Na Woinde Shizza Arusha
Mahakama nchini zimetakiwa kutoahirisha kesi mara kwa mara ikiwa hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo kwa kuwa inachelewesha wahusika kupata haki zao kwa wakati.
Hali hiyo inatokana na mahakama nyingi hapa nchini kuahirisha kesi mara kwa mara bila sababu za msingi hali ambayo haileti tija kwa wenye kudai haki.
Hayo yamesemwa na Jaji Mkuu wa Tanzania,Othman Chande wakati akifungua mkutano mkuu wa chama cha wanasheria Tanzania bara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa(AICC) mkoani Arusha.
Jaji chande amesema kuwa kesi zinaweza kuahirishwa ikiwa kuna sababu za msingi kama msiba au wakili ambaye yupo katika kesi hiyo ana kesi nyingine lakini sababu nyingine ambazo si za msingi zisisababishe kesi kuahirishwa ili kesi hizo zimalizike kwa wakati.
Pia Jaji chande amesema kuwa kuna changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wananchi wenye uwezo wa kawaida kupata haki yao ya msingi ya wakili pindi wanapokuwa wanakabiliwa na kesi kubwa kama ubakaji ambazo adhabu zake ni kubwa kama vile kifungo cha maisha ambapo walitakiwa kupata mtetezi lakini kutokana na mawakili wa serikali kuwa wachache wanakosa huduma hizo.
"napenda pia kuwahasa hawa mawakili kuwa katika kazi yao wasiangalie jicho la mteja tu bali waangalie na upande wapili kwani watu wote tunafanya kazi kwa pamoja"alisema Chande
Kwa upande wake Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika Francis Stola alisema kuwa mkutano huo ni wa kutathimini utoaji haki na majukumu ya mahakama ambapo ameiomba serikali upande wa mahakama kutenga fungu la fedha za kutosha ili mahakimu na majaji waweze kufanya kazi zao kwa umakini zaidi.
Hata hivyo amesema kutokana na kukosekana kwa fungu la fedha la kutosha hali hiyo inapelekea wanasheria wengi kupokea rushwa na kupelekea haki kupotea kwa wananchi ambao waniotegemea mahakama.
Aidha stola ameeleza kuwa kukosekana kwa vitendea kazi kama maktaba na kukosekana kwa vitabu vya sheria ni tatizo pindi mahakama inapotaka kutoa maamuzi.
Alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili baadhi ya changamoto ambazo wanakutana nazo ikiwa ni pamoja na kujadili jinsi ya kuzuia rushwa katika mahakama mbalimbali ,jinsi ya kukarabati majengo ya mahakama pamoja na jinsi ya kuwasaidia wananchi wa kima cha chini jinsi ya kutatua kesi zao.
Stola alisema mada ambazo zitakazotolewa kuwa ni pamoja na mfumo wa uendeshaji wa kesi za madai,njia gani iweze kutumika ili bunge liweze kutunga sheria ambazo zitakuwa bora,mfumo wa uwendeshaji wa kesi a jinai na nyingine nyingi.
mkutano huo unatarajiwa kumalizika kesho ambapo wanasheria kutoka Tanzania bara wameshiriki ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na mchango wao ili wananchi wenye uwezo wa chini wanapatiwa haki zao.
Aidha Allitaka serekali kuwapa nafasi wananchi katika swala zima la katiba mpya na watoe fursa kwa kila mwananchi kuchangia katiba hiyo.
"ili katiba iwe katiba ni wajibu wa kila mwananchi kuchangia maoni yake hapo ndio tutaiita katiba tofauti na hapo kwakweli sijui"alisema Stolla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...