Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiongea wakati wa Sherehe za kumbukumbu ya Mashujaa wa vita ya Majimaji iliyoadhimishwa jana mjini songea.Kushoto ni Kkatibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi na Kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel Zullu.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanal Mstaafu Joseph Simbakalia akiongea na wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji yaliyofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini humo.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi. Maimuna Tarishi na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi akiongea na wakazi wa manispaa ya songea kwenye maadhimisho ya kumbukmbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini songea jana.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu na kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel Zullu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiweka ngao na mkuki katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini songea.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi,Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoani Ruvuma,Alhaji Mustafa Songambele na Mkuu wa Zamani wa Mkoa wa Ruvuma,Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo wakiinua mikono juu ikiwa ni ishara ya kuomba dua kwa Mashujaa wa Vita ya Majimaji wakati wa maadhimisho ya Mashujaa hao mjini songea jana.
Baadhi ya wazee wa kabila la wangoni wakiwa wamevaa mavazi mfano wa yaliyokuwa yakivaliwa na machifu wa kabila hilo wakati wa ukoloni kabla ya vita vya majimaji kwenye mahadhimisho ya sherehe za kumbukumbu za nmashujaa hao jana mjini songea.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.
Mbona hawawataji mashujaa wenyewe. Nasikia shujaa mkubwa alikua Ali Songea Mbano ambaye wajarumani walimyonga na kumzika karibu na shimo walimozikwa kwa pamoja mashujaa zaidi ya 60 wa majimaji. Nisahihisheni kama nimekosea. the germans were/are terrorists.
ReplyDeleteNa mimi nilisikia kwamba eti nasikiri kwamba wengi katika hao waliokuwa wakiupinga ukoloni na ambao walianzisha vita vya maji maji walikuwa waislamu ila walipokuwa wananyongwa walilazimishwa kubatizwa wakati wa kunyongwa. eti kweli jamani tuelezeni watoto hatujui mambo haya. Lakini suala wakiwa wamebatizwa au la bado ni wananchi wa nchi na wamefanyiwa unyama. Hawa wakoloni walikuwa wakatili sana.
ReplyDeletewalikuwa wengi wakina mpambalioto/chabuluma/zamchaya songea /magoha nawengine wengi
ReplyDeleteHao ndio walikuwa wazalendo wa kweli wakiipigania nchi hadi kufa.
ReplyDeletesio siku hizi vibaka, vicheche na mijambawazi kila kona.