Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia wakitelemka eneo la Mahakamani leo kutoka kwenye Lori lililowabeba wakisafiri kwenda nchini Afrika Kusini mara baada ya kukamatwa Mwishoni mwa wiki.
Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia wakitelemka eneo la Mahakamani leo kwenye Lori lililowabeba wakisafiri kwenda nchini Afrika Kusini mara baada ya kukamatwa Mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia wakipatiwa kifungua kinywa kabla ya kupandishwa Mahakamani
Mmoja wa Wahamiaji Haramu raia wa Ethiopia akisoma majina ya wenzake kwa ajili ya kuingia mahakamani kusikiliza kesi yao , Wahamiaji hao walikamaatwa mwishino mwa wiki na kufikishwa Mahakamani hapo
Wahamiaji haramu wa Raia wa Ethiopia wakiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro wakisubiri kusomewa mashitaka yao.
Habari na Picha na John Nditi, Morogoro
WAHAMIAJI haramu 98 wa kutoka nchini Ethiopia, pamoja na Watanzania wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali,ikiwemo ya wahamiaji hao kuingia nchini bila kuwa na hati za kusafiria wala kibali kutoka Mamkala za Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Watanzania waliofikishwa Mahakamani hapo jana na kusomewa mashita yao ni Emili Kimario (33) mkazi wa Rombo, Mkoani Kilimanjaro ambaye ni Dereva wa Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 718 AZY mali ya Emmanuel Juma ,pamoja na msaidizi wake , John Kisima (28) mkazi wa Himo, Mkoani Kilimanjaro ambaye ni ndugu mwenye Lori hilo.
Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Evodia Kyaruzi, Mwendesha Mashitaka wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Morogoro,Helmina Foya, akidai kuwa washitajiwa hao wawili ambao ni Watanzania wanathumiwa kuwasaidia raia wa Ethiopia 98 kuingia nchini bila kuwa na nyaraka halali pamoja na hati za kusafiria.
Pia alidai kuwa mnamo Januari 19, mwaka huu majira ya saa moja usiku eneo la Melela , Wilaya ya Mvomero , Mkoani Morogoro kuwa wakiwa ni madereva wa Lori la mizigo waliwabeba raia wa Ethiopia na kuwasafirisha wakati wao wakiwa hawana vibali wala hati za kusagiria sambamba na kutumia gari la mizigo kubeba abiria raiaa wa kigeni na kuwaingiza nchini.
Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo, Kyaruzi, alipowata wajibu tuhuma hizo, kwa nyakati tofauti walikana kuhusika na kosa hilo , hata hivyo Mwendesha Mashitaka wa Idara hiyo aliiomba Mahakama kutotoa dhamana kwa watuhumiwa kufuatia kuonekana ni wazoefu wa usafirishaji wa Wahamiaji haramu.
Mwendesha Mashikata huyo alidai kuwa Watanzania hao walikamatwa miezi miwili iliyopita ( Mwaka jana) wakiwasafirisha wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 103 kwa kutumia Lori hilo na baada ya kupigwa faini kwa mara nyingine limetumika kusafirisha wengine.
Hata hivyo Hakimu wa Mahakama hiyo alizingatia hoja ya upande wa Mashitaka kwa kukubaliana na hoja hiyo na kuzuia kutoa dhamana kwa watuhumiwa hao hadi suala hilo litakapokamilika.
Kwa upande wa kesi ya Wahamiaji hao haramu wa kutoka Ethiopia, Mwendesha Mashitaka huyo wa Idara ya Uhamiaji, aliomba mbele ya Hakimu kuisogeza mbele ili kutoa muda wa kumpata mkalimali wa kutafasiri lugha ya kihabeshi kwenda kiingereza na kiingereza kwenda kihabeshi kwa vile walikuwa hawafahamu lugha ya kiingereza.
