Watazamaji 14,150 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Februari 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 47,554,000.

Hata hivyo ni watazamaji saba tu waliokata tiketi za VIP A zilizokuwa zikiuzwa sh. 15,000. Viingilio vingine vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa na kiiingilio cha sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani kilichovutia watazamaji 12,853.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mechi hiyo namba 119 na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,254,000 kila timu ilipata sh. 8,583,000 wakati mgawo wa uwanja ulikuwa sh. 2,861,000.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,144,400, TFF sh. 2,861,000, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,430,500, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 286,100 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 2,861,000.

Gharama za awali za mechi ni nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna sh. 10,000, posho ya kujikimu kamishna sh. 40,000, posho ya kujikimu waamuzi sh. 120,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000. Gharama za tiketi sh. 4,000,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 990,500 wakati DRFA ilipata sh. 849,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ankal,,,

    Tafadhali turushie angalau chenga chenga ilivyojiri ktk Shughuli za Ubwabwa 'mpya' wa Maulidi ya Jirani (USHINDI WA ZAMBIA)...haya Makande yetu ya 'jana' (LIGI NA SOKA LA KIBONGO) vinatunyo ng'onyesha na kutuchosha vilivyo!

    ReplyDelete
  2. Michuzi bado tu mnashabikia Yanga na Simba huu mwaka 2012? Hizi timu hazina dili zaidi ya uchawi na ndiyo hawa wanaoua mpira wa bongo. Sasa watu wameshituka na ndiyo maana hawaendi uwanjani kuangalia porojo. Si unaona mwenyewe?

    ReplyDelete
  3. Hivi DRFA na FDF NA BMT hupokea hel;a hizi kwa sababu gani? Kuna miradi fani ya kimsingi ya maendeleo ya soka hapo Dar es Salaam na Tanzania? Zaidi ya pesa hizi kwenda kulipa maofisa wa vyama hivi ambao hawana kazi yeyote ya kimsingi inayoonekana kwetu wadau wa soka? Michuzi wakilisha usifiche maoni na tunaomba majibu kutoka DRFA, FDF na BMT.

    ReplyDelete
  4. Vyama na Taasisi za Michezo Tanzania zipo kwa ajili ya kula fedha za bure,,,pamoja na Bunge na Wanasiasa!

    Ndio maana wasaka Utajiri wa haraka haraka huhangaikana Sekta zingine wakiona dira hazisomi huingia katika ,DINI,SIASA NA MICHEZO!

    HUKU NDIO KUNA FEDHA ZA BURE NA HAKUNA UKAGUZI WA WAHASIBU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...