA KUTAFUTIWA AJIRA,,,NA AKARUDI TENA KUSHUKURU,,,HUYU DADA ANGESEMA KUWA LABDA MUME WAKE KAFARIKI,AU KAMTELEKEZA,HAPO SAWA,WALA USINGEONA COMMENTS ZA KASHIFA,,,KILA MTU ANGETOA KIMYA KIMYA,,WATANZANIA TUNA ROHO NZURI SANA NA TUNALIELEWA HILO!,,,ACHA KUWALAANI WATU,,MWENYE UWEZO WA KULAANI NI MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE...AHLAM,,,UK

    ReplyDelete
  35. Mama ana bahati huyu mweee, sasa vipi Ankal, kidume cha mbegu from New York kashabeba jumla jumla au bado?

    ReplyDelete
  36. ankali nimekuchunguza habari yenye kutumiwa comment nyingi unaichelewesha kuitoa

    kumbe nawewe mwenyewe ankali ni mmoja wa waosha vinjwa unapenda sana mambo ya kushadidia hahaha

    ReplyDelete
  37. Jamani watu wakusaidia wla hawaulizi maswali maswali, ni kutoa tu. anagalia hao watoto hawana makosa hapa ni malaika tu, saidieni, wale masikini wanaomba huwa mnawauliza maswali khaaaa! mmenikera na mikono yenu ya birika loh! Tenda wema uende zako, no question

    MUNGU AWABARIKI HAO WATOTO,WAPATE WATU WA KUWAPENDA NA KUWASAIDIA HII NJIA TU MUNGU AMEMTUMIA HUYO MAMA KUWALETA WATOTO HAO,

    ReplyDelete
  38. awape maziwa ya ng'gombe asishindane na wenye nazo angekuwa na shida asingetaka hayo maziwa ya lactogen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...