“ Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,
Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”
Ndugu zangu,

Hapa nanukuu gazeti la Mwananchi leo Jumatano; “Majuzi, Dk Magufuli alifanya ziara ya ghafla katika eneo la vivuko hivyo na kuwaambia wananchi waliomzomea kwamba kama wakishindwa kulipa nauli hiyo ya Sh200 ni vyema wakapiga mbizi baharini au kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au warudi vijijini wakalime.”- Mwisho wa kunukuu.
Utotoni katika Dar es Salaam hii, nilishuhudia kwa macho yangu msako wa wazururaji. Niliona jinsi mgambo wa jiji walivyokuwa wakiwadhalilisha vijana na watu wazima kwa kuwakamata, kuwafunga mashati na kuwapandisha kwenye malori tayari kwa safari za kwenda Gezaulole. Kosa lao, walikuwa wakizurura mijini bila kazi. Hivi, anayetafuta kazi atabaki nyumbani kuisubiri, si ni lazima apige mguu kuitafuta? Sijui leo ungefanyika msako wa wazururaji Dar yangehitajika malori mangapi?
Na miaka ile ya sabini tulipokuwa watoto tulisikia hata nyimbo za redioni kuhimiza ‘ wazururaji’ waende kwenye vijiji vipya vilivyoandaliwa na Serikali kama makazi ya ‘ Wazururaji’. Watoto wa enzi hizo huenda tunakumbuka wimbo huu;
“ Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,
Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”
Kigamboni ya enzi hizo ilikuwa shamba kweli. Wengi wa waliofikishwa huko Gezaulole na vijiji vingine kule Kigamboni wakayaanza maisha mapya ya vijijini. Kuna waliokimbia Gezaulole wakarudi tena mjini au kwenye vijiji vyao vya asili. Kuna waliobaki huko Gezaulole, wakafyeka mapori yao. Wakaanza kilimo, . Wakaizoea hali mpya. Wakajenga familia zao huko.
Ajabu, leo wenye fedha ndio wanaokwenda kuyanunua kwa bei ya hadaa, maeneo ya watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu. Kuna watoto na wajukuu wa ‘wazururaji’ waliobaki na vieneo vidogo. Miongoni mwao ndio hao wanaofanya shughuli za kusukuma mikokoteni na kuendesha maguta.
Ndio hao, waliokisikia kilio cha kutaka uwepo wa pantoni ya uhakika kwa miaka nenda , miaka rudi. Wamesikia kilio cha kujengewa daraja pia na ahadi zake. Na sasa wanaongezewa nauli ya kivuko kwenda na kurudi mjini.
Ni hivi; mkazi wa Magomeni hata kama hana nauli anaweza kutembea kwa miguu kukatisha Jangwani na akamwona mgonjwa wake Muhimbili, au kwenda kuhangaikia kibarua Kariakoo. Na jioni ikifika, hata kama hana nauli ya Daladala, atakatisha Jangwani na kufika Magomeni kwenye chumba chake cha kupanga.
Lakini, mkazi wa Kigamboni kama hana nauli ya mia tatu ya pantoni na kama anataka kuvuka kwenda kumwona mgonjwa wake Muhimbili au kuhangaikia kibarua Kariakoo ana mawili, kwa mujibu wa Magufuli; ama apige mbizi au azungukie Kongowe, kwa miguu, mwendo wa nusu siku kama si siku nzima. Na hapa ndipo ilipo hoja ya msingi ya kumfikiria mtu wa kawaida wa Kigamboni, Gezaulole na kwingineko ng’ambo ya pili ya bahari.
Vinginevyo, kwa kusema kuwa asiye na nauli arudi kijijini akalime ina maana pia, kuwa kuishi Jangwani, Mburahati na Mabibo kunaweza kuwa na nafuu zaidi kwa mtu wa Kigamboni mwenye hali ngumu kiuchumi. Kwamba hatimaye tunawaambia watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu; “Rudini mjini’. Na wimbo ule leo labda ungeimbwa hivi;
“ Mburahati mama, Mburahati baba ee,
Rudini Jangwani, na Mwananyamala kwenye maisha bora!”
Haki ya Mungu!
Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro.
http://mjengwablog.com
http://mjengwablog.com
Hii imenigusa ! nakumbuka huo mwimbo sana! na kuna kitu kimenigusa hicho cha kwamba mtu wa magomeni ataweza kukatiza JAngawani kwenda kumuona mgonjwa wake Muhimbili na je wa Kigaboni! tunaomba waziri mkuu atumie busara kumaliza hili na ikiwezekana nauli zipande lakinis i kwa asilimia mia moja !
ReplyDeleteMajid nilikuwa nakuheshimu sana, kwa makala hii umechemsha. sh 200/= unaona kuwa serikali imewaonea wakati huko vijijini kuna vivuko vinatoza mpaka sh 800/=. Watanzania tumezoea bure, unataka kulipa sh50 halafu upate huduma zote, hebu mwacheni Magufuli afanye vitu vyake. Alichosema magufuli ni sawa kabisa, hakuna kubembelezana, mambo ya kubembelezana si umeona yalivyotokea jangwani.
