Mheshimiwa Michuzi, pole sana kwa machofu ya safari. Nilikuwa na ombi dogo unibandikie hili dukuduku langu. Majuzi Jumamosi nilikuwa nimepaki mbele ya jengo jipya la Golden Jubilee Towers mtaa wa Ohio ambalo kwa sasa ndio jengo refu kabisa nchini nikagundua kitu ambacho inawezekana si muhimu sana ila mimi kilinitia hofu kidogo. 

Lobby ya hili jengo ipo level moja na parking ya nje pamoja na barabara, na kutoka parking kwenda ndani ya jengo hakuna kizuizi chochote cha maana. Nakubali kama sisi ni kisiwa cha amani lakini je wale ndugu zetu wa nchi za magharibi waliozungushia concrete blocks kwenye majengo yao ni wajinga? 

Kuna balozi nyingine wameweka mpaka matuta kwenye barabara zinazopita mbele ya jengo ili kupunguza uwezekano wa mtu au kikundi chechote chenye nia mbaya ya kutumia gari kama silaha kufanya ugaidi. Binafsi roho yangu itatulia zaidi kama kutawekwa vizuizi  ya jengo na parking/ barabara maana dunia hii wehu wamezidi na ni vizuri tukajihadhari kuliko kusubiri madhara. 

Vizuizi hivi vinaweza vikawa kama sehemu ya mapambo na kupandwa maua au miche ya miti mbalimbali. Nakushukuru kwa kunipa nafasi na nakutakia heri katika ujenzi wa Taifa - Mdau Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Wazo zuri.

    Hatari haiko kwenye ugaidi tu. Mlevi mmoja anaweza kuliachia gari huko atokako akazama na watu ndani!

    ReplyDelete
  2. Usalama ni muhimu kuzingatiwa!

    Wahalifu wengi hutumia hadi itikadi za Kisiasa na Kiimani ili kufikia lengo.

    ReplyDelete
  3. Mdau wewe kula ugali wako ukalale,maoni yako ni ya maana sana,lakini nchi ulio itolea hayo maoni, siyo, watu hapo wamekula hela, ukipewa ramani ya hilo jengo,mpaka hivyo vizingiti utaviona,lakini wala hela wamesha kula hela yake.

    ReplyDelete
  4. Looooh mdau nakupongeza sana kwa mawazo yako.Jambo uloliongea laaingia akilini.

    Tafadhali michuzi wafikishie ujumbe hao wahusika,bila shaka watapokea hilo wazo na kulifanyia kazi.

    Mdau wazo lako ni la kujenga sana yabidi watu walitilie maanani.

    ReplyDelete
  5. watu waovu ni waovu tu hata kama utajenga matuta au hivyo vizuizi unavyotaka waweke ,haitakupa usingizi mnono hata hivyo, je wakitumia ndege ? au wakimtumia mtu akavaa mabomu, sijakuona kama umekuja na solution babu kubwa ,mimi naona kama bado vile, je unaonaje kama watatumia security guard, binadamu akakaa pale masaa 24 yaani kwa zamu, na ndugu yako akapata ajira hapo-kuliko hayo matuta na maconcreate unayosema ?-Ulaya mbona hakuna hayo maconcreate ? ni kuchafua mazingira tu-wewe lala usingizi, acha presha ,maisha yenyewe ni mafupi haya. Ngwana Ndoho.

    ReplyDelete
  6. Ngwana Ndoho acha uzushi ulaya vizuizi vimejaa kibao tu kwenye majengo muhumu kuanzia hizo concrete unazosema mbaka vyuma..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...