Bw. Nehemia Mchechu, Mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya marehemu mama Ester Nyimbo Badi mama mzazi wa  Bi. Blandina Nyoni, akizungumza katika ibada maalum ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika leo kwenye kanisa kilutheri la Azani Front jijini Dar es salaam leo.Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa na utazikwa katika kijiji cha Ilembula huko Njombe.
 Ibada ya kuombea mwili wa marehemu leo.
Bi. Blandina Nyoni Mtoto wa Marehemu mama Esther Badi akitoa historia ya marehemu wakati wa ibada hiyo leo.
Waombolezaji mbalimbali wakiwa mkatika ibada hiyo.
Ndugu na jamaa wakiwa katika ibada hiyo leo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hadji Mponda kulia akiwa pamoja na Paniel Lyimo katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu wamehudhuria ibada hiyo pia.
Mwili wa marehemu ukiandaliwa tayari kwa waombolezaji kuanza kutoa heshima zao za mwisho.
Waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza la mwili wa marehemu Mama Esther Badi.
Waombolezaji wakielekea kutoa heshima zao za mwisho.
Picha na John Bukuku wa Full Shangwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Pole sana Mama Blandina Mungu akutie nguvu

    ReplyDelete
  2. RIP mama Esther Badi, tutakukumbuka daima,poleni sana wana familia.

    ReplyDelete
  3. poleni sana wanafamilia kwa msiba huu mzito

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...