Hata hivyo Hakimu wa Mahakama hiyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu itakapotajwa tena sambamba na watanzania hao wawili , hivyo wote kurudishwa rumande hadi siku hiyo.
wameshtakiwa kwa kubeba watu katika gari ya mizigo...na hapo kwenye picha naona wamefikishwa mahakamani kwa kutumia gari ya mizigo. SHERIA OYEEEEEEEEEEEEEE.
ReplyDeleteAcheni kuwanyanyasa wenzenu, hao wanaelekea South Africa. Bongo nini watafanya?
ReplyDeleteWe anony wa 10:37a.m,jaribu ww kupita nchi za watu kinyemela uone.sasa hapo wananyanyswa au sheria inafata mkondo???ebu nyamaza.
ReplyDeleteNashauri ujumbe utumwe kwa serikali ya south africa kuuliza kama wanahitaji watu hao waingie nchini kwao.Unajua kwa sisi tunaoishi Euro,Kusema kweli Wasomali na hasa wa kawaida na wale maskini wanateseka sana.Na wakiona jua wanajua Mungu amewavusha kweli.Kila kukifika jioni hawana uhakika wa kuamka keshoyake.
ReplyDeleteMungu wasaidie wasomali,Mungu ibariki africa,Mungu tuepushe na vita ili africa iwe moja na watu wake wawe wamoja.
Siku ikitokea Tanzania,khali kama ya wasomali,TUTAKIMBILIA WAPI?
Hao ni economic refugees. Wakabidhini kwa serikali yao ya Ethiopis kwa usmaria wema. Ndiyo wamevunja sheria sababu ya njaa tumieni uanadamu.Italy wanaingia sana wakimbizi haramu lakini wengi wao wanapewa refugee status na wengine kurudishwa. Hao ndugu zetu waafrica ajamani waoneeni huruma.
ReplyDeleteKwakweli wanatia huruma sana kuona binaadamu wanahangaika huku na kule na yote husababishwa na serikali za Afrika kutokujali raia wao.Na huko South Africa nako ni yaleyale tu hakuna uhakika kiivo,na isitoshe hao wa south Africa hawapendi wageni na wapo tayari hata kuua.Ni vijana wapo ktk harakati za kutafuta maisha hata sisi ni hayo hayo tu tumezagaa duniani karibu kote,mwenyezi mungu atawasaidia na sisi vilevile.
ReplyDeleteGood Luck
nyinyi wabongo mna hela ya kuwalisha na kuwahudunia hawa au basi mlikuwa mnataka rushwa watu wenyewe mmewakamata njaa kali mnataka kujionyesha mnawajibika upuuzi mtupu
ReplyDeleteMdau
Somalia
wengine tunaondoka, wengine wanakuja, da
ReplyDeleteunajitia gharama za kijinga. Kama ni wapita njia wasindikizeni waondoke wanakoelekea.
ReplyDeleteWakigomea hapo na kuomba ukimbizi mtawakatalia wakati haki za binadamu na ukimbizi zinawalinda.
Tunajitia mizigo ya kijinga bure wakati sheria hatujui. Hapo kinachowazwa ni rushwa...mnahesabu vichwa.
Dover wa kirkuk, wa iraq, afghanistan na waafrika wanadakuliwa kila kukicha lakini police border wanachfanya ni kuwarudisha calais, france. Hawapelekwi jela wala wapi. Ndo tabu ya kuongozwa na viongozi darasa la saba.
Mbona kuna wazamiaji kibao Afrika Kusini wanatoka bongo, wapo pia Ulaya na Marekani? Hebu waacheni hao ni ndugu zetu japo Wa Ethiopia wanajifanya si Waafrika....!!Wasameheni bure.....!! Mdau-NYC, USA
ReplyDeletemaskini wanatia huruma!!
ReplyDeleteMasikini, wamechokaaaaa
ReplyDeleteNdio maana nchi kama Tanzania haziendelei. Jamani tuwekeni mazingira mazuri ya kuwakaribisha watu ambao wapo tayari kufanya kazi. Pia kama wanapita njia kwenda South Africa. Waachieni jamaini.
