Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia wakitelemka eneo la Mahakamani  leo  kutoka kwenye Lori lililowabeba wakisafiri kwenda nchini Afrika Kusini mara baada ya kukamatwa Mwishoni mwa wiki.
 Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia wakitelemka eneo la Mahakamani  leo kwenye Lori lililowabeba wakisafiri kwenda nchini Afrika Kusini mara baada ya kukamatwa Mwishoni mwa wiki.

 Baadhi ya Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia wakipatiwa kifungua kinywa kabla ya kupandishwa Mahakamani
 Mmoja wa Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia akisoma majina ya wenzake kwa ajili ya kuingia mahakamani kusikiliza kesi yao , Wahamiaji hao walikamaatwa mwishino mwa wiki na kufikishwa Mahakamani hapo
Wahamiaji haramu wa Raia wa Ethiopia wakiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro wakisubiri kusomewa mashitaka yao.

Habari na Picha na John Nditi, Morogoro

WAHAMIAJI haramu 98 wa kutoka nchini Ethiopia, pamoja na Watanzania wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali,ikiwemo ya wahamiaji hao kuingia nchini bila kuwa na hati za kusafiria wala kibali kutoka Mamkala za Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Watanzania waliofikishwa Mahakamani hapo jana na kusomewa mashita yao ni Emili Kimario (33) mkazi wa Rombo, Mkoani Kilimanjaro ambaye ni  Dereva wa Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 718 AZY mali ya Emmanuel Juma ,pamoja na msaidizi wake , John Kisima (28) mkazi wa Himo, Mkoani Kilimanjaro ambaye ni ndugu mwenye Lori hilo.

Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Evodia Kyaruzi, Mwendesha Mashitaka wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Morogoro,Helmina Foya, akidai kuwa washitajiwa hao wawili ambao ni Watanzania wanathumiwa kuwasaidia raia wa Ethiopia 98 kuingia nchini bila kuwa na nyaraka halali pamoja na hati za kusafiria.

Pia alidai kuwa mnamo Januari 19, mwaka huu majira ya saa moja usiku eneo la Melela , Wilaya ya Mvomero , Mkoani Morogoro kuwa wakiwa ni madereva wa Lori la mizigo waliwabeba raia wa Ethiopia na kuwasafirisha wakati wao wakiwa hawana vibali wala hati za kusagiria sambamba na kutumia gari la mizigo kubeba abiria raiaa wa kigeni na kuwaingiza nchini.

Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo, Kyaruzi, alipowata wajibu tuhuma hizo, kwa nyakati tofauti walikana kuhusika na kosa hilo , hata hivyo Mwendesha Mashitaka wa Idara hiyo aliiomba Mahakama kutotoa dhamana kwa watuhumiwa kufuatia kuonekana ni wazoefu wa usafirishaji wa Wahamiaji haramu.

Mwendesha Mashikata huyo alidai kuwa Watanzania hao walikamatwa miezi miwili iliyopita ( Mwaka jana) wakiwasafirisha wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 103 kwa kutumia Lori hilo na baada ya kupigwa faini kwa mara nyingine limetumika kusafirisha wengine.

Hata hivyo Hakimu wa Mahakama hiyo alizingatia hoja ya upande wa Mashitaka kwa kukubaliana na hoja hiyo na kuzuia kutoa dhamana kwa watuhumiwa hao hadi suala hilo litakapokamilika.

Kwa upande wa kesi ya Wahamiaji hao haramu wa kutoka Ethiopia, Mwendesha Mashitaka huyo wa Idara ya Uhamiaji, aliomba mbele ya Hakimu  kuisogeza mbele  ili kutoa muda wa kumpata mkalimali wa kutafasiri lugha ya kihabeshi kwenda kiingereza na kiingereza kwenda kihabeshi kwa vile walikuwa hawafahamu lugha ya kiingereza.

