Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa meza kuu na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mh Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Mh Wilson Mkama kabla ya kuanza kwa mkutano wa Halmashauri Kuu leo katika jengo la White House la Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Sehemu ya wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM katika mkutano huo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI:
Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi imefanya kikao chake maalum chini ya Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 12.02.2012. Katika kikao hicho Halmashauri kuu ya Taifa pamoja na mambo mengine imeamua;
Kufanya Marekebisho ya Katiba ya CCM ya 1977, Toleo la 2010 na Kanuni zake.
Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhia marekebisho ya Katiba ya CCM ya 1977, toleo la 2010 hivyo kubadili namna ambavyo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inavyopatikana.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM watakuwa katika makundi yafuatayo:-
(a) Ngazi ya Taifa
Wajumbe 10 kutoka Tanzania bara
Wajumbe 10 kutoka Tanzania visiwani
(b) Wajumbe 10 wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa
(c) Wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao.
(d). Wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi
i. Wanaochaguliwa na Bunge 10 (Bara 8, Zanzibar 2)
ii. Wanaochaguliwa na BLW 5 (Zanzibar 5)
(e). Wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani.-221
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliochaguliwa kupitia Wilaya watakuwa ni Viongozi wa Kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa Wajumbe hao wa kuwa karibu na Wanachama na kushughulikia shida zao.
(f). Wajumbe toka kwenye Jumuiya za Chama
i. Wanaochaguliwa na UWT 15 (Bara 9, Zanzibar 6)
ii. Wanaochaguliwa na UVCCM 10 (Bara 6, Zanzibar 4)
iii.Wanaotokana na WAZAZI 5 (Bara 3, Zanzibar 2)
Aidha Halmashauri kuu ya Taifa imeamua kuwa Viongozi Wakuu Wastaafu Ngazi ya Taifa waundiwe Baraza la Ushauri.
Baraza hilo litakuwa na Wajumbe wafuatao:-
• Marais Wastaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walikuwa Wenyeviti wa CCM Taifa.
• Marais Wastaafu wa Zanzibar ambao pia walikuwa Makamu Wenyeviti wa CCM Taifa.
• Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Wastaafu.
Baraza litakuwa na kazi ya kutoa Ushauri kwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali zinazoongozwa na CCM, kwa madhumuni hayo hayo katika jambo mahsusi. Wajumbe wa Baraza hilo wanaweza pia kualikwa ama wote au mwakilishi wao kuhudhuria Vikao vya Chama Ngazi ya Taifa.
Imetolewa na:
Nape M. Nnauye.
Katibu wa NEC wa Itikadi na Uenezi

Wamejivua Magamba?
ReplyDeleteHoja:
ReplyDelete1. Wajumbe wa ngazi ya taifa watachaguliwa vipi?
2. Wajumbe wa kuteuliwa na rais wawe wanadhibitishwa na kikao kingize kama kamati kuu au hilo baraza la ushauri.
3. Wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao ni wapi? Wasije wakawa ni wakuu wa wilaya.
CCM Inatesa, kidumu chama cha mapinduzi.
Nape, tafadhali tueleze kujivua gamba kumefikia wapi?
ReplyDelete