Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisamiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma,Michael Kamuhanda wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa mjini Songea mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu (kushoto) akikabidhi taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Meneja wa wakala wahifadhi ya taifa ya chakula kituo cha Songea,Morgan Mwaipyana (kushoto) akimkabidhi Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal taarifa ya kituo hicho ambacho hadi sasa kinakabiliwa na upungufu wa fedha za kununulia mahindi ya wakulima ambayo bado yapo majumbani kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma.
Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal akizungumza na wakazi wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma katika viwanja vya manispaa ya Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu akitoa taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal (hayupo pichani) katika viwanja vya ikulu mjini Songea.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu (wa pili kushoto) akimuonesha Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal (katikati) moja ya maghala ya kuhifadhia mahindi katika kituo cha wakala wa hifadhi ya chakula ya taifa kituo cha Songea.
Meneja wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula kituo cha Songea,Morgan Mwaipyana (kulia) akimueleza jambo Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal (kulia) juu ya  kukosekana kwa maghala ya kutosha ya kuhifadhi mahindi ambapo hadi sasa yaliyopo yanauwezo wa kuhifadhi tani 26 huku kiasi walichonacho ni zaidi ya tani 40.PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII,RUVUMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. jama kama sura kama nyerere sijui na vitendo vyake viko hivyo hivyo

    ReplyDelete
  2. Sikujua kwamba ndege bado ndege zinatua uwanja wa ndege wa Songea. Toka Air Kamata (au Air Dala Dala) ilipozorota basi.

    ReplyDelete
  3. Wewe mwandishi umekosea jina la mke wa Mh. Bilal anaitwa Zakhia na hajaongeza, hebu rekebisha kabla sijakasirika.

    Abiola Jr.
    Mafia kiduka cha Juice

    ReplyDelete
  4. Ziara ya Kiserikali, Magwanda ya Magamba ya nini? Tuelimike.

    ReplyDelete
  5. Anony Wed Feb 15, 05:32:00 AM 2012, tangu lini Zakhia akatabasamu?

    ReplyDelete
  6. wewe Abiola wa Mafia kiduka cha juice wacha ujuaji, mwandishi yuko sahihi huyo ni Asha Bilali mke wa pili wa Makao wa Rais na mke wa kwanza ni Zakia Bilal......ona watakucheka watu kujifanya unajua sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...