HALIMA M. MCHUKA (18 Mar.1967- 29 Dec. 2011)

Familia ya Mchuka wa Dar es Salaam, pamoja na ndugu wote walioko Miono na Kibindu-Bagamoyo, wanatoa shukrani za dhati kwa  wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kipindi kigumu cha msiba wa mpendwa wao, Halima Mohamed Mchuka uliotokea tarehe 29/12/2011 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa tarehe 30/12/2011 katika makaburi ya Msasani Dar es Salaam.

Shukrani za pekee ziwaendee, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt.Emanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Mhe. Sofia Simba, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt. Fenella Mukangara, Waheshimiwa wabunge wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, IGP, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,   Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mstahiki Meya wa Ilala.

Shukrani nyingine ziwaendee viongozi na wafanyakazi wa TBC wakiongozwa na M/Kiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana, wafanyakazi wastaafu wa RTD, wafanyakazi wa kampuni ya Ndege Tanzania, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Dar Group na Muhimbili, viongozi wa vyama vya michezo, waandishi wa habari na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari, Uongozi wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, BAMITA, majirani wa Karakata, Msasani, Mabibo na Mbezi, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia ya MCHUKA wa ndani na nje ya nchi. Tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa kutufariji kufuatia kifo cha HALIMA MCHUKA.

Arobaini ya Marehemu itafanyika  Miono Bagamoyo siku ya Ijumaa Tarehe 3/02/2012  kuanzia saa 11:00 jioni na Hitma itasomwa Jumamosi ya Tarehe 04/02/2012  saa 3 :00 asubuhi.Nyote mnakaribishwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na wanafamilia moja kwa moja au kupitia simu namba 0713477790 au 0784737253.Karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...