Kwa watanzania wote wa Washington DC na vitongoji vyake na wale wa miji mingine waliosaidia; Kwa niaba ya mume na familia ya marehemu Christavina, ninapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliohudhuria na kushiriki katika harambee ya mazishi ya Christavina. Mungu awabariki sana na awazidishie. Pia, tunapenda kutoa shukrani kwa washiriki, waimbaji na wachungaji wa The Way of Gospel Ministries kwa ukarimu wao na moyo wao wa upendo.

Kwa kifupi Harambee ilifanikiwa sana. Jumla iliyopatikana ni kama ifuatavyo:
Pesa (Cash) $4,421
Hundi (Checks) $3,250
Ahadi (Pledges) $1,520
Jumla $9,171

Kwa mara nyingine, tunashukuru sana.

Kwa wale ambao bado wangependa kusaidia zaidi, tafadhali wanaweza kufika mume wa marehemu, anwani ni 3237 75th Avenue, Apt 201, Landover (or Hayattsville), MD 20785. Tupo kila siku jioni kuanzia saa 12 (6pm). Kwa wale wa mbali, bado tunapokea michango kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing # 255071981. Jina la Account ni Lavorn Cryor.

Mipango ya mazishi ni kama ifuatavyo:
Misa ya kumuaga marehemu itafanyika Jumapili Februari 19, saa 4 asubuhi (10 am) katika kanisa la Takoma Park Seventh Day Adventist, lililoko 6951 Carroll Avenue, Takoma Park, MD 20912. Misa hiyo itamalizika saa 6 mchana (12 noon). Baada ya hapo tutarudi nyumbani kwa mume wa marehemu kwa chakula cha mchana. Mume wa marehemu ameomba, kwa heshima, mwili wa marehemu usipigwe picha. Tutashukuru kwa hilo.

Mazishi yatafanyika Jumatatu Februari 20. Tutakutana kwa marehemu saa 2 asubuhi (8am), na saa 2.30 (8.30) tutaelekea J.B Jenkins Funeral Home iliyoko 7474 Landover Rd, Landover, MD 20785. Pia Unaweza kwenda J.B Jenkins Funeral Home moja kwa moja.

Tutaondoka J.B Jenkins Funeral Home saa 3.30 asubuhi (9.30 am) kuelekea makaburi ya Gate of Heaven yaliyoko 13801 Georgia Avenue Aspen Hill (wakati mwingine GPS itaonyesha Silver Spring), MD, 20906.

Asanteni sana na tunamtakia mpendwa wetu Christavina, pumziko la amani.

Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile(240.938.3177); Teddy (301.254.4169); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au Rebecca(240 898 7161).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. michuzi na kikosi chako cha kazi ni vyema kabla ya kuweka matangazo mngelikuwa mnayapitia kidogo kwa ukaguzi

    kwa mfano hiyo picha haijafaa kuwa picha ya kutangaza msiba wahusika wanapaswa kuchagua kati ya picha za marehemu zenye muonekano wa kawaida na sio hiyo

    poleni sana wafiwa ndugu na marafiki

    mola ilaze roho ya marehemu pema peponi ameen.

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa kwanini mmewe akatae mkewe asipigwe picha za kumbukumbu?na kwa nn wasimlete nyumbani $9000 ingetosha kumleta mpendwa wetu nyumbani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...