Hata hivyo Hakimu wa Mahakama hiyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu itakapotajwa tena sambamba na watanzania hao wawili , hivyo wote kurudishwa rumande hadi siku hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. wameshtakiwa kwa kubeba watu katika gari ya mizigo...na hapo kwenye picha naona wamefikishwa mahakamani kwa kutumia gari ya mizigo. SHERIA OYEEEEEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  2. Acheni kuwanyanyasa wenzenu, hao wanaelekea South Africa. Bongo nini watafanya?

    ReplyDelete
  3. We anony wa 10:37a.m,jaribu ww kupita nchi za watu kinyemela uone.sasa hapo wananyanyswa au sheria inafata mkondo???ebu nyamaza.

    ReplyDelete
  4. Nashauri ujumbe utumwe kwa serikali ya south africa kuuliza kama wanahitaji watu hao waingie nchini kwao.Unajua kwa sisi tunaoishi Euro,Kusema kweli Wasomali na hasa wa kawaida na wale maskini wanateseka sana.Na wakiona jua wanajua Mungu amewavusha kweli.Kila kukifika jioni hawana uhakika wa kuamka keshoyake.
    Mungu wasaidie wasomali,Mungu ibariki africa,Mungu tuepushe na vita ili africa iwe moja na watu wake wawe wamoja.
    Siku ikitokea Tanzania,khali kama ya wasomali,TUTAKIMBILIA WAPI?

    ReplyDelete
  5. Hao ni economic refugees. Wakabidhini kwa serikali yao ya Ethiopis kwa usmaria wema. Ndiyo wamevunja sheria sababu ya njaa tumieni uanadamu.Italy wanaingia sana wakimbizi haramu lakini wengi wao wanapewa refugee status na wengine kurudishwa. Hao ndugu zetu waafrica ajamani waoneeni huruma.

    ReplyDelete
  6. Kwakweli wanatia huruma sana kuona binaadamu wanahangaika huku na kule na yote husababishwa na serikali za Afrika kutokujali raia wao.Na huko South Africa nako ni yaleyale tu hakuna uhakika kiivo,na isitoshe hao wa south Africa hawapendi wageni na wapo tayari hata kuua.Ni vijana wapo ktk harakati za kutafuta maisha hata sisi ni hayo hayo tu tumezagaa duniani karibu kote,mwenyezi mungu atawasaidia na sisi vilevile.
    Good Luck

    ReplyDelete
  7. nyinyi wabongo mna hela ya kuwalisha na kuwahudunia hawa au basi mlikuwa mnataka rushwa watu wenyewe mmewakamata njaa kali mnataka kujionyesha mnawajibika upuuzi mtupu

    Mdau
    Somalia

    ReplyDelete
  8. wengine tunaondoka, wengine wanakuja, da

    ReplyDelete
  9. unajitia gharama za kijinga. Kama ni wapita njia wasindikizeni waondoke wanakoelekea.
    Wakigomea hapo na kuomba ukimbizi mtawakatalia wakati haki za binadamu na ukimbizi zinawalinda.
    Tunajitia mizigo ya kijinga bure wakati sheria hatujui. Hapo kinachowazwa ni rushwa...mnahesabu vichwa.
    Dover wa kirkuk, wa iraq, afghanistan na waafrika wanadakuliwa kila kukicha lakini police border wanachfanya ni kuwarudisha calais, france. Hawapelekwi jela wala wapi. Ndo tabu ya kuongozwa na viongozi darasa la saba.

    ReplyDelete
  10. Mbona kuna wazamiaji kibao Afrika Kusini wanatoka bongo, wapo pia Ulaya na Marekani? Hebu waacheni hao ni ndugu zetu japo Wa Ethiopia wanajifanya si Waafrika....!!Wasameheni bure.....!! Mdau-NYC, USA

    ReplyDelete
  11. maskini wanatia huruma!!

    ReplyDelete
  12. Masikini, wamechokaaaaa

    ReplyDelete
  13. Ndio maana nchi kama Tanzania haziendelei. Jamani tuwekeni mazingira mazuri ya kuwakaribisha watu ambao wapo tayari kufanya kazi. Pia kama wanapita njia kwenda South Africa. Waachieni jamaini.

