Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Ghalib Bilal anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma yenye lengo la kukagua na kuhamasisha shughuli za Maendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema ziara hiyo inatarajia kuanza tarehe 14 Februari 2012 na atahitimishwa tarehe 17 Februari 2012.
Akiwa mkoani Ruvuma Mheshimiwa Makamu wa Rais atatembelea wilaya za Songea, Namtumbo na Mbinga. Wilaya ya Songea atapokea taarifa ya Maendeleo ya mkoa na pia taarifa ya Mkoa ya chama Tawala (CCM). Kazi zingine atakazofanya ni pamoja na kukagua Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Mheshimiwa Makamu wa Rais apata fursa ya kutembelea wilaya ya Namtumbo ambapo atapata taarifa ya mradi wa Uranium unaoendeshwa na kampuni ya Mantra Tanzania na atasilimiana na wananchi wa kijiji cha Likuyu Sekamaganga.
Akiwa wilaya ya Mbinga Makamu wa Rais atakagua shamba la mbegu bora za mahindi linaloendeshwa na gereza la Kitai kisha atakagua na kupokea taarifa ya mradi wa makaa ya mawe uliopo Ngaka na mwisho atasalimiana na wananchi wa Mbinga.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi siku ya Jumanne kumpokea Mheshimiwa Makamu wa Rais atakapowasili mkoani na kumshangilia atakapopita katika barabara kama ilivyo desturi wa wana Ruvuma
Imetolewa na :
Revocatus A.Kassimba
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...