Bunge la Tanzania litakuwa mwenyeji wa Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa). Mkutano huo utakaofanyika Mjini Arusha, kesho tarehe 24 Februari, 2012, ambapo kamati hiyo ya CPA Africa, inakutana nchini kujadili maswala mbalimbali ya chama hicho kwa kanda ya Afrika. Bunge la Tanzania ndio makao makuu ya chama hicho kwa kanda ya Afrika.

Kamati hiyo itahudhuriwa na wajumbe wa kamati tendaji ambao ni:

Mhe. Rose Mukantabana (Mb) Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika na pia ambaye ni Spika wa Bunge la Rwanda

Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji wa Chama hicho ambaye pia ni Spika wa Bunge la Afrika Kusini

Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) Makamu wa Rais wa CPA Afrika na pia ndiye Spika wa Jimbo la Gauteng, nchini Afrika Kusini

Mhe. Request Mutanga (Mb) Muweka Hazina wa CPA Afrika, na Mbunge kutoka Bunge Zambia

Mhe. Job Ndugai (Mb) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, ambaye pia ndiye mwenyeji wa kamati hiyo hapa nchini,

Na Dr. Thomas Kashililah, Katibu wa Kanda wa chama hicho ambae pia ni katibu wa Bunge la Tanzania

Tanzania imekuwa makao makuu ya Kanda ya CPA Afrika tangu mwaka 2004, ambapo shughuli zote za chama hicho huratibiwa na sekretariat ya CPA ambayo ipo nchini Tanzania.

Imetolewa na Ofisi ya Bunge
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
24, Februari, 2012
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. 100% confidence levelFebruary 24, 2012

    Hongera sana wajumbe wa CPA kutoka Bunge la Tanzania kwa kuonesha heshima,utendaji na ushirikiano kwa wajumbe wa CPA toka mataifa mengine.Kimsingi huu ni mfano wa kuigwa na taasisi,idara,wakala,na wizara mbalimbali ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata global sustainable opportunities kama hizi kwani siyo tu zina lipa Taifa letu sifa bali pia kunufaika na sustained developmental strategic plans and policies for both national and international communities katika nyanja za kiuchumi,kisiasa,kijamii,kimazingira na kiteknolojia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...