Makamu wa Rais wa Kampuni ya African Barrick Gold (ABG) anayeshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Makamu wa Rais wa Kampuni ya African Barrick Gold (ABG) anayeshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, akitoa cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) walionufaika na mchango wa kampuni hiyo wa kusomesha wanafunzi kwenye sekta ya madini.
KAMPUNI ya uchimbaji dhahabu ya African Barrick Gold (ABG) imeingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yatakayoiwezesha kampuni hiyo kufadhili elimu ya wanafunzi wanaosomea kozi ya madini chuoni hapo ili taifa liweze kupata wataalamu wa kutosha kwenye sekta ya madini.
Mkataba huo wa kufadhili elimu ulitangazwa kwenye chuo cha UDSM Jumatatu wiki hii kati ya Makamu wa Rais wa ABG anayeshughulikia mahusiano ya kampuni hiyo, Deo Mwanyika, na Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM, Prof. Rwekaza Mukandala.
Katika makubaliano hayo, kampuni ya ABG itafadhili masomo ya wanafunzi 12 ambao wamekuwa wakiongoza kwa kuwa na matokeo bora zaidi darasani.
Kampuni hiyo pia imetoa zawadi kwa wanafunzi bora wa mwaka 2011/12.
Tangu program hiyo ya ABG ya kugharamia elimu ya juu ianze mwaka 2009,zaidi ya wanafunzi 70 wamenufaika.
Mwanyika alisema kuwa kampuni ya ABG itaendelea kuwekeza kwenye elimu nchini ili kuhakikisha kuwa wataalamu wengi zaidi wa madini wanazalishwa katika chuo hicho cha UDSM na vyuo vingine nchini.
Ufadhili huo wa Barrick utaifanya Tanzania iwe na wataalamu wengi zaidi wa sekta ya madini badala ya kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi.
Mwanyika alisisitiza kuwa lengo la ABG ni kuhakikisha kuwa Tanzania inajikomboa kwa kuwa na wataalamu wake wenyewe wa sekta hii muhimu ya madini.
“Tunataka ifike wakati wataalamu wa madini kati ya 200 na 300 tuliowaajiri katika kampuni yetu kutoka nje ya Tanzania wanawaachia wataalamu Watanzania nafasi zao," alisema.
"Hii ndio maana tunachangia ada, vifaa na matumizi mengine, ikiwa ni pamoja na kuwaajiri wanaohitimu, kutoa nafasi za mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi walio katika hitaji hilo na michango mingine.”
Aliongeza kuwa mchango wa chuo hicho katika kitivo cha uhandisi wa madini umeonekana na kuitia moyo Barrick kuendelea kuchangia elimu hiyo.
“Tumetoa mchango wetu katika elimu hii kwa mara ya nne mfululizo na tunaahidi kuongeza nguvu zaidi ili tutimize malengo yetu ya kuiletea nchi wataalamu bora wa kutosha katika sekta ya madini kupitia Udsm.
Tumeona mwanga huo kwa wahandisi wa madini wa Tanzania tuliowaajiri,wanaweza,” Mwanyika alisema na kuahidi kutoa ajira ya miezi 36 kwa wanafunzi hao waliopata ufadhili wa ada, pindi watakapomaliza masomo.
Naye Prof. Mukandala aliishukuru kampuni hiyo na kusema kuwa imekuwa kichocheo cha mafanikio katika kitivo hicho kutokana na michango ya vifaa,tuzo mbalimbali kwa wanaofanya vizuri zaidi, pamoja na nafasi za mafunzo ya vitendo kwa wanaoyastahili.
“Tutashirikiana na Barrick kuhakikisha katika miaka 50 ijayo Tanzania inakuwa na wataalamu wake wa madini wenye ubora unaohitajika ili yaliyopo;kama vile mafuta na gesi yachimbwe na wazawa wenyewe…”.
“Nafasi za mafunzo ya vitendo katika kampuni hizo zimeweza kuwaongezea uwezo hata maofisa wa chuo wanaohusika na kitivo hicho hivyo ni jambo la kufurahiwa na kupongezwa. Hatutegemei kuona waliopata ufadhili huu wanapoteza muda wa kujifunza kuandamana kwenda bodi ya mikopo kudai ada,fedha za kujikimu na nyinginezo kwa sababu mmewalipia”.
Mwanyika pia aliwataka wanafunzi hao 12 wa UDSM waliopata ufadhili wa ABG pamoja na wanafunzi wengine wote wa alimu ya juu nchini kujitolea ili kuleta maendeleo ya kasi zaidi nchini.
Alitumia maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,kuwaasa wasomi nchini kutolisaliti taifa na kutumia elimu na ujuzi wao kwa manufaa mapana ya taifa.
barrick ni muajiri mzuri tatizo lao ni kufukuza wafanyikazi wake kila kukicha na nadhani ndio wanaongoza kwa kesi nyingi mahakama ya kazi
ReplyDeleteBarrick wanajitahidi sana licha ya mapungufu machache.
ReplyDeleteKatika kitu ambacho jamaa nimewakubali Barrick zaidi ya huu Udhamini wa Masomo kwa watakaosoma sekta ya Madini, Jamaa mwaka juzi 2010 walitoa IPO (Initial Public Offering) yaani Toleo la Awali la Hisa hadharani hii ilikuwa ni nafasi kubwa sana kwa Wawekezaji na Wakuza TIJA nchini kuichangamkia kwa kukuza Mitaji yao kwa njia ya Hisa ktk DSE (Soko la Hisa la Dar),,,
Isipokuwa cha kusikitisha Wabongo tupo na utafutaji pesa wa kizamaani wa kwenda China kununua bidhaa feki,Dubai na Kufanya shughuli za Mipango mipango ili kupata pesa, badala ya mipango halali ya Hisa kama hii.
Matokeo yake mwitikio ulikuwa wa chini sana nchini kwa watu kuwekeza na ikapelekea jamaa Barrick wakahamishia biashara(Cross Listing) huko LSE (London Stock Exchange-UK ) huko Ushuani kwa Wajanja wenye kuijua pesa.
Nakubaliana na mdau wa kwanza,Maana ukifukuzwa Bulyanhulu,huwezi kupata kazi Buzwagi,Tulawaka wala North Mara.Deo mliangalie hili linawaharibia jina zuri.Inabana ajira.Mimi Barrick nimewafanyia kazi miaka 7 kwa kweli ni mwajiri mzuri na nilifurahia maisha.
ReplyDelete