Na Mashaka Mhando,Korogwe
VILIO, majonzi na huzuni vilitawala leo asubuhi katika shule ya sekondari ya Wasichana Korogwe, kufuatia wanafunzi wapatao saba na mpiga picha mmoja wa kujitegemea, kujeruhiwa vibaya kwa kugongwa na gari lililokuwa likichezewa na mmoja ya wahitimu wa kidato cha sita aliyeweka gia ya kurudi nyuma na kisha gari hilo, kuwagonga wahitimu hao.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa 4:20 asubuhi katika shule hilo, baada ya mwanafunzi mmoja Kibibi Mmasa anayesoma kidato cha sita shuleni hapo, kuingia katika gari la kaka yake lenye namba za usajili T489 AGJ ambaye alifika kushuhudia mahafali hayo, aliweka gia hiyo kisha gari hilo kurudi nyuma kwa mwendo kasi na kuwaparamia wahitimu hao waliokuwa wamejikusanya vikundi.
Wanafunzi waliojeruhiwa na hali zao kuelezwa zipo katika hali mbaya ni Zahra Jumanne (19) na mpiga picha wa siku nyingi Bw. Elias Ngole 'Ngoswe', wengine ni Renata Renatus (25), Sophia Godfrey (19), Victoria Mtwale (19), Nancy James (19) na Mwanamkonda Kapunda (19) ambao wote wanasoma kidato cha sita na ambao walikuwa wakitarajia kufanya mahafali ya kumaliza shule.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia gari hilo likiendeshwa na mwanafunzi huyo likitembea kwa kasi kurudi nyuma na kuanza kumgonga mpiga picha huyo ambaye alikuwa akizungumza na Mwandishi wa ITV na Redi One Bw. William Mngazija ambaye baada ya kuliona gari hilo aliruka pembeni lakini mwenzake alishindwa na badala yake gari hilo lilimgonga kisha kunasa chini yake na kuburuzwa hadi kiasi cha mita 30 gari hilo lililopogonga mti na kusimama.
Baada ya kugongwa mpiga picha huyo liligonga wanafunzi wengine ambao walikuwa wamejikusanya wakibadilishana mawazo namna watakavyosherehekea mahafali yao ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa benki ya posta nchini Bw. Sabasaba Moshingi ambapo mmoja Zahra aligongwa vibaya na kunasa chini ya gari hilo ambapo gari hilo lilipinduliwa ili kumnasua huko chini akiwa amevunjika miguu na kupata jeraha kubwa kichwani.
"Kaka alinituma mle ndani ya gari wakati nikichukua mzigo aliyonituma ghafla nikaona gari linakwenda, nikawa sijui kinachoendelea nikasikia makelele wenzangu wanapiga huko nje huku nikiwa nimekanyaga mafuta," alisema Kibibi huku akisihi viongozi wamweche kaka yake ambaye alishikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo. Kaka yake ni Hussein Mmasa.
Akizungumzia tukio hilo, Bw. Mngazija alisema kama si kupata ujasiri kuwa kusogea kulipisha gari hilo pengine naye angekuwa miongoni mwa watu waliojeruhiwa lakini ana mshukuru mungu kukwepa ajali hiyo.
"Nilikuwa nasalimiana na Ngoswe hatujaonana muda mrefu, sasa ghafla nikaliona gari linakuja kwa kasi nikaruka na kumuacha mwenzangu ambaye alisogea kwa nyuma badala ya kulikwepa matokeo yake likamgonga," alisema Bw. Mngazija na kuongeza kwamba alikwepa gari hilo likiwa limemfikia hatua mbili tu na kama siyo kuitwa kuelezwa gari kuja uswa wao, lingemgonga.
Mkuu wa wilaya ambaye alifika kwenye eneo hilo na baadaye kwenda hospitali kushughulikia tiba ya wanafunzi hao, alisema tukio hilo ni la kusikitisha na alishawahi kutoa taadhali kuhusu magari yanayokwenda kwenye sherehe kama hizo shuleni kwamba magari yaegeshwe kwenye maeneo maalum kuliko kuwekwa katika maeneo kama hayo ambayo yanaweza kutokea ajali kama hizo.
