Na Mary Ayo,Arusha

JAMII imetakiwa kuhakikisha kuwa inawajali na kuwathamini watoto wenye ulemavu kwa kushirikiana nao kwa kuwapatia haki za msingi sambamba na kuwajali kimaisha kwa kuwapatia elimu bora kwa kuwa nao wanahitaji haki sawa kama walivyo watoto wengine.

Ambapo watanzania wengi wamekuwa na mazoea ya kuwabagua katika mambo mbali mbali ya msingi kama vile elimu na mahitaji mengineo swala ambalo linawafanya wajione wametengwa na jamii inayowazunguka.

Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa kanisa la fpct bw. Elias Shija alipokuwa akiongea katika kikao cha wadau wa maswala ya mtoto na ulemavu ili kujadili kuhusu haki ya mtoto na kuanzishwa baraza la watoto wenye ulemavu kilichofanyika mjini hapa.

Alisema kuwa kwa sasa jamii ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa kila mtoto anayo haki sawa hivyo swala la watoto wenye ulemavu ni la kila mtu na sio la mtu mmoja kwa kuwa nao wako kama watoto wengineo. .

Aidha aliongeza kuwa wao kama kanisa wmaekuwa na nafasi kubwa ya kusaidia walemavu ambapo walianzisha programu ya huduma kwa watoto na vijana wenye ulemavu katika jamii kupitia mfumo jumuishi na endelevu ulioanzishwa kwa malengo ya kuboresha maisha ya jamii Tanzania.

Vile vile alisema kuwa ni vema makampuni na taasisis mbali mbali nazo zikajumuika na asasi nyinginezo katika kuhakikisha kuwa zinawapatia nafasi mbali mbali tu wenye ulemavu ili nao waweze kushiriki katika kazi za
maendeleo.

Hata hivyo alieleza kuwa lengo la watoto walemavu kuomba kanisa liwasaidie kuanzisha baraza lao ni ili liweze kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu na wenzao wasio na ulemavu katika baraza la watoto la taifa katika kupigania haki za mtoto ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera.

Amesema kuwa hadi sasa mabaraza ya watoto wenye ulemavu yamekwisha undwa katika mikoa ya tanga ,rukwa ,mwanza shinyanga na mara.

Kwa upandewake bw Gidion Mandesi amesema kuwa haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu ni muhimu kwa kuwa inasaidia kupunguza makali ya ulemavu,kuinua vipaji vyao na pia inawafanya wachanganyane na wenzao pamoja na kuwafanya wajitambua katika familia.

Aidha alivitaka vyuo vyote nchini vinavyofundisha ualimu kutambua mbinu nyinginezo mbadala za kufundisha wenye ulemavu ili waweze kuelewa kwa urahisi wawapo mashuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...