ReplyDeleteKwa kweli hii siyo sawa kabisa. Hawa waafrika wenzetu wanasafiri na wamepita njia tu kwa nini kuwafanyia unyama namna hii.
ReplyDeleteWaacheni wapite waende zao huo Africa kusini.
Waafrika tutaheshimiana lini? Kazi kulaumu wazungu na kuingilia magomvi ya nchi kubwa huku wananchi wenu hamuwajali kabisa.
Mungu tunakuomba uwasaidia waafrika wenzetu wanaohangaika kutafuta maisha ili watunze familia zao. Amina
Kosa kubwa kubeba watu kwenye Lori, na nyinyi je mkishitakiwa na Wadau wa haki za binadamu, mtasemaje?
ReplyDeleteHilo lori lipigwe mnada hela itakayopatika ndio itumike kuwahudumia pamoja na kuwasafirisha hao jamaa kurudi kwao haraka iwezekanavyo..hakuna sababu ya kuwasweka jela kwani ni kujiongezea gharama..hao wapumbavu wawili ndio wana kesi kwani inaonekana wazoefu...utakuwa mwisho wao lori likitaifishwa..mwenye lori nadhani nae anahusika,haiwezekani lori likamatwe mara ya 1,halafu acmfukuze kazi huyo dereva..hilo ni dili lao wote
ReplyDeleteacheni hizooo wala hawana mpango wa kuishi bongo hapo ni kama wapo transit tuu, na hata kama wamekuja kujitafutia maisha wabongo wangapi wamejilipua ughaibuni? roho mbaya tuu.
ReplyDeleteWawarudishe tu kwao Ethiopia watafute njia nyingine ya kwenda Afrika kusini. Hakuna faida kwa kuwafunga jela
ReplyDeleteWatanzania kuweni na moyo wa uruma.kumbukeni sisi site ni ndungu watoto Baba mmoja.Kumbukeni sote tupo hapa kwa mipango ya Mungu kwa hio hakuna raia haramu hapo mnakufulu tuu.na Kama ninyi ni raia halali ishi milele.wenzenu ni watafutaji wanaenda zap south nyie mmewakatizia safari yao wakishinda hiyo kesi meafikishe Huko waaliko kua wakienda kutafuta Maisha.Tanzania juuuuuuuuuuu lakini zaidi.
ReplyDeleteany human rights lawyers in bongo awasaidie hao. Ona wanavyoshuka, where is the duty of care? Ughaibuni huwezi kufanya hivyo, mfungwa akianguka, serikali italipa mamilioni. Hakuna mzaha hata kidogo. Hao sio wahalifu, serikali ingwwarudisha kwao mara moja.
ReplyDeleteSawa kwenda South Africa hawakatazwi isipokuwa watumie njia zinazokubalika kisheria na kiutaratibu kama Kutumia Pasipoti, Kuwa na viza za huko waendako na kupita katika Mipaka na Vivuko vyetu Tanzania kwa njia ya halali.
ReplyDeleteKwanini mnatuongezea gharama ya kutunza watu wote hao. Baki na watanzania na hao wahabeshi rudisha nyumbani kwao kwa kutumia ghari hilo hilo. Msitumie vibaya hela za watanzania walio masikini.
ReplyDeleteAu vinginevyo waache waendelee na safari yao ili mradi wasibaki tanzania kwani haya jamaa ni makatili.
hawajui nchi za kuhamia.
ReplyDeleteNCHI IMEKWISHA!!!. Usalama wa taifa wako wapi, watu wanasafiri kilomita zote hizo ndani ya nchi. ingekuwa wakati wa mwalimu ingeingia hata kilomita moja ndani ya nchi bila kukamatwa.
ReplyDeleteKwa hali ilivyo sasa adui anaweza kuingiza jeshi zima ndani ya nchi yetu sie tumelala. kama hawa wamekamatwa 100 inamaana walishapita zaidi ya 1,000.
