Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, Halima Dendego, ( mwenye kuvaa kapero) akiwatuliza baadhi ya wananchi wa Vijiji vya Mambegwa na Msowero,ili awezekusikiliza kero yao iliyosababisha wachukue uamuzi wa kufunga Barabara ya Kilosa- Dumila kwa magogo na mawe makubwa , mara baada ya kuwasili eneo la tukio hivi karibuni na kufanikiwa kusuruhisha tatizo lililojitokeza kati ya wakulima na wafugaji.
Wananchi wa Kijiji cha Mambegwa na Msowero katika Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Halima Dendego ( hayupo pichani), alipozungumzanao baada ya kuziba kwa mawe makubwa na magogo Barabara ya Kilosa- Dumila eneo la Msowero,kwenye daraja la mto Msowero na kusababisha hadha ya usafiri wa magari ya abiria na mizingo, kama walivyokutwa juzi eneo hilo.
Baadhi ya wananchi pamoja na Askari wa Polisi wakipita kwa shida katika daraja la mto Msowero baada ya wananchi wenye hasira kufunga barabara ya Kilosa- Dumila, na kusababisha hadha kubwa ya magari kushindwa kupita akwa siku nzima ya kama ilivyokutwa eneo hilo.
Askari Polisi wakiwashikiria vijana waliojaribu kuleta fujo wakati wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro Halima Dendego (hayupo pichani) katika Kijiji cha Msowero,baada ya wananchi wa Vijiji vya Mambegwa na Msowero kuamua kufunga Barabara ya Kilosa- Dumila kwa magogo na mawe wakishinikiza kusikilizwa madai yao ya migogoro ya mipaka ya Vijiji vya wafugaji na wakulima kama walivyokutwa eneo hilo, hata hivyo Mkuu wa Wilaya alifanikiwa kuafikiana nao na kufungua njia hiyo saa 12 jioni baada ya kuifunga saa 12 asubuhi ya siku hiyo.
Mkazi wa Kijini cha Msowero, Tarafa ya Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, ambaye jina lake halikuweza kufahamika akibeba baiskeri yake begabi baada ya wananchi wenye hasira wa Kijiji cha Mambegwa kufunga barabara ya Kilosa- Dumila kwenye daraja la Msowero na kusababisha usumbufu na hadha kubwa ya magari kushindwa kupita kama ilivyokutwa katika eneo hilo.
Msururu wa magari ya abiria na mizigo yakiwa upande wa kutoka Dumila kwendaa Kilosa yakisubiri kufunguliwa kwa Barabara ya Kilosa – Dumila,Wilaya ya Kilosa, baada ya wananchi wenye hasira kufunga njia hiyo kwa kuweka mawe makubwa na magogo ili kushinikisha kusikilizwa na kutekelezewa madai yao dhidi ya wafugaji kama yalivyokutwa Msowero.Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jamani hao ni wapiga kura wetu,naomba wasikilizwe badala ya kupigwa na mabomu. Mpaka wamefikia hatua hiyo ina maana shida hazijafanyiwa kazi ipasavyo. Kumbukeni wakulima ndio wenye asili ya sehemu hiyo! Au ukarimu wao unawaponza?

    ReplyDelete
  2. alaf ndo mnawapa wawekezaji ardhi kama pipi na wakati sisi wenyewe iliyokuepo haitutoshi..

    ReplyDelete
  3. Jamani waandishi tilieni maanani sana lugha sahihi hasa katika tahijia (spelling) mwandishi wa habari hii hakuzingatia matumizi sahihi ya tahijia R na L kwa mfano neno kushikilia limeandikwa kushikiria, neno kusuluhisha limeandikwa kusuruhisha au neno adha limeandikwa hadha mara kadhaa na hivyo kupoteza maana halisi ya neno hilo hasa kwa wale wano jifunza lugha ya kiswahili. Nauliza hakuna mhariri anayewajibika kuzipitia ripoti kabla hazijachapishwa?

    ReplyDelete
  4. Mdau unaeskitika kwa kiswahili kilichotumika hapa..huyu muandishi sio kwamba kakosea no bali hajui kiswahili na mbaya zaidi watu km hawa huwa hawataki kukubali kwamba hawajui kiswahili hivyo itakua kazi ngumu kuwarekebisha.Mimi huwa nashangaa sana jinsi kiswahili chetu kinavyoharibiwa leo utaskia vijana wanasema GUBU(eti mwanaume ana gubu huyu) wakati usahihi ni BUGU au ZARURA badala ya DHARURA au kuchanganya matumizi ya BADALA na BAADA yani ni kichefuchefu kwakwenda mbele.Mimi sipingi maneno yamitaani ya vijana ila ninachopinga nikuyaandika,kuyatamka au kuyatumia vibaya maneno yakiswahili ama kuhusu lugha ya mitaani sawa inakubalika.

    ReplyDelete
  5. te!te! akina ras makunja mzigoni tena? eh! muziki huu wa sasa naona mkubwa

    ReplyDelete
  6. Tehe,tehe hiyo haitoshi baba kiswahili cha humu ni kibovu kila siku,angalia habari ya JK kuwasili Addis Ababa wameandika KUHUDHULIA badala ya KUHUDHURIA.

    ReplyDelete
  7. sawa wapiga kura, lakini wanatakiwa wamsikilize kiongozi ambbae amekuja kuwatatulia shida zao na sio kumzomea na kuleta fujo. Ukizomea wakati kiongozi wako anaongea unadhani utafanikiwa vipi? hata m/mungu hatokusikiliza kama huwaheshimu viongozi wako. Hongera police kwa kuwadhibiti hao waleta fujo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...