Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mtaro wa kupitishia maji ya umwagiliaji katika Kilimo mradi uliopo katika Kijiji cha Kisegese, wakati akiwa katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya Mkoa wa Mbeya
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi katika chanzo cha mradi wa maji ya umwagiliaji katika Kijijji cha Kisegese, Wilaya ya Rungwe mtaro wenye urefu wa Kilomita 7, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbey
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, wakiangalia Mpunga katika eneo la Shamba Darasa, lililopo Kijiji cha Kisegese Wilaya ya Rungwe
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Mkuki na Vazi rasmi la heshima la Kabila la Wanyakyusa, baada ya kukabidhiwa wadhifa huo na wazee wa Kabila la Wanyakyusa wa Kijiji cha Mbambo Wilaya ya Rungwe, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea  Mkuki kutoka kwa mwakilishi wa Wazee wa Kabila la Wanyakyusa wa Kijiji cha Mbambo Wilaya ya Rungwe, Ambakisye Mwakatobe, ikiwa ni ishara ya kumkabidhi wadhfa wa kuwa Mzee wa Kabila la Wanyakyusa, wakati alipofika katika Kijiji hicho kuwahutubia akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana Februari 26, 2012. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hawa ndugu wa Mbambo nimependa mawazo yao walivyomkaribisha Makamu wa Rais.

    Wamempa vazi rasmi la kabila la Wanyakyusa kwa heshma yake,si kama wengine wanaowapa viongozi uchifu wa kabila fulani.Hii ni matusi,hawezi kila mtu tena wa kabila lingine akawa chifu wa kabila lingine eti tu kwa kuwa ni kiongozi.

    Wa Mbambo wameiweka vema.Au ni mwandishi ndo kaiweka vema!Siku zingine labda ni waandishi tu wanaikosea!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...