ReplyDeleteWakati Cleopa Msuya akiwa Waziri wa Fedha katika moja ya Hotuba zake za Bajeti (sikumbuki nimwaka gani) aliondoa nauli ya vivuko na kusema kama kungekuwa na daraja wananchi hawa wangevuka bila kulipa. Pia hii inatukumbusha kuwa enzi hizo kazi ya kupanga bei za huduma za Serikali zilifanywa kupiti bajeti ya Serikali siyo mtu anatoka hujo baada ya ulexi wa Xmass anatangaza bei mpy ya kivuko. Ukilionganisha kwa sasa nauli ya meli kweda Zanzibar ni ndogo kuliko kwenda Kigamboni; kwa maana ya aina ya huduma, speed, muda na risk. TAFAKARI
ReplyDeleteMwandishi tupunguze siasa na kutafuta cha kufanya kuhusu hili, kila upande una hoja za msingi, cha msingi ni kufikia makubaliano ya pande zote.
ReplyDeleteKuna njia mbali mbali zingetumika ili wananchi waendelee kupata huduma ya kivuko. Kuongeza kodi, kubinafsisha, na hii ya mtumiaji alipe papo hapo. Kwa vile hii huduma ni muhimu kwa raia wanaoishi hapo wananchi itabidi wachangie ili huduma iendelee vizuri. Na wale wasiokuwa na kazi wapewe barua na serikali yao ya mtaa ili waruhusiwe kuvuka bila ya kulipia.
ReplyDeleteHoja ya kupandisha ni ya msingi na hoja ya wananchi ya kufikiriwa ni ya msingi vilevile! Kinachotakiwa ni busara itumike katika kutafuta muafaka.
ReplyDeleteKinachonikera ni kuingiza siasa katika mambo ya msingi na shida za wananchi hasa huu unafiki wa wawakilishi wetu ambao kazi yao kubwa ni kuchumia tumbo!
Hawa wabunge hawana hoja ila wanataka kudandia shida za wananchi kujijenga kisiasa tu mbona suala la kuongezana posho wamenyamaza tu. hawana nia kabisa ya kuona wananchi wanaendelea zaidi ya kuangalia maslahi yao tu.
Geza ulole mamaa Gezaulole Maaeee...Magufulicjui kama anaujua wimbo na kisa hiki kama mwandishi alivyoeleza...hebu tafakari tena uamuzi wako..yaani guta 1800 jameni hebu vaeni viatu vya mwendesha guta ndo mjue cha kufanya..hii misfa itatumaliza sisi kinakapuku...sijaipenda hata kidogo hii ya kupandisha nauli ya kivuko cha SERIKALI kiasi hiki...Halafu Dr. Magufuli lugha yako chafu kabisa...hata kama walikuzomea..ungedhibiti hasira na jazaba zako kwani hawa watu wana shida bana..ah SIJAPENDA HATA KIDOGO..au ndo kama Dewji alivyosema...mnatafuta vyanzo vya kujilipa posho ya 200,000!
ReplyDeleteMwandishi anapiga siasa badala ya kusema nini kifanyike ili kila upande utoke ukiwa meno nje. Hajui anachofanya sasa ni uchochezi. Tanzania bila uandishi wenye jazba inawezekana.
ReplyDeleteHapa umejaa uchochezi tu toka habari hii iibuke naona waandishi wamejaza ushabiki na uchochezi. mimi nilidhani waandishi sasa wangeibuka na mawazo endelevu ya nini kifanyike kutatua hili na siyo kushupalia kupiga mbizi. hivi tujiulize tatizo hapa ni nauli ama ni kauli ya kupiga mbizi? na je Mheshimiwa Pombe Magufuli akiwaomba radhi wakazi wa kigamboni kwa ile kauli tatizo la nauli ndo limeisha! waandishi anzeni kujadili hoja ya msingi iliyopo mbele mfano ni vigezo gani vimetumika kupandisha nauli ya GUTA kutoka 200 mpaka 1800! wakati magari ya matajiri yakilipa 1300! uwapi usawa hapa? je hii ndo kumuondoa mtanzania kwenye umaskini? binafsi sina tatizo na kupandishwa nauli toka 100 kwenda 200 baada ya 100 kukaa hivyo kwa miaka 15 tatizo hapa ni namna walivyofikia kupandisha hiyo bei bila kushilikisha pande zote. walifanya hivyo mwaka juzi wakatupandishia nauli ya kivuko mpaka 200 na hiyo nauli ilidumu kwa siku mbili ikasitishwa baada ya kuona idadi ya watu wanaovuka imepungua kiasi cha pantoni kutembea na watu kichele. enyi waandishi acheni siasa njooni na mawazo mbadala na si kuendekeza siasa mambo mengi hayaendi hii nchi sababu ya siasa
ReplyDeletehivi huyu Maggid mbona naona watu wanamsema ila sioni uchambuzi wala point zozote za kusisimua kwenye makala zake?