Wanafunzi hao, wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani hapa wakiendelea kupatiwa matibabu huku mmoja wao Zahra akiwekewa mtambo wa kumuongezea kupumua Oksijeni na wengine hali zao zinaendelea vizuri. Mahafali yaliendelea lakini hayakuwa na furaha kutokana na tukio hilo.
Mapicha yanafuata muda si mrefu ujao. Stay tuned!!

Ikiwa alitumwa kuchukua chochote kwenye gari mambo ya kukanyaga mafuta yanatoka wapi? Inaelekea alidhamiria kabisa. Wote wakamatwe na waeleze huo upuuzi wao wa kutaka damu za binadamu wenzao. Ukimtazama huyu Kibibi wala hana wasiwasi. anamtetea nini kaka yake awekwe rumande mpaka kieleweke, sisi tusomeshe watoto wetu kwa shida halafu yeye asisome aje kutibua mambo ili wenzake wasiweze kufanya mitihani.
ReplyDeletePoleni wanafunzi na wanafamilia wote mliokumbwa na ajali hiyo. Mungu awaponye haraka majeruhi wote.
ReplyDeletePoleni sana ndugu zetu kwa waliyowakuta.Mungu awajalie majeruhi wapone haraka ili waendelee na masomo yao,ingawa kwa kiasi fulani itawaathiri kwani wanatarajia kufanya mitihani yao.??Ila kauli ya huyo aliyewagonga wenzake ni ya kijinga inawezekana hakutumwa na kaka yake kuchukua mzigo labda alilewa sifa akajifanya dereva ahojiwe vizuri huyo
ReplyDeletePoleni sana wathirika na ndugu zenu na waalimu wao kwa ujumlaHakuna aliyekusudia,naomba wote tuchukulie ni ajali tu ni bahati mbaya.
ReplyDeleteNa mara nyingi kwenye furaha majanga hutokea.Ni kuchukua tahadhali ingawa ajali haina kinga,lakini tahadhali yasaidia.
Mwanafunzi huyu na kaka yake hawakukusudia watu wagongwe.Wote wapewe pole.
Poleni sana wadau wa janga hili kule Korogwe na popote pale walipo. Hiyo ni ajali kama ajali nyingi hapa duniani. Napenda tu kuueleza umma kuwa hakuna duniani gari linaloweza kurudi kinyumenyume kwa mwendo kasi wa km 120 kwa saa.
ReplyDeleteHeeeeeeee... Saa kumi na nusu asubuhi!!!! Siamini kuwa hata Kiswahili nacho kimetushinda sasa! Tumekuwa taifa ambalo haliwezi kuongea lugha yoyote kwa ufasaha!
ReplyDeletePoleni wote mliofikwa na ajali hii. Mungu wajalie muendelee vizuri na kupona kabisa.
Hiki nini, ndo maana tunasema,watu wasiwe na furaha kupita kiasi, binti huyu hana drivers license, hajui kuendesha anakaa kwenye kiti cha dereva anafanya nini?na nani anamruhusu kufanya hivyo.huu ni uzembe usio vumilika, weka mahabusu huyo kakake maramoja, ingawa tunajua haitasaidia.
ReplyDeleteMajira ya saa 4:20 asubuhi au saa 10:20 jioni? Ktk Kiswahili hakuna saa 10:20 asubuhi. Kuna saa 10:20 usiku au jioni. Kama ni saa 10:20 usiku basi likuwa mahafali ya wanga. Kiswahili nacho kigumu.
ReplyDeleteeeeh mungu....
ReplyDeletemimi nahisi gari haikuwa kwenye handbreak
ReplyDeleteso Kibibi aliitoa kwenye gia na gari ikaanza kurudi.
simple kama ilikuwa kwenye gia then
no handbreak na ikawekwa kwenye gia ya reverse ndo maana ikarudi.
ingekuwa kwenye gia ya kwenda mbele labda yasingetokea yaliyotokea.
anaweza kuwa alipoingia garini labda alipanda na kiti alisukuma gia na mwili wake bila kujijua esp kama alitaka kuchukua kitu
poleni mlioumia
Poleni wahanga. Ni ajali jamani, inaweza kumtokea mtu yeyote.
ReplyDeleteyaani its so sad, Mungu awajalie afueni ya haraka majeruhi wote.
