Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Bi. Terezya Huvisa pamoja na ujumbe kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma wakiwapokea wageni katika uwanja wa ndege wa Kigoma, ambao ni Waziri wa Elimu ya Msingi na Mazingira wa Zambia Prof. Nkandu Luo (wa pili kulia) na Balozi wa Congo Nchini Tanzania Bw.khalfan Juma Mpango (wa kwanza kushoto). Ugeni huo upo Nchi kuhudhuria Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Bi. Terezya Huvisa (wa pili kulia),Waziri wa Elimu ya Msingi na Mazingira wa Zambia Prof. Nkandu Luo(wa kwanza kulia) na Balozi wa Congo Nchini Tanzania Bw.khalfan Juma Mpango wakiangalia ngoma ya Warumba - mayanga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani kigoma. Ugeni huo upo Nchi kuhudhuria Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika. (Picha na Ali Meja)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Safi sana,picha ya kwanza kwenye 'background' naona kama ndege ya ATCL?.Nimeipenda hii..hivi ndivyo tunavyoweza kulifufua shirika letu..Misafara mikubwa kama hii ya serikali tutumie ndege ya?/za ATCL.

    David V

    ReplyDelete
  2. Kichwa cha habari kinamaanisha waziri mmoja anatumikia Zambia na Congo kwa pamoja.

    ReplyDelete
  3. Tujitahidi Air UDA iwe ni ndege anayeruka kwa mbawa zake (Air Tanzania kamili) na badala ya kuwa 'Air Mbuni' ndege asiyeweza kuruka kwa kutumia mbawa zake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...