KAMPUNI ya uchimbaji wa dhahabu ya African Barrick Gold (ABG) imeahidi kuendelea kuwekeza zaidi kwenye elimu nchini Tanzania ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Barrick, ambayo ina migodi minne ya dhahabu nchini -- Bulyanhulu, North Mara, Buzwagi na Tulawaka - imeshawekeza mabilioni ya shilingi mpaka sasa kwenye maeneo mbalimbali ya sekta ya elimu.
"Tunaamini kuwa elimu na ukuaji wa uchumi ni vitu ambavyo vinaenda sambamba na ABG imekuwa ikifanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kusaidia vipaumbele na programu zao," Barrick ilisema kwenye taarifa katika tovuti yake.
"Tunasaidia kuendeleza miundombinu ya shule, kutoa scholarships ili kuchochea wanafunzi wengi wawe wanaenda shule. Pia tunawawezesha wafanyakazi kwenye migodi yetu kusaidia kukuza elimu kwenye shule zinazozunguka migodi hiyo."
Ripoti mpya ya Benki ya Dunia iliyotolewa Jumatano wiki hii imesisitiza umuhimu wa serikali kuendelea kutoa kipaumbele kwa elimu ili kuleta maendeleo nchini.
Sekta ya elimu imekuwa ikiongoza kupewa rasilimali na serikali, huku ikipata mpaka asilimia 20 ya bajeti ya serikali kila mwaka.
Kwa upande wake, ABG imekuwa ikiwekeza kwenye elimu nchini ili kuhakikisha kuwa Watanzania wengi zaidi, ikiwemo wale wa vijijini, wanapata huduma hiyo muhimu.
Kampuni hiyo imeingia mikataba na vyuo vikuu mbali mbali nchini, ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Sokoine na vyuo vya VETA ili kufadhili sekta ya elimu.
ABG imekuwa ikiwekeza kwenye elimu ili kupata idadi kubwa zaidi ya Watanzania wenye elimu ya juu na ufundi wa kitaalamu kwenye kuendeleza sekta ya madini.
Mpaka hivi sasa ABG imewekeza kiasi cha dola za Marekani milioni 1.5 (takriban shilingi 2.4 bilioni) kuendeleza elimu na taaluma kwenye sekta ya madini nchini.
Kampuni hiyo pia imekuwa ikiwekeza kwenye elimu na mafunzo ya wafanyakazi wake wenyewe, huku ikitumia bajeti ya dola za Marekani milioni 4 kwa kazi hiyo.
ABG imeajiri moja kwa moja zaidi ya watu 4,000, huku zaidi ya watu wengine 5,000 wakiwa wameajiriwa na wakandarasi mbalimbali wa kampuni hiyo.
nawasifu kwa kusomesha tatizo wanasomesha watoto wachache kwenye shule ya mamilioni ya shilingi.
ReplyDeletemfano
walisomesha watoto 2 ISM Moshi ambapo ada ni kati ya 8ml hadi 18ml kulingana na darasa/kidato. Hao watoto wamepata scholarship kwenda nje ya nchi. Na walijua walivyo vichwa nina hakika watazuiwa huko huko hatutawaona tena.
Ni wazo zuri kusomesha shule za kisasa lakini tuangalie suala la kusomesha shule za gharama ya 2.5ml hadi 5ml ili tupate wasomi wengi wanaofaidika na Barrick
Good support the ABG you are devoting to the education sector within the country,that is great concern of the community's life role you are playing.Keep it up!
ReplyDeleteI believe that the community whose young boys and girls are supported by ABG for further education,do appreciate this enduring help from the corporate,however if not critically noted based on both short and long run achievements,the communitys' members can think that the ABG has not played its role thus giving no support to the corporate's prosperity.
Ni vizuri,lakini mkumbuke na mnavyovuna hizo ounces kutoka kwenye ardhi yetu.Bulyanhulu kwa mfano,ni mgodi wa chini ya ardhi lakini grade(daraja?) lake liko juu-high grade orebody(nashindwa hata kiswahili chake)..Kwa hiyo mnapata faida kubwa..Uwongo Mwanyika?Kisiasa mtasema gharama za uzalishaji zipo juu.
ReplyDeleteDavid V
Barrik Gold tunatambua mchango wenu, lakini bado mnatunyonya kuliko mnavyowekeza. Juzi tu hapa waziri alilalamika mnatumia utaalamu wenu kuficha baadhi ya mapato kwa kutake advantage ya shortage ya wataalam kwny nchi maskini kama Tanzania. Bado hatudanganyiki kwa publication zenu, because we know u can do more than that knowing that Tanzania is poor country.
ReplyDelete