Ingawa Onyo la kimaandishi linaweza kuwepo kuweka tahadhari ya uegeshaji magari, lakini nahisi bado Tanzania, hususan Dar es Salaam bado hatujafikia kutoa tenda za kibinafsi kwa mtu au watu wachache kuzuia na kuwabana wenye magari na kuzuia magari yao kwa kuwatoza pesa ambayo kipato cha mwenye gari hilo hakimtoshelezi haja yake yeye binafsi na hata familia yake.
Nimeanisha kwa kusema BADO hatujafikia hatua hiyo ni kwasababu ya miundo-mbinu (infrastructure) ya usafiri wa magari jijini bado hauturuhusu kuwabana watu ili waweze kutumia usafiri wa madaladala, taxi au vibajaji ambazo zinafanya kazi kubwa na msaada kwa serikalil kuinua uchumi, lakini pia zimebanwa kimiundo-mbinu.
Mwaka jana ilipendekezwa uzuiaji wa uegeshaji magari uendelee kutanuka nje ya katikati ya jiji mpaka maeneo ya nje kuelekea Ilala mpaka Buguruni, Magomeni mpaka Ubungo na kadhalika. Uzuiaji huu wa uhuru wa kuegesha magari mjini (kwa sababu nilizozielezea hapo juu) utasababisha kupunguza kasi ya uchumi wa mji wa Dar es Salaam pamoja na uchumi wa taifa.
Ingawa uzuiaji wa magari huu unaleta ajira kwa baadhi ya watu ambao malipo yao ni kidogo, na ugawaji wa hayo mapato yanayopatikana hayakidhi kuleta maendeleo ya miundo-mbinu, mapato haya ni faida ya wachache, lakini athari yake ni kubwa kwa mtazamo wa mbali kwa wananchi kwa ujumla na taifa ambalo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana kupita miundo-mbinu iliyopo sasa.
Kuna sehemu hifadhi (conserved areas) ambazo sheria hizo zinaweza kuwepo na kuendelea kuwepo kwababu mbalimbali ambazo baadhi ya sehemu hizo hivi sasa sheria hizo zipo kama vile maeneo ya Ikulu, n.k., lakini kwa ujumla mwisho wa yote kitu ambacho mimi ninachopendekeza ni kufaidika kwa muwekezaji, mtoa tenda, mpewa tenda, mwananchi/mzawa na taifa kwa ujumla.
Samahani kama nimekosea.
Ndugu yenu,
Saleh Jaber.
HUYU AJUI KUSOMA WALA KUANDIKA
ReplyDeletePamoja na kwamba mdau amegusia suala la parking, inabidi hatua madhubuti zichukuliwe kuweka sehemu maalumu za parking. Maana kama sehemu ni chache unakuta jamaa wanaovaa reflector za kijani wanatafuta pesa kwa nguvu, kama huna ya faini, uwape nusu!
ReplyDeleteNa wale wa orange wanakata tiketi 3 na kuchukua za 4, tabia hii ni sehemu nyingi za jiji!
Siono mistari miwili wala alama ya NO PARKING kwa mujibu wa sheria za barabarani. Kauli ya mwenye duka hapo siyo sheria na aliyepaki hakuvunja sheria yoyote. Dereva una haki ya kumfikisha mahakamani aliyeweka hilo chuma kwenye gari lako.
ReplyDeletewatanzania tuweni makini sana tusiropokwe tu, huyu alieandika hapo no parking ni mtu wakawaida mwenye duka lake tu hapo
ReplyDeletesasa je kila mtu atakapoandika hivyo mbele ya duka au nyumba yake ndio iwe tayari ishakuwa sheria ya usalama barabarani hapo
tusiwe wapumbavu kwakila kilichoandikwa ndio mtu asifanye*** suala ni nani kaandika hapo iwepo alama maalumu ambayo inatambulika kwa kila mmoja na hata unaposoma kwenye kitabu cha sheria za usalama wa barabarani hukuti mwandiko wakipumbavu ulioandikwa hapo