Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Mh. Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa pamoja na Waziri kivuli Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekia Wenje wakiwa kwenye mkutano na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Ijumaa February 3, 2012 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
 Kaimu Balozi Mh. Lily Munanka (kulia) akiwa na Maafisa Ubalozi kutoka kushoto, Suleiman Saleh na Abbas Missana katika mkutano huo.
 Kutoka kushoto ni Maafisa, Brigedia jenerali Maganga, Mama Kiju na Suleiman Saleh wakiwa katika mkutano huo.
 Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe (CHADEMA).
 Kushoto na Dr, Switebert Mkama akiwa na Afisa Mindi Kasiga.
 Kushoto ni Afisa Edward Masanja akiwa na Afisa Agnes Lusinde.
 Kutoka kushoto ni Afisa Mindi Kasiga, Afisa Suleiman Saleh, Dr Switebert Mkama, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe, Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Ezekia Wenje, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu, Afisa Kiju, Kaimu Balozi, Mh. Lily Munanka, Afisa Abbas Missana, Afisa Agnes Lusinde, Afisa Edward Masanja na Brigedia Jenerali Maganga wakiwa katika picha ya pamoja.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akisaini kitabu cha wageni.
 Kiongozi kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe akisani kitabu cha wageni.
Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiamtaifa, Mh. Ezekia Wenji akitia saini kitabu cha wageni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wameenda kufanya nini huko US?Kufanya mkutano na maofisa wa Ubalozi wa TZ tu?Sikuelewa vizuri maelezo ya huu msafara

    David V

    ReplyDelete
  2. Tanzanians loves sitting around tables discussing things and looking important. But nothing ever changes.

    ReplyDelete
  3. Wabunge na mawaziri wapo nje ya nchi kuhudhuria sala na chakula cha asubuhi(Breakfast) na Obama. Nyumbani wameacha matatizo, mfumuko wa be (inflation), Madaktari kugoma hayo ni machache tu! Serikali imetumia kiasi gani cha fedha kutuma hiyo deligate kuhudhuria kula chakula cha asubuhi na Obama, wakati muda sio mrefu serikali iliwatuma wajumbe sijui wangapi kwenda Uswiss na kila kichwa kililipiwa zaidi ya $40000 elfu arobaini, serikali inalalamika haina pesa kutuma kwenye halmashauri zake, shughuli nyingi zimesimama! Tanzania sasa hivi tunapaswa kufunga mikanda na kuacha kutumia pesa tusizonazo! Huu ni ufujaji wa mali ya umma! Tuache matanuzi na kungalia mambo muhimu yanayoikabili Taifa.

    ReplyDelete
  4. CDM naona wananenepa sasa haaa haaaaaa. haya ndo mambo hapa ahh wako kimyaaaaaa

    ReplyDelete
  5. Tanzania inajengwa na wenye nguvu na kutafunwa na wenye meno kama huna meno kaa kimya. Sisi tuko DC tunabaridhi ni kiwinter , ngoja niingie mtaani nikapige shopingi

    ReplyDelete
  6. mbona muislam mmoja tu ktk kundi lote ilo????????????????????

    ReplyDelete
  7. Mbowe mtoto wa CCM kabisa huyu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...