Rais wa Chama cha Soka Cha Zambia Kalusha Bwalya (suti nyeusi) akiwaongoza wachezaji wa timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' kuelekea mahali ambapo siku ya Jumanne jioni ya Aprili 27, 1993 ndege ya jeshi la nchi hiyo aina ya Buffalo DHC-5D iliyokuwa na wachezaji wa timu ya Taifa enzi hizo ikijulikana kama 'KK 11' ikielekea Dakar, Senegal, kucheza mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia ilishika moto na kuanguka katika bahari ya atlantic kiasi cha mita 500 hivi toka katika ufukwe wa jiji la Liberaville,  Gabon, nchi ambayo   usiku huu wameitoa Ivory Coast kwa penati 8-7 katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika na kutwaa ubingwa huo na kuwaenzi wenzao waliopotea miaka 19 iliyopita kwa namna ya kipekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Nadhani inabidi tuwapeleke wachezaji wa taifa stars nchini Zambia wakajifunze maana ya uzalendo na kupigania taifa lao- Great performance from Zambia well deserving championship

    ReplyDelete
  2. tanzania tumepata somo zuri kuwa penye nia pana njia hebu nasi tuamue kufanya kweli

    ReplyDelete
  3. Hongera Zambia mmetufariji sana.leo swala zangu zote niliwapa Zambia.Zambia wana kocha wa maana sisi tumeibiwa na Maximo na sasa huyu Mzee wa Kidenishi naye ni Magumashi kama Maximo.

    Mdau Jongo wa Kisiju-Mtalaam wa soka.

    ReplyDelete
  4. Sio swala wa wachezaji wa tanzania kutokuwa wazelendo..Tatizo la Tanzania ni mizengwe mingi..waTanzania tunaimba sanaa..songi songi nyingi lakini vitendo butu...Vipaji Tanzania tunavyo vingi sana..Tatizo uaandaaji na mipangilio/ mipango..planning inatuangusha sana sisi watanzania..wanaopewa dhamana ya kuziandaa timu zetu kwenye mashindano ya kimataifa wanakuwa walafi na mijizi mikubwa ya kutafuna fedha za kutengeneza timu imara....Tuache wizi, tuache udokozi, tuwalipe wachezaji wetu haki zao kama wajibu unavyotamka. Ongera Zambia !!

    ReplyDelete
  5. sisi tutabaki tu, na mambo ya bonanza,ambayo yanauwa uzalendo wa nchi.kwa hiyo tuangalie sana haya mabonanza na matamasha ya makampuni na watu binafsi yanauwa uzalendo wa vijana walio na vipaji vya kutetea taifa lao.

    ReplyDelete
  6. Hongera Zambia mmetufuta kimasomaso
    TFF wanatakiwa kujifunza kwa Jirani zetu tuwekeze katika soka kwani inaweza ikawapa ajira Wachezaji wetu

    ReplyDelete
  7. Well done KALUSHA BWALYA and CHIPOLOPOLO!

    ReplyDelete
  8. Taifa Stars:

    Ni wazuri kwa Kulewa Sifa,Ubinafsi,Umwinyi,Uvivu,Kubweteka,Ngono,Bangi na Ulevi!

    Huku Uzalendo Uchungu za nchi licha ya kubeba jina (TAIFA STARS) linaloashiria MUAMKO WA UZALENDO!

    ReplyDelete
  9. Uzalendo lazima uanzie kwa viongozi, huwezi kutegemea wachezaji wafanye uzalendo wakati viongozi wanasimamia ufisadi

    ReplyDelete
  10. Sikubaliani na mdau wa kwanza kamwe. Sikia, TZ sisi mpaka leo bado tuna imani kuwa wachezaji wazuri wanatoka Simba na Yanga jambo ambalo si kweli. Kwa kifupi, wachezaji wa hizi timu mbili ni wachawi mno na si wachezaji kweli pia hawafubdishiki kutokana na kutokuwa na vipaji. Niambieni katika hizi timu wana wachezaji wangapi wanafaa kuitwa wa kimataifa ambao ni wazalendo? Yes, jibu ni hapana na ndiyo maana rais Mwinyi alikuwa anawaita vichwa vya mwendawazimu because he saw it. We uneona wapi kila kukicha mnafundishwa kile kile lakini kichwani hakiingii. Acheni uchawi tafuteni talent ya ukweli toka mijini na vijijini, alaaaah!

    ReplyDelete
  11. Nyie mashabiki wa kibongo ni wapuuzi, tatizo hapa si makocha bali ni kanuni za kina Tenga kuwaweka ama kumrithisha kocha wachezaji wachawi na ndiyo maana hawafundishiki. We angalia mpaka sasa wabongo wengi wanaamini Ngassa ni bonge la mchezaji wakati si kweli, dogo hana mpira wowote zaidi ya spidi ila ukimwambia mbongo hivi anakutukana wakati unasema ukweli. Bongo bado sana kimpira inatubidi tufute kasumba ya uchawi waliyonayo wabunge na mawaziri wetu ndo tutafikia ila hivi hivi, sijuwiiiiii!

    ReplyDelete
  12. Eti TFF ijifunze kwa majirani zetu, Tenga ataiba hela na nani?