Juzi juzi mshikaji mmoja kasafirisha kiloba cha ndizi (risasi na bunduki za kivita)toka mwisho wa reli hadi Dar. Kwa maoni yangu alikamatwa kwa bahati mbaya na ndizi nyingi zilisha sambazwa kwa walaji hapa Dar na mikoa mingine.
Enzi za Mwalimu kila mahali kulikuwa na mashushushu kuanzia vijijini hadi mijini. Miaka ya 60, 70 na 80 we acha tu, muulize Idi Amini na watawala wa kikoloni kusini mwa Afrika kila mbinu waliyotumia walinaswa.
Hivi kwa mwendo huu itokee tuwe na bifu na akina Elishabibi kama ilivyo kwa jirani zetu hapo pande za kaskazi, si watatumaliza!!!
ReplyDeleteWasituingizie Gharama za bure!
ReplyDeleteCha msingi wafungwe huku wakifanyishwa kazi zinazolipia gharama yao ya Huduma za Magereza na FAIDA JUU!
Sio watuingizie gharama kwa hela ya Walipa Kodi wa Tanzania kuwalisha bureee Wahabeshi wasafiri haramu.
Tukumbuke kama JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) ni sehemu ya Uzalishaji Ujenziwa Taifa na Ulinzi,,,basi GEREZANI IWE NDIO ZAIIIIDIII!.
jamani hao ni wakimbizi,wamekimbia makwao sababu ya shida,mie sioni kuna sababu gani ya kuwafungulia mashitaka,huo ni unyanyasaji wa kijinsia jamani..
ReplyDeleteAIBU KUBWA KWA AFRIKA KUWATENDEA UNYAMA WAAFRIKA WENZENU
ReplyDeleteAFRIKA TUTAZIDI KUWA CHINI NA TUTAENDELEA KUWA WATUMWA IKIWA WENYEWE HATUPENDANI
HAO NI WAKIMBIZI WA KIAFRIKA WANAPASWA KUNYANYASWA NCHI NYINGINE ZISIZO ZA KIAFRIKA LAKINI SIO AFRIKA KUWANYANYASA NDUGU ZAO
HAPO TANZANIA WANAPITA NJIA TU NA WALA HAWANA SHIDA NA NCHI HIYO
ILITAKIWA WATENDEWE WEMA HATA WAKIFIKA HUKO WENDAPO WATUSIFU NCHI YETU KUWA NA UKARIMU NA ROHO YA UPENDO
LEO HII UTAKUJA KUKUTANANAO KATIKA MAISHA UTASEMA WEWE MTANZANIA HAWATOKUONA KUWA NI MTU WA NCHI NZURI
WATAKUONA KUWA NI MTU WA NCHI YA WATU WENYE ROHO MBAYA HATA KAMA UNA SHIDA NINA HAKIKA HAWEZI KUKUSAIDIA
WASAIDIENI WAAFRIKA WENZETU WAPITA NJIA ILI NASISI KESHO TUSAIDIWE KWENYE NCHI ZA WATU TUKIPITA NJIA
KUMBUKENI KUWA SHIDA HAINA MMOJA.
MUNGU WASAIDIE HAWA WAKIMBIZI
DINI ZOTE ZINA NENO MOJA KUWA MSAIDIE MWENYE SHIDA AU MKIMBIZI
MPOKEE MGENI WOWOTE ATAKAEFIKA MLANGONI KWAKO.
KWA UWEZO WA MUNGU MAHAKAMA MSHINDWE.