ReplyDeleteEmbu tuwe wawazi..kweli Sh. 100 sasa hivi unaweza kununualia nini zaidi ya pipi? Hata maandazi hivi sasa yanaenda kwa Sh. 200! Tuache siasa uchwara na uandishi wa kishabiki, tuwe realistic na hali halisi ya maisha!
siasa bwana!! watupunguzie nauli na sisi wa mtwara iwe 200 kuja dar kuwaona ndugu zetu waliolazwa muhimbili kama wale wa kigamboni!?
ReplyDeleteSerikali imedhihirisha kuwa ni MFANYA BIASHARA NAMBA MOJA!
ReplyDeleteUkisikia UBEPARI NI UNYAMA ndio hapaaaa!
ReplyDeleteKAKA TUNAJUWA WEWE UMEOA KULE SWEDEN,KABLA YA DARAJA KUJENGWA LINALO UNGANISHA MJI WA MALMO NA COPENHAGEN(WAKATI WEWE BADO UKO TAMBAZA)KULIUWA DEBATE KALI JUU YA NAULI YA KIVUKO HICHO MARA KITAKAPO MALIZIKA(DARAJA)KIASI GANI KITOZWE IKAMULIWA NAULI ZITOZWE KUPITIA ROAD TOLL,WAKATI ULE KRONA NA SASA NI EURO KADRI YA MAISHA NA THAMANI YA PESA INAVYO PANDA NA NDIVYO ONGEZEKO LA NAULI LINAPO KUJA.MICHUZI WEWE UMESOMA KULE WALES UNAPO INGIA KUTOKA ENGLAND KWENYE KIVUKO MIAKA ILE GARI NDOGO ILIKUWA NI PAUND 2.35TWO YEARS AGO NIMEPITA PALE NI PAUND 5.75p LEO NASIKIA NI PAUND 6.00.MAENDELEO YA NCHI YANALETWA NA WANANCHI WENYEWE NA SIO KUPINGA KILA KITU,LABDA NJIA AU MATAMSHI ALIOTUMIA WAZIRI SIO SAHIHI NA TUMKOSOE KWA HILO,HAYO MAMBO YA GEZA ULOLE NA CHAKACHUA TUWACHIE AKIANA JUMA MRISHO NA CHIDUMULE MABO YA MAENDELEO YA NCHI LALIMA WANANCHI WACHANGIE NO MATTER WHAT.MAKALA HII INONYESHA NI KIASI GANI TANZANIA MTU YEYOTE AKIJIAMULIA ANAKUWA MUANDISHI WA HABARI.
ReplyDeleteMajjid hoja yako umeileta kisiasa na kiushabiki zaidi badala ya kiuchambuzi yakinifu. Tunatarajia nyie waandishi wakongwe mtusaidie kujenga hoja madhubuti ili wananchi wajue haki zao za msingi lakini pia kuisaidia au kuikosoa serikali ili kuhakikisha maslahi ya mwananchi yanazingatiwa. Na hata hivyo hali halisi nayo ipewe kipaumbele si kwa wakazi wa Dar tu hata na sie wa mikoani! Kama swala la nauli za kivuko kupanda, wasitetewe wa Dar tu, hata mikoani tunaotegemea vivuko tunakinywea kikombe cha ongezeko la nauli. Hivyo nakushauri leta hoja yakinifu ya nini kifanyike na sio kupokea kolasi za mipasho ya taarabu ya kina Mtemvu juujuu, itakushushia hadhi yako buree
ReplyDeleteMaggid is unfortunately as bankrupt as most of our ujamaa academics! The reliance on government is simply unrealistic if not imprudent! And this is the area those in the NGO entrepreneurship such as Maggid thrive upon. You cant go "I want, I want" all the time! It is unsustainable. We are going to be forced to actually look at how we reinvent ouraselves as a people most atune to ujamaa and decide that there ares ome services the government wont be able to provide. A contibutor here earlier inquired why ferry services are still being provided buy the government. In the villages we have locallities that are only connected by services provided by private individuals. Why shouldnt marine services be the same? The government will have to say we were no longer in that bussiness. That's where leadership is going to come to in. You cant be everything to everyone. Mr Magufuli is showing the way and he should not be vilified for but commended. The likes of Maggid are a great disservice to the reinvention of the attitudes of our people; shame unto them!
ReplyDeleteMwandishi huyu amejitahidi kutetea hoja zake hata pale ilipopingwa maana kaandika ya kuomba radhi, akaja ya Dewji na sasa hii, yote haya ni kutaka kushawishi kuungwa mkono , kama mie ningeishia ile ya kwanza baada ya kuandika kishabiki bila kuangalia ukweli, any way kuna waandishi na waandiki
ReplyDeleteWooi, cha! nimechoka na siasa mimi nasubiri feri ya kuanzia kunduchi bichi, au bagamoyo hadi posta. Magufuli hongera unakaribia kutenga siasa na taaluma.
ReplyDeleteWAANDISHI ACHENI UCHOCHEZI.