    ReplyDelete
  13. huy kochi wa Zambia aliomba kuja TZ kabla hajaenda Zambia

    TFF wakasema eti hatufai ona sasa hata muda haujapita kachukua kombe

    haya mmelala jana usiku????

    well done Zambia na Coach

    ReplyDelete
  14. safi sana zambia

    ReplyDelete
  15. Nyie TFF acheni kudokoa hela za wachezaji,acheni ufisadi.Kwenye hao wailofariki kwenye ajali hii nawamkumbuka sana Numba Mwila na Kelvin Mutale(R.I.P),wakati wanaenda kucheza mechi hii na senegal walikuwa wametoka kucheza na Mauritius na kuwachapa 3-0 jijini Port Louis magoli yote 3 yakifungwa na Kelvin Mutale(nilikuwa na miaka 23 JKT Ruvu Operation Vyama Vingi,Kombania A)

    David V

    ReplyDelete
  16. Chipolopolo ya Kalusha Bwalya BIG UP, TFF nendeni mkachukue somo, na sisi wa TZ tunataka mambo kama hayo.

    ReplyDelete
  17. Kocha wao anabidi hadi kumbeba mchezaji wake aliyeoumia ali asherehekee na wenziwe!!

    ReplyDelete
  18. BLAA BLAA BLAA BLAA BLAA BLAA TUNAMPIGIA MBUZI GITAA

    BONGO MPIRA SIO MAMBO YETU TUSIJILAZIMISHE

    BONGO MAMBO YETU NI MUZIKI KWA KWENDA MBELE

    TUPIGE MUZIKI

    TUJAZE MADISCO..TUONGEZE MAUZO YA POMBE TUENDELEZE NGONO ILI GONJWA HATARI LA UKIMWI LIWE NDIO USHINDI WA TAIFA.....FULLSTOP.

    ReplyDelete
  19. Watanzania hatuna uvumilivu tunataka mafanikio haraka sana, nakumbuka huyu kocha kakaa na hii timu mda mrefu sana si chni ya miaka mitano leo ndo wanapata mafanikio unayoyaona.Swala la pili tunatatizo la kutojua position yetu na kuanza kujiringanisha na vitu ambavyo havipo, mfano kuilinganisha Tanzania na Zambia kwenye soka ni kosa sana, kwa hiyo inabidi kocha wa timu ya taifa aanze kujenga foundation at least three years, then another three years tuanze kushindana kwenda AFCON then baada ya miaka miwili tupate hiyo nafasi baada ya miaka mitatu mingine tuweze kutoa ushindani wa kweli kwa hiyo upesi si chini ya ten years.Alikuwepo Maximo alikuwa ameanza kuonyesha njia tukaanza majungu yetu ya kipwani tumerudi kulekule kwenye matakataka yetu,watu walipiga kelele ooh Kaseja sijui Boban tuko wapi sasa na kaseja wetu hata CHAN hakuna, majungu na waandishi habari njaa ndo wanaharibu hii nchi kwenye kila kitu na tunakoenda ndo pabaya kabisa

    ReplyDelete
  20. tanzania hakunaga timu ni hayo tu, hakuna cha simba wala fisi, wanangurumaga wakiwa ndani tu nje mkia fyatu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndiyo dalili ya uchawi, unatamba ndani ya hemaya yako ukitoka nje unafyata mkia. Bongo tuna bidii sana ya kuiga vya wenzetu na kubatiza kuwa ni vyetu mfano Wa fleva, why not copy Zambians then?

      Delete
  21. TUNA SAFARI NDEFU.VIONGOZI WETU WA MPIRA NI MAKANJANJA MATUPU.

    ReplyDelete
  22. Kila kocha Tanzania atufai'' Siyo kweli hila ni majungu hatuangali hukweli huko wapi?Na pia Tanzania tunahamini uchawi sana ktk michezo na hata viongozi wetu pia wanahamini uchawi kwahiyo hatutafika popote hasa ktk michezo.Kinachotakiwa sasa Bongo wabadilishe mfumo wa kuchagua timu ya taifa siyo lazima wachezaji watoke Simba na Yanga.Ni nahamini Tanzania kuna wachezaji wazuri sana Mikoani ktk machuleni vyuoni na chuo kikuu.Pia hinatakiwa kuchagua wachezaji kutoka ktk machindano ya mikoani.Kwamfano mchezaji wazamani kama Chuma kutoka mtwara hakuwahi kucheza Simba or Yanga.Hinatakiwa kutafuta wachezaji wazalendo na pia wapatiwe pocho kwasababu hawa wachezaji wana familia zao .Kilakitu kiwe wazi kama hunachezea timu ya taifa pocho yako ya siku hitkuwa kiasi kadhaa mkifika robo fainali pocho hitaongezeka kiasi kadhaa and so on hutasikia sahingine wachezaji hawapewi posho zao

    ReplyDelete
  23. Ukweli ni hata mimi na wewe ambao ni Wadau tunachangia haya yote hapa nchini..ni mchango gani tunatoa katika kuendeleza mchezo..hao viongozi wa TFF sidhani kama wameshushwa toka mbinguni,ni sisi wenyewe tunawachagua sasa hapo ni nani kweli wa kulaumiwa..Tuache Unafiki wakati sisi wenyewe ni kati ya tatizo au hilo gonjwa sugu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...