ReplyDeleteKiukweli suala limenigusa na kunisikitisha sana, haswa nikiona mhusika hana hata wasiwasi, yuko bize anamuombea kakake asiwekwe ndani.....au alikusudia?
Yote hiyo ni misifa na swagger kuwa kwao wana gari na anajua kuendesha ndo akaamua kuonesha kuwa anajua wakati hajui.
Mimi sielewi, kama alitumwa kufuata kitu katika gari, imekuwaje gari litembee? Manake ni kuwa alichomeka switch akawasha gari na kukanyaga accelerator.......... she is so stupid. Amewaharibia wenzie maisha yao.
Aah naongea kwa hasira tu lakini Mungu atusamehe maana tunamhukumu, yawezekana ni bahati mbaya tu, Mungu ndo anajua.......... aaaah
Ipy
Saa 10.20 asubuhi?
ReplyDeleteAlitumwa kuchukuwa mizigo au kuwasha gari?
Gari haliwezi kuwa limezimwa ukakanyaga mafuta likaenda spidi hiyo,kwanza haliwezi kuondoka litabaki linaunguruma.
Huyo binti alitaka awaonyenyeshe wenzake kuwa anajuwa kuendesha gari,ndio hayo yakamkuta
Sheria inasemaje hapo?
Kaka yake hana makosa anashikiriwa na polisi kimakosa kwani hakuwa anaendesha yeye wakati ajali inatokea.
Binti ndo ana makosa ya kuendesha gari bila leseni(sidhani kama anayo) na kusabaisha ajali na kujeruhi watu
Polisi jipangeni vizuri
Gari inarudi nyuma kwa mwendokasi wa Km120/saa, mmmh itabidi tuwaulize vizuri hawa wahandisi wa Toyota. sidhani kama kweli.
ReplyDeletehapo wadau hakuna bahati mbaya kunajamaa mmoja aliumia mpaka kukatwa mguu kisa jamaa alikuwa na pikipiki yake akaja akasimama baada ya kusimama jamaa aliye umia akachukua ile pikipiki bila kumweleza basi, akaiwasha moto akapanda akaanza kuendesha basi bwana kumbe ilepikipiki inamatatizo kwenye exceleleta yake akivuta mafuta inakwenda kuna sehemu inanasa kwavile yeye anaijuli anaistua inakuwa safi sasahuyu aliyeumia akawa hajui kitu kama hicho basi bwana kila akivuta mafuta moto huo ikamchachia mwishowe akaenda kupalamia ukuta augonga huo mguu hapohapo mpaka leo tunamwita kigulu,utakuta mtu mwingine anafika nyumbani kwako haulizi anachukua remot ya tv anawasha bila kuuliza matokeo yake inaungua inabaki samahani bahati mbaya hakuna bahati mbaya kuna uzembe
ReplyDeletePoleni sana wahanga.............nilishituka sana nilipo sikia cause toka nisome Korogwe hakujatokea maafa kama hayo tena kwenye Graduu. All in all,mungu ndo anajua ukweli ni upi.cha muhimu tuwaombee walio hosptali hasa huyo anayetumia mashine ya kupumulia. and that girl aache ujinga wa kumtetea kaka yake while karibia atoe roho za wa2 and kuwatia vilema wenzie. Mungu atusaidie.
ReplyDeleteUjana bwana plus utandawazi kweli una mambo yake! Pole binti na asante kwa kutupa fundisho kwa wale tunaowapenda watoto wetu kwa sana.
ReplyDeleteInauma sana, poleni wote mliofikwa, MUNGU awajalie afya njema. AMEN.
ReplyDeleteEE MWENYEZI MENGU WAJALIE UPONAJI WA HARAKA ILI WATOTO HAWA WAWEZE KUFANYA MITIHANI YAO,WEWE NDIYE MUWEZA WA YOTE KWAKO HAKUNA LINALOSHINDIKANA.
ReplyDeleteNDUGU ZANGU MBONA MIMI KAMA SIMUELEWI HUYU BINTI ALIYESABABISHA HII AJALI!! MAANA HAONYESHI KAMA ANAJUTIA KITENDO ALICHOKIFANYA!!
MUNGU TUSAIDIE.