“Ina thamani machoni pa Bwana, mauti ya wacha Mungu wake”. Zaburi 116:15
Leo ni miaka mitatu (3) tangu Bwana wetu Yesu Kristo akuite tarehe 4th Feb 2009.  Familia inamshukuru Mungu kwa kutupa muda wa kuishi nawe kwa kipindi chote ulipokuwa hai. 

Ilikuwa ni fahari kuwa na baba kama wewe, japo muda ulionekana  mfupi kuwa nawe lakini Upendo, malezi ya kimwili na kiroho, mafundisho, ucheshi wako hautasahaulika.

Daima utakumbukwa na mke wako, watoto wa kiroho na kimwili, wajukuu wa kiroho na kimwili, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu ana makusudi katika kila jambo, Jina la Bwana libarikiwe.

       “Maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu , Mungu atawaleta pamoja naye”. 1 Wathesalonike 4:14.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                    

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nyie mlimpenda lakini bwana alimpenda zaidi..Ila jamani ingekuwa vizuri mkatueleza ni Familia ya Mabondo wa wapi(sehemu,mji,mtaa nk) na si vibaya kutaja na majina ya mke,watoto,nk katika kipindi hiki cha kumbukumbu.Ni ushauri tu

    David V

    ReplyDelete
  2. Naona kama ni jana tu ulipoondoka baba yangu.

    ReplyDelete
  3. RIP Mchungaji, kwani ulikuwa na Upako wa kweli, na ulinitoa mapepo na sasa nimepona kabisaa RIP Amen!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...