    ReplyDelete
  14. Kwa kweli hii siyo sawa kabisa. Hawa waafrika wenzetu wanasafiri na wamepita njia tu kwa nini kuwafanyia unyama namna hii.

    Waacheni wapite waende zao huo Africa kusini.

    Waafrika tutaheshimiana lini? Kazi kulaumu wazungu na kuingilia magomvi ya nchi kubwa huku wananchi wenu hamuwajali kabisa.

    Mungu tunakuomba uwasaidia waafrika wenzetu wanaohangaika kutafuta maisha ili watunze familia zao. Amina

    ReplyDelete
  15. Kosa kubwa kubeba watu kwenye Lori, na nyinyi je mkishitakiwa na Wadau wa haki za binadamu, mtasemaje?

    ReplyDelete
  16. Hilo lori lipigwe mnada hela itakayopatika ndio itumike kuwahudumia pamoja na kuwasafirisha hao jamaa kurudi kwao haraka iwezekanavyo..hakuna sababu ya kuwasweka jela kwani ni kujiongezea gharama..hao wapumbavu wawili ndio wana kesi kwani inaonekana wazoefu...utakuwa mwisho wao lori likitaifishwa..mwenye lori nadhani nae anahusika,haiwezekani lori likamatwe mara ya 1,halafu acmfukuze kazi huyo dereva..hilo ni dili lao wote

    ReplyDelete
  17. acheni hizooo wala hawana mpango wa kuishi bongo hapo ni kama wapo transit tuu, na hata kama wamekuja kujitafutia maisha wabongo wangapi wamejilipua ughaibuni? roho mbaya tuu.

    ReplyDelete
  18. Wawarudishe tu kwao Ethiopia watafute njia nyingine ya kwenda Afrika kusini. Hakuna faida kwa kuwafunga jela

    ReplyDelete
  19. Watanzania kuweni na moyo wa uruma.kumbukeni sisi site ni ndungu watoto Baba mmoja.Kumbukeni sote tupo hapa kwa mipango ya Mungu kwa hio hakuna raia haramu hapo mnakufulu tuu.na Kama ninyi ni raia halali ishi milele.wenzenu ni watafutaji wanaenda zap south nyie mmewakatizia safari yao wakishinda hiyo kesi meafikishe Huko waaliko kua wakienda kutafuta Maisha.Tanzania juuuuuuuuuuu lakini zaidi.

    ReplyDelete
  20. any human rights lawyers in bongo awasaidie hao. Ona wanavyoshuka, where is the duty of care? Ughaibuni huwezi kufanya hivyo, mfungwa akianguka, serikali italipa mamilioni. Hakuna mzaha hata kidogo. Hao sio wahalifu, serikali ingwwarudisha kwao mara moja.

    ReplyDelete
  21. Sawa kwenda South Africa hawakatazwi isipokuwa watumie njia zinazokubalika kisheria na kiutaratibu kama Kutumia Pasipoti, Kuwa na viza za huko waendako na kupita katika Mipaka na Vivuko vyetu Tanzania kwa njia ya halali.

    ReplyDelete
  22. Kwanini mnatuongezea gharama ya kutunza watu wote hao. Baki na watanzania na hao wahabeshi rudisha nyumbani kwao kwa kutumia ghari hilo hilo. Msitumie vibaya hela za watanzania walio masikini.

    Au vinginevyo waache waendelee na safari yao ili mradi wasibaki tanzania kwani haya jamaa ni makatili.

    ReplyDelete
  23. hawajui nchi za kuhamia.

    ReplyDelete
  24. NCHI IMEKWISHA!!!. Usalama wa taifa wako wapi, watu wanasafiri kilomita zote hizo ndani ya nchi. ingekuwa wakati wa mwalimu ingeingia hata kilomita moja ndani ya nchi bila kukamatwa.

    Kwa hali ilivyo sasa adui anaweza kuingiza jeshi zima ndani ya nchi yetu sie tumelala. kama hawa wamekamatwa 100 inamaana walishapita zaidi ya 1,000.

