Katibu Mkuu aliemaliza muda wake Mhe. John Cheyo ambae pia ni Mwenyekiti wa PAC nchini Tanzania akizungumza machache mbele ya Naibu Spika. Mhe. Cheyo alikuwa ni Katibu Mkuu kwa muda wa miaka sita katika umoja huo.
Naibu Spika akifurahi jambo na viongozi wa Chama cha Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati za Hesabu za Serikali za Nchi za SADC (SADCOPAC) walipomtembelea leo katika Ofisi ndogo za Bunge Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mwenyekiti mpya wa chama hicho Mhe. Fish Mahlalela kutoka Afrika Kusini, wa pili ni Mhe.Webber Chinyadza kutoka Zimbabwe ambae ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, wa tatu kulia ni Mhe. Prince Maele kutoka Botswana ambae ni Katibu Mkuu Msaidizi, Wa nne kulia ni Mhe. Agnes Tjongarero kutoka Namibia ambae ni Makamu Mwenyekiti. Ujumbe huo upo nchini Tanzania kukutana na Sekretarieti ya Chama hicho ambayo iko katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu nchini (CAG).
Picha ya pamoja baina ya Naibu Spika na ujumbe mzima wa Uongozi wa SADCOPAC uliomtembelea Mhe. Naibu Spika Ofisini kwake hivi leo. Picha zote na mdau Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...