MKURUGENZI wa uuguzi na Huduma ya Wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agness Mtawa (katikati), akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya kufuatilia mgogoro wa madaktari wakiongozwa na Mwenyekiti

wao, Mh Margaret Sita (kushoto). Kulia ni Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangwala na wa pili kulia ni Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile

MARGARET Sitta akimjulia hali Sada Imili, aliyelazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dar es Salaam, leo. Baada ya hoja ya mgomo wa madaktari kuibuliwa mara sita bungeni, Naibu Spika Mh Job Ndugai ameamua kwamba swala hilo lijadiliwe na kutafutiwa ufunbuzi - baada ya kamati hii kuwasilisha ripoti yake.


HABARI ZILIZOTUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA;

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YUPO DAR ES SALAAM KUTOKA DODOMA KUSHUGHULIKIA MGOMO WA MADAKTARI AMBAO UMEKUWA UKIENDELEA KWA LENGO LA KUUPATIA UFUMBUZI.

LEO AMEKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PAMOJA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA WASTAAFU.

KESHO SAA 3 ASUBUHI ATAKUTANA NA MADAKTARI BINGWA, MADAKTARI WALIOSAJILIWA (REGISTRALS) NA MADAKTARI WALIOKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS) NA BAADA YA HAPO SAA 4 ATAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD NA WAWAKILISHI KUTOKA HOSPITALI ZA MKOA WA DAR ES SALAAM, KWENYE UKUMBI WA CPL, MUHIMBILI.

MATARAJIO YA SERIKALI NI KWAMBA MAZUNGUMZO HAYO YATAWEZA KUMALIZA MGOGORO HUU NA MADAKTARI WOTE KUREJEA KAZINI NA HIVYO KUREJESHA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HALI YA KAWAIDA KWA WANANCHI WA TANZANIA.

HIVYO SERIKALI INAWAOMBA WOTE WANAOHUSIKA WAFIKE KATIKA MIKUTANO HIYO BILA YA KUKOSA.

                                                    (IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi Bunge linatusaidia vipi wananchi? Namshauri mtu anayefanya Masters degree in Political Science afanye thesis yake katika topic hii kama ataona inafaa. Ni vema tujue. Leo hii mtu akiniuliza kwa haraka haraka nitalikandia sana bunge, na ninaamini sio vema kwa sababu pengine sina uewelwa wa kutosha juu ya mchango wa bunge katika maisha ya Watanzania. Namaanisha mchango wa kivitendo na si wa kimaneno.

    ReplyDelete
  2. Acheni maaigizo jamani,watu wanakufa nyie mnapiga danadana tuuu! Najua si Serikali wala madaktari watapata ushindi kwenye hili zaidi kuleta maangamizi kwa jamii ya Watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...