Mary Ayo ,Arusha
MAMLAKA ya mapato Tanzania(TRA)imeanzisha utaratibu wa ukusanyaji kodi shirikishi kwa kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara nchi nzima,ikiwa ni mkakati wa kuongeza mapato ya serikali bila shuruti
.Aidha mkakati huo ambao umeanzia katika mikoa ya kandaya kaskazini,unalenga kuwafanya wafanyabiashara waelewe kuwa TRA ni rafiki ya mlipa kodi na kwamba kulipakodi bila shuruti ni wajibu kwa
maendeleo ya taifa.
Meneja wa mambo ya ndani ,ofisi ya kamishina mkuu wa TRAnchini,Stela Cosmas aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na chama cha wafanyabiashara mkoani ArushaTCCIA,katika mkutano uliofanyika katika hotal ya Golden Rose jijini hapa.
Alisema kuwalengo la TRA kukutana nawafanyabiashara,ni mwendelezo wa kushirikiana na wadau katika utoaji wa elimukwa mlipa kodi,kujenga uaminifu kwa mamlaka zake ,kumjulisha haki ,wajibu wamlipa kodi na kutambulisha sera mpya yamamlaka ya mapato katika kupambana na rushwa.
Cosmas aliwataka wafanyabiashara kufuata taratibu nakanuni za mlipa kodi ikiwemo kutoa stakabadhi zilizosahihi kwa wateja wao kuwasilishamalipo ya kodi sahihi,ritani sahihi, nyaraka za forodha na madai ya marejesho ,kutoa na kudai stakabadhi /ankra za kodi.
Aidha alito wito kwa wafanyabiashara kuepuka ukwepajikodi kwa kutumia risiti,ambapo alidai yakuwa wafanyabiashara wamekuwa na tabiaya kumwandikia mteja risiti yenyekiwango tofauti na iliyopo kwenye kitabu chake cha mauzo,kwani kwa kufanyahivyo ni kuinyima serikali mapato na ninikinyume cha sheria.
Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Arusha,EvaristKileva alisema kuwa, wajibu wao kama TRA ni kuhakikisha kuwa wanahamasisha walipa kodi kulipa kodi kwa wakati kwa ajili ya manufaa ya watanzania kwa ujumla .
Kileva alisema kuwa wadau wakuu wa TRA ambao niwalipa kodi wanapaswa kuhudumiwa kwa umakini mkubwa bila kuwepo kwa malalamikoyoyote kati yao na mamlaka husika ambapo alisema endapo kutakuwepo na kutokuelewanakati yao na wafanyakazi wa TRA wawakilishe malalamiko yao kwa meneja mwenyeweili yaweze kuchukuliwa hatua.
Aliongea kuwa, ni vizuri walipa kodi wakawa na mahusianomazuri kati yao na mamlaka ya mapato ili kuboresha huduma zinazotolewa bilakuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ikiwa ni pamoja na walipa kodi kujijengea tabia ya kuwasilisha malalamiko kwa wakati na kwa mamlaka hiyo na sio nje yahapo huku lengo hasa likiwa ni kuendelea kudumisha mahusiano mazuri .
‘’ndugu zanguwafanyabiashara ofisi yetu ipo wazi kila siku kwa ajili yenu tafadhili kamakuna matatizo yanajitokeza msikumbatie malalamiko leteni ofisini’’alisemaKileva
.Kwa upande wake ,mwenyekiti wa chama cha wafanyabiasharamkoa wa Arusha(TCCIA),Adolf Olomi pamoja na kuipongeza TRA kwa uamuzi wake wakutoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara,alisema itasaidia kuongeza uelewa na punguzaukwepaji kodi kwa baadhi yao na kujenga mahusiano yenye tija na TRA.
Alisema kuwa, elimu hiyo imeweza kuwanufaisha kwa kiasikikubwa sana kwani hapo awali walikuwa hawana uelewa wowote jinsi ya kuwahojiwatendaji wa TRA pindi wanapofika katika maeneo yao kwa ajili ya kudai kodi.