    Juzi juzi mshikaji mmoja kasafirisha kiloba cha ndizi (risasi na bunduki za kivita)toka mwisho wa reli hadi Dar. Kwa maoni yangu alikamatwa kwa bahati mbaya na ndizi nyingi zilisha sambazwa kwa walaji hapa Dar na mikoa mingine.

    Enzi za Mwalimu kila mahali kulikuwa na mashushushu kuanzia vijijini hadi mijini. Miaka ya 60, 70 na 80 we acha tu, muulize Idi Amini na watawala wa kikoloni kusini mwa Afrika kila mbinu waliyotumia walinaswa.

    ReplyDelete
  25. Hivi kwa mwendo huu itokee tuwe na bifu na akina Elishabibi kama ilivyo kwa jirani zetu hapo pande za kaskazi, si watatumaliza!!!

    ReplyDelete
  26. Wasituingizie Gharama za bure!

    Cha msingi wafungwe huku wakifanyishwa kazi zinazolipia gharama yao ya Huduma za Magereza na FAIDA JUU!

    Sio watuingizie gharama kwa hela ya Walipa Kodi wa Tanzania kuwalisha bureee Wahabeshi wasafiri haramu.

    Tukumbuke kama JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) ni sehemu ya Uzalishaji Ujenziwa Taifa na Ulinzi,,,basi GEREZANI IWE NDIO ZAIIIIDIII!.

    ReplyDelete
  27. jamani hao ni wakimbizi,wamekimbia makwao sababu ya shida,mie sioni kuna sababu gani ya kuwafungulia mashitaka,huo ni unyanyasaji wa kijinsia jamani..

    ReplyDelete
  28. AIBU KUBWA KWA AFRIKA KUWATENDEA UNYAMA WAAFRIKA WENZENU

    AFRIKA TUTAZIDI KUWA CHINI NA TUTAENDELEA KUWA WATUMWA IKIWA WENYEWE HATUPENDANI

    HAO NI WAKIMBIZI WA KIAFRIKA WANAPASWA KUNYANYASWA NCHI NYINGINE ZISIZO ZA KIAFRIKA LAKINI SIO AFRIKA KUWANYANYASA NDUGU ZAO

    HAPO TANZANIA WANAPITA NJIA TU NA WALA HAWANA SHIDA NA NCHI HIYO

    ILITAKIWA WATENDEWE WEMA HATA WAKIFIKA HUKO WENDAPO WATUSIFU NCHI YETU KUWA NA UKARIMU NA ROHO YA UPENDO

    LEO HII UTAKUJA KUKUTANANAO KATIKA MAISHA UTASEMA WEWE MTANZANIA HAWATOKUONA KUWA NI MTU WA NCHI NZURI

    WATAKUONA KUWA NI MTU WA NCHI YA WATU WENYE ROHO MBAYA HATA KAMA UNA SHIDA NINA HAKIKA HAWEZI KUKUSAIDIA

    WASAIDIENI WAAFRIKA WENZETU WAPITA NJIA ILI NASISI KESHO TUSAIDIWE KWENYE NCHI ZA WATU TUKIPITA NJIA

    KUMBUKENI KUWA SHIDA HAINA MMOJA.

    MUNGU WASAIDIE HAWA WAKIMBIZI

    DINI ZOTE ZINA NENO MOJA KUWA MSAIDIE MWENYE SHIDA AU MKIMBIZI

    MPOKEE MGENI WOWOTE ATAKAEFIKA MLANGONI KWAKO.


    KWA UWEZO WA MUNGU MAHAKAMA MSHINDWE.