NYIE MSIJAZE WATU MAGEREZANI MNAITIA SERIKALI GHARAMA ZISIZO ZA LAZIMA WAPENI MTAA HAO JAMAA WAJIACHIE WANAPOTAKA KWENDA MBONA WAJOMBA ZETU WALITUMIA NJIA HIZO HIZO ZA BODA KWA BODA HADI GREECE
ReplyDeleteHao jamaa wangelikuwa ni wazungu basi Gov ya bongo ingewaachia tu lakini vile ni Wa Africa wenzetu ndio wanataka kuwaonea tu.....Pale JK Int Air port Wazungu ndio wanaopita bila kufanyiwa matatizo yeyote yale lakini ukipita mwa Africa wee utakoma kila mfanyakazi pale airport atataka kujua mpango wako vipi watakupelekesha hao mpaka utajuta kupita katika hiyo air port wakati ni Mwafrika mwenzao. Wazungu pale wanapita na uzito mkubwa wa unga ki ulaini kabisa.
ReplyDeleteHahahhaha watanzania eti mna huruuuma, wangekamatwa nchi nyingine mngesikia vile wangefanyiwa!hapo ni sheria ifuate mkondo wake, Tanzania Oyeee, watu wana huruma hadi raha ndo maana mnaendelea!
ReplyDeleteMimi kweli naona suala la usalama wa taifa ndo concern. Annoy uliyesema kuwa enzi za mwalimu wasingefika hata maili moja ni kweli. Hii inaonyesha kuwa mipaka hailindwi inavyopaswa...!! Kwahiyo wamekamaiwa Morogoro?? Aibu kweli..wapite kote huko waje kukamatiwa Morogoro? Katikati ya nchi???
ReplyDeleteMdau-USA
Mdau Tue Jan 24 03:35:00 umenena kabisa hakuna watu wanaotaka rushwa kama wa Airport,,na hasa ukiwa mtu mweusi,,,na ukisikika unaongea kiswahili na una pass ya nje unakamatwa na kuulizwa umeipataje,,,yaani hawa watu wanallaaana,,,Wewe masikini vijana wa watu wanajipitia tu,,mnawatesa hivyo kwa ajiri gani,,si muwaache wapite?kwani wamepita nchi ngapi kwa usalama tu,,nyie wabongo ndo mnawatesa hivyo,,,tena huko mikoani ndo usiseme ni wanyanyasaji kweli kweli,,Hata Mungu atawaathibu kwa kuwatesa viumbe vyake namna hiyo,,,Mimi naona ubalozi wa Ethiopia wawasaidie watu wao ili warudi home,,au kama kweli walikuwa wanaenda South wawaachie waende,,kama ni maneno tu walikuwa wanaazamia tu hapo TZ basi muwape hifadhi,,maana TZ inajulikana kwa Amani uwenda walikuwa wanakuja tu hapo Bongo,,waacheni jamani vijana wadogo bado wanatafuta maisha,,,Ahlam ,,,UK
ReplyDeleteHiyo gharama yote ya kuwaweka rumande ni kubwa sana, la muhimu mngewarudisha uhabeshini au muwakabidhi UNCCR, kuwaweka rumande ni kuwatesa tu, kwani wako katika utafutaji, hawajamuibia mtu sana sana wamechukua nafasi za sisi tuliopo nje, kudadadadadaki wapeni mtaa hao bana. Ingekua hivyo wengi wetu huku Ughaibuni tungekufia rumande. Mjomba Michu mwenyewe unalijua hilo. Asanteni wadau tuwaombee warudishwe kwao. Mdau Mbegu.Kwa wachonga
ReplyDeleteAnony wa nane toka juu SADATAAA.
ReplyDeleteAfrica ni moja na waafrica wote ni ndugu zangu.
Ni wazi bila kificho hata sisi waTZ kuna wakati utafika tutakuwa hivi katika nchi za waafrica wenzetu. kwa nini viongozi wa juu wasiongee na viongozi wenzao kuhusu swala la wakimbizi?
waacheni waingie then serikali ianzishe kambi ya wakimbizi. kwani unafikiri wale walio kigoma wakifanya kazi muyovosi na lugufu wataenda wapi wateja wakirudi kongo? bora kuwaandalia mazingira ya kambi mpya wapate ajira!
ReplyDelete