Alifafanua kuwa kupitia mafunzo hayo yamewawezesha kwakiasi kikubwa sana kuwa na mahusiano mazuri kati yao na mamlaka hiyo ,pamoja nawatendaji wa mamlaka kwa ujumla kwani wataweza kufanya kazi kwa ushirikiano wahali ya juu tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Safi sana TRA kwa mbinu bunifu za ukusanyaji mapato, lakini kwanini msije na mbinu bunifu za matumizi ya hayo mapato? Katika nchi corrupt kama Tanzania, tatizo sio tu ukusanyaji wa mapato, bali na matumizi ya mapato.
ReplyDelete-Ishaurini serikali kuacha kununua magari ya kiafahari kama v8, mbona rwanda wameweza?
-TRA, mje na mkakati kuwa 0.001% ya makusanyo yenu kila mwezi, yakanunue magodoro na vitanda mahosipitalini ili kina mama wasijifungulie chini.
-Kila mnapofanya mnada wa magari yalioshindwa kulipa kodi, mnatoa japo gari 2 tu ili zikasaidie mahosiptali as ambulance.
-Njooni na mafunzo shirikishi kwa serikali na taasisi zake kuacha kulipana posho zisizo na tija..!
Kibanga Msese
Kaka michuzi, wacha ni weke kaujumbe kangu hapa ,sasa wewe kaweke vizuri sehemu yake, MIMI kama mlipa KODI bila shurutishi, kwa kupenda nchi yangu,ni mjasilia mali mzalendo, nahangaika nakujituma zaidi ya hawa wachina unaowaona kariakoo,nina kimgahawa hapa Magomeni naamuka usiku saa 10 kwenda Mabibo kila siku kufuata ndizi na viazi ili niwapikie na kuwalisha watanzania wenzangu, jamani , nimeletewa bili ya million 19 na baada ya kwenda na risiti zote za mwaka mzima ninazolipia kila mwezi na kuwalalamikia wahusika, leo umeme tanesco wamekata kabisa aa giza tupu kwangu, na bili ya mwezi huu nimelipa na sina deni, ndugu zangu wapenda amani hii kweli ni HAKI ?? mgahawa na bili ya million 19 wapi na wapi ??? jamani nisaidieni ?? nikimbilie wapi ?? kupata huu msaada, je ?? haki ya mnyonge iko wapi hapa kwetu ?? kwa nini Tanesco wasiige mfano wa TRA kuwapenda wateja wao na kutufanya tuwe marafiki zao madala ya kuwa maadui zao ?? je tumekosa nini ?? bili zote za kila mwezi tumezitunza na hatudaiwi, sasa kutukatia umeme na kututia hasara ya kutupa nyama na kuku kwenye mafriza yetu !! hii hasara nani atatulipa ?? MUNGU wangu wee !!! tuone na sisi wanyonge wako, tunanyanyasika katika nchi tuliyozaliwa , kila tukifurukuta tunakumbana na virungu vya hao waliokwenda chuo kikuu kutafuta kazi za kalamu, ili wajenge haraka haraka ,kama hivi sasa sufuri zimeongezwa hadi kufikia million 19 hii ni bili ya mwezi mmoja, ni mwaka mzima sasa bili yetu huwa laki 6 au laki 7 kila mwezi na kila mwezi tunakwenda kulipa -hata siku moja ya Mungu hatujakosa, ndugu zangu mlioko majuu na sisi tuliopo hapahapa nabaki africa nawaombeni mchango wenu wa mawazo, je ?? niende moja kwa moja kwa Ngeleja au nikapige hodi kwa Kikwete ?? au kama kuna wakili wakujitolea aishike hii kesi yangu twende huko mahakamani, niwa shitaki tanesco kwa hasara hii tukishinda kesi na nikilipwa basi wakili atachukua 30 percent yake , je wazo ZURI ?? Meneja Kipara
ReplyDelete