    ReplyDelete
  29. NYIE MSIJAZE WATU MAGEREZANI MNAITIA SERIKALI GHARAMA ZISIZO ZA LAZIMA WAPENI MTAA HAO JAMAA WAJIACHIE WANAPOTAKA KWENDA MBONA WAJOMBA ZETU WALITUMIA NJIA HIZO HIZO ZA BODA KWA BODA HADI GREECE

    ReplyDelete
  30. Hao jamaa wangelikuwa ni wazungu basi Gov ya bongo ingewaachia tu lakini vile ni Wa Africa wenzetu ndio wanataka kuwaonea tu.....Pale JK Int Air port Wazungu ndio wanaopita bila kufanyiwa matatizo yeyote yale lakini ukipita mwa Africa wee utakoma kila mfanyakazi pale airport atataka kujua mpango wako vipi watakupelekesha hao mpaka utajuta kupita katika hiyo air port wakati ni Mwafrika mwenzao. Wazungu pale wanapita na uzito mkubwa wa unga ki ulaini kabisa.

    ReplyDelete
  31. Hahahhaha watanzania eti mna huruuuma, wangekamatwa nchi nyingine mngesikia vile wangefanyiwa!hapo ni sheria ifuate mkondo wake, Tanzania Oyeee, watu wana huruma hadi raha ndo maana mnaendelea!

    ReplyDelete
  32. Mimi kweli naona suala la usalama wa taifa ndo concern. Annoy uliyesema kuwa enzi za mwalimu wasingefika hata maili moja ni kweli. Hii inaonyesha kuwa mipaka hailindwi inavyopaswa...!! Kwahiyo wamekamaiwa Morogoro?? Aibu kweli..wapite kote huko waje kukamatiwa Morogoro? Katikati ya nchi???
    Mdau-USA

    ReplyDelete
  33. Mdau Tue Jan 24 03:35:00 umenena kabisa hakuna watu wanaotaka rushwa kama wa Airport,,na hasa ukiwa mtu mweusi,,,na ukisikika unaongea kiswahili na una pass ya nje unakamatwa na kuulizwa umeipataje,,,yaani hawa watu wanallaaana,,,Wewe masikini vijana wa watu wanajipitia tu,,mnawatesa hivyo kwa ajiri gani,,si muwaache wapite?kwani wamepita nchi ngapi kwa usalama tu,,nyie wabongo ndo mnawatesa hivyo,,,tena huko mikoani ndo usiseme ni wanyanyasaji kweli kweli,,Hata Mungu atawaathibu kwa kuwatesa viumbe vyake namna hiyo,,,Mimi naona ubalozi wa Ethiopia wawasaidie watu wao ili warudi home,,au kama kweli walikuwa wanaenda South wawaachie waende,,kama ni maneno tu walikuwa wanaazamia tu hapo TZ basi muwape hifadhi,,maana TZ inajulikana kwa Amani uwenda walikuwa wanakuja tu hapo Bongo,,waacheni jamani vijana wadogo bado wanatafuta maisha,,,Ahlam ,,,UK

    ReplyDelete
  34. Hiyo gharama yote ya kuwaweka rumande ni kubwa sana, la muhimu mngewarudisha uhabeshini au muwakabidhi UNCCR, kuwaweka rumande ni kuwatesa tu, kwani wako katika utafutaji, hawajamuibia mtu sana sana wamechukua nafasi za sisi tuliopo nje, kudadadadadaki wapeni mtaa hao bana. Ingekua hivyo wengi wetu huku Ughaibuni tungekufia rumande. Mjomba Michu mwenyewe unalijua hilo. Asanteni wadau tuwaombee warudishwe kwao. Mdau Mbegu.Kwa wachonga

    ReplyDelete
  35. Anony wa nane toka juu SADATAAA.
    Africa ni moja na waafrica wote ni ndugu zangu.

    Ni wazi bila kificho hata sisi waTZ kuna wakati utafika tutakuwa hivi katika nchi za waafrica wenzetu. kwa nini viongozi wa juu wasiongee na viongozi wenzao kuhusu swala la wakimbizi?

    ReplyDelete
  36. waacheni waingie then serikali ianzishe kambi ya wakimbizi. kwani unafikiri wale walio kigoma wakifanya kazi muyovosi na lugufu wataenda wapi wateja wakirudi kongo? bora kuwaandalia mazingira ya kambi mpya